Ufafanuzi wa UDART tukio la abiria kupanda mwendokasi bila kufuata utaratibu

Ufafanuzi wa UDART tukio la abiria kupanda mwendokasi bila kufuata utaratibu

Masaa mawili hukuwa na haraka, kuna option za bajaji, daladala unaunga unga mpaka unafika kuliko kusubiri.
Muwe mnatuambia ukweli kuwa tusikate tiketi bali tupande bajaji na kuungaunga safari. Siyo tunakata tiketi halafu mabasi hamleti
 
Kwamba ajali ndio ilisababisha? Na kwamba ni kitu cha siku moja tu na kilidumu dakika 20 pekee? Haahaaa hii nchi ya ajabu sana, nilitegemea nione barua za kujiuzulu kumbe kujitetea!! BRT is a failure yaani wateja wa kumwaga ila mabasi hamna, hizo hela mnapeleka wapi?
Na hata samahani hayaombi kwa usumbufu yanayo sababisha. Pambavu zao
 
🛑 TAARIFA KWA UMMA KUTOKA UDART KUHUSU UFAFANUZI JUU YA TAARIFA YA TUKIO LA ABIRIA WA MABASI YAENDAYO HARAKA KUPANDA PASIPO KUFUATA UTARATIBU
View attachment 3415398
Toka mwaka juzi 2023, nilipoona changamoto kama hiyo, nakata tiketi nasubiri dakika 30, na likija linakuja limejaza. Nikaacha kupanda 'Mwendo Pole' nikarudi huduma ya Bolt nikiwa na haraka.
 
Nanukuu. Kutokana na uchache wa mabus mwendokasi kama ilivyotajwa na mtoa huduma. Kwa nini serikali isiluhusu wamiliki binafsi Waingia pia kutoa huduma hadi apo tatizo la uchache wa mabus ya mwendokasi litakatatuliwa na mtoa huduma. Tushee mawazo.
 
Hayo majibu ni mepesi sana, kila mara tunaona humu, picha na video za abiria wakihangaika na hayo mabasi. Kila siku mabasi mapya yanatokea mbinguni? Kwanini mnasumbua watu na wanalipa kodi.

Wanaandika kama wamekatwa vichwa, eti vyombo vya moto, visiingilie njia ya mwendo kasi. Mnawajua wanaoingilia hizo njia, watu binafsi ni wachache, magari yote ya Serikali ndiyo njia yao walimeni barua. Kiufupi huo mradi mpaka saaa umekufa kama mingine tu.
 
Back
Top Bottom