Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Mkuu Kifyatu kuna chombo kilitumwa Jupiter kinategemewa kuwepo kwa miezi 18 toka kimefika huko!!.
Nini wanategemea kugundua toka kwenye icho chombo...
Kwa nini ni mission ya miezi 18 wakati chombo kimetumia miaka 4 kusafiri toka Duniani mpaka Jupiter???

Kama nilivyozungumza hapo awali Jupiter ni sayari kubwa na yenye magnetic fields na radiation kubwa sana. Hii ni mara ya kwanza kwa chombo kutumwa kwenda kuizunguuka (hasa mizunguuko hiyo kupitia north na south poles zake. Sehemu hizi ni hatari sana radiation zake.) ili kujifunza kiundani sayansi ya Jupiter. Kujua kama Jupiter ina solid core, maji, amonia, n.k. ni muhimu kujua Jupiter ilivyoanza na hatma yake.

Zaidi ya hizi sensors zinazoichunguza Jupiter kiundani pia itapiga picha za rangi na kurekodi sauti ili sisi wengine tuweze kufuatilia hii mission. Juno mission inategemea kuizunguuka Jupiter mara kama 37 hivi. Hii ni kwa sababu inategemea kupaa chinichini sana na pengine ikazidiwa na radiations na electro-magnetic fields na kuangukia ndani.

Unaweza kupata taarifa nyingi tu kwenye internet. Fuatilia kwenye tovuti za NASA kama hizi hapa chini.

https://www.nasa.gov/feature/jpl/nasa-s-juno-spacecraft-sends-first-in-orbit-view
Juno
Latest News About the Juno Mission to Jupiter | NASA Solar System Missions, Space Probe to Outer Planets
 
hivi hizo telescope za kutazamia angani tanzania hii zinapatikana?
 
Actually, unaweza kutumia binoculars za kawaida tu pamoja na filter (kama vile vioo vya welding) na unaweza kuiona Venus au Mercury ikipita kwenye uso wa jua.
 
Jua ni star ndiyo lakini siyo the biggest star mkuu!Ila jua ni nyota iliyo karibu zaidi na dunia

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Jua ni biggest star katika milk way galaxy ambapo jua ni miongoni mwake(the sun is a part in the milk way galaxy). Lakini tuna polinganisha na star zingine zilizopo katika galaxy zingine kama wachangiaji wengine walivyosema kama vile SAYANSIKIMU ndipo tunakataa kwamba jua si kubwa kuliko baadhi ya star zingine katika galaxy hizo.
 
Jua sio the biggest Star on the Milk Way Galaxy. Bado ipo kijana haijafikia hata stage ya Yellow Giant na Red Giant. Kuna star (jua) kubwa ambalo hili jua la solar system yetu linakuwa dogo kama dunia na jua letu.

Joris ndio the biggest star(jua) iliyoweza kuonekana kwa Telescope mpaka sasa. Ni kubwa mara bilioni ya jua letu.

Actually, unaweza kutumia binoculars za kawaida tu pamoja na filter (kama vile vioo vya welding) na unaweza kuiona Venus au Mercury ikipita kwenye uso wa jua.
mkuu hii dark matter na dark energy katika universe vinanichanganya kidogo.. ni vitu gani hivi na imejulikana vipi kwamba ndio vinavyochukua nafasi kubwa katika huu ulimwengu??? nisaidie hapo mkuu kifyatu
 
Wanasayansi wanapoiangalia universe yetu na galaxies zake zote (zinavyokimbiana) wanafanya mahesabu kujaribu kuelezea ni nini kinachotokea/kinachoendelea. Katika haya mahesabu yao wanashindwa kuelezea kinachotokea kwa sababu kingehitaji kuwepo na chanzo kingine cha gravity na nishati ili mahesabu yajipe. Kwa hiyo hivi vyanzo vya gravity na nishati ambavyo hawavioni ndio wamevipa jina la dark matter na dark energy.

Hii ni sawasawa na wanasayansi wanavyoshindwa kuelezea hapo mwanzoni mwa hii universe yetu kulikuwa na / kulitokea nini. Kila wakifanya mahesabu yao kuhusu mwanzo wa universe wanakutana na jibu = X/Y (yaani ratio) ambayo numerator X sio sifuri lakini siku zote denominator Y ni sifuri. Jibu la namna hii katika mahesabu linaitwa "Singularity" au sekondari tuliliita infinity au haiwezekani. Hii singulaity ndio wanasayansi wanayoiita "BIG BANG". Hawajui kwa uhakika kama ni kweli big bang ilitokea au ilisababishwa na nini (au kulikuwa na nini kabla ya hiyo big bang) lakini hii ndio jeuri ya wanasayansi. Hata kama hawana jibu basi wanachokipata watakipa jina. Hivyo hivyo ndio haya maelezo tunayopata kuhusu dark matter na dark energy.

Sijui kama hii imesaidia.
 
nimekupata mkuu.. vipi kuhusu black holes zipo vipi.. nazo haziwezi kuwa ni sehemu ya dark matter?
 
Black holes nimezielezea kirefu kwenye mambandiko yangu ya awali katika uzi huu huu lakini sio sehemu ya dark matter.

Kuna dhana kuwa black holes za kale (primordial black holes) ndio chanzo cha hii dark matter. Hii dhana inajadiliwa lakini sijui kama inaweza ku-account for gravity field yote inayokosekana katika haya mahesabu.
 
Mkuu Kifyatu mimi nina ombi,
Kama unakuwa na kitu unapenda kutufundisha au ku-share na sisi jambo tafadhari tufundishe....hatuwezi kuwa na maswali pengine ya kutosha kufanya u kashare na sisi vitu vya Ulimwengu na changamoto zake.

Pia unaweza ku-share na sisi kidogo kuhusu astrology katika upande wako..maana ww unaisoma astrology kisasa sio kama zamani. Pengine tufahamu mipangilio ya nyota na kujua zaidi yajayoooo

Kama utapenda hata Kuanzisha Darasa la haya mambo!,me ntakuwa mwanafunzi wako mwaminifu!
Kifyatu
 
Mkuu Kifyatu mimi nina ombi,
Kama unakuwa na kitu unapenda kutufundisha au ku-share na sisi jambo tafadhari tufundishe....hatuwezi kuwa na maswali pengine ya kutosha kufanya u kashare na sisi vitu vya Ulimwengu na changamoto zake
Pia unaweza ku-share na sisi kidogo kuhusu astrology katika upande wako..maana ww unaisoma astrology kisasa sio kama zaman...
Pengine tufaham mipangilio ya nyota na kujua zaidi yajayoooo,

Mkuu neo1 kwanza nitoe shukrani kwako na kwa wadau wengine humu JF kwa kuniamini na kunipa fursa ya ku-share nanyi kile kidogo ninachokijua kuhusu elimu ya nyota na anga.

Nimependa sana hii format ya kujibu maswali ya watu pale nilipoweza (na siku zote nitakuambia kama kitu sikijui kuliko kukudanganya) kwa sababu hii ni aina ya ACTIVE LEARNING. Mtu ana dukuduku lake basi akipata ufafanuzi anajifunza kwa undani zaidi kuliko kama ningemwaga nondo tu za vitu mbalimbali bila kujua nani anataka kuzijua au hataki. Nimejaribu mara nyingi kupanua wigo wa maswali ya watu zaidi ya kile kilichoulizwa ili nielezee kiundani hata kile ambacho hakikuulizwa. Mfano ni swali la awali la mkuu Mwamba028 alilouliza lililoufungua uzi huu.

Lakini nakubaliana na wewe kuwa katika topics nyingi tulizojadili humu inawezekana kuna vitu vya nyongeza vinavyoweza kusaidia watu wapate ufahamu zaidi. Kwa hapa nitajaribu kupitia hizi topics tangu mwanzo ili nione ni vitu gani vinavyohusiana na hizo topics ni vema kuvijua ambavyo hatujavijadili bado. Nitafanya hivi kwa nadra sana ili nisichoshe watu, lakini naahidi kufanya.

Astrology/Unajimu:
Bila ya kujifaragua niseme tu nina ufahamu wa ndani sana kuhusu uhusiano wa mipangilio ya jua/mwezi/nyota/sayari angani na maisha yetu sisi viumbe (binadamu, wanyama, mimea), matukio katika jamii, na matukio hapa duniani. Ingawaje mimi sio muumini wa dini yoyote ile lakini kutokana na ninachokiona katika utafiti wangu wa astrology saa nyingine nawaza kama kweli hakuna "mkono" unaotuongoza katika maisha yetu. Tunaweza kuona kazi ya huo "mkono" kwa kuangalia angani na kuzisoma nyota ipaswavyo. Najua dini nyingi zinapingana na elimu ya unajimu lakini kuna mengi yanayojitokeza ukijifunza Astrology yanayojieleza vinginevyo.

Nimekuwa mwepesi sana kujadili masuala ya Astronomy kwa sababu hii ni sayansi na anayekupinga unaweza kumshushia nondo za kisayansi zisizokua na utata. Astrology (Unajimu), kwa upande mwengine, ni mchanganyiko wa sayansi ya nyota na imani (Science & Spirituality). Hapa sasa ndipo panaponiletea ugumu sana kuijadili astrology humu JF. Kuijadili humu itabidi kwanza nikufanye uamini ninachokijua bila ya mimi kuwa na scientific proof.

Mfano wa kweli: Sayari ya Jupiter ni aina ya "nyota ya jaha," nikimaanisha kuwa inakuletea bahati kubwa sana ikikutembelea kwenye zodiac sign yako. Kwa sasa Jupiter iko kwenye constellation ya Libra (Mizani) na itakaa hapo kwa mwaka mmoja. Wale wote waliozaliwa katika nyota hii ya Libra (September 23 - October 22) basi watakuwa watu wenye bahati kubwa kupata mali, kazi, vyeo, n.k. katika miezi 12 ijayo. Sasa ni lini ufanye nini ku-maximize hii bahati itategemea siku, saa, na mahali ulipozaliwa (itatupa Natal Chart yako).

Tatizo ni kuwa ukiuendekeza sana huu utabiri unaweza kuwa mtumwa wa hizi nyota. Halafu pia sitajua nianzie wapi kuelezea unajimu bila kuonekana kama mganga wa kienyeji (Sangoma).

So, respectfully, I decline to discuss Astrology hapa JF. - Sorry.
 
Aiseeeee Kufyatu umenifungua sana na kunifunza mengi.
Mimi pia napenda sana Elimu hii ya anga pamoja pia na ilmu ya Nyota.
Nitakuwa naendelea kukufuatilia ktk hoja,majibu mblmbl unayoweka humu.
Na niseme Asante sana.
 
Thanx aisee kwa nondo hizi munhu akuzidishie,ila mwisho wa yooote haya tunakuja kuelewa kuwa yupo mwenye nguvu aliye leta mpangilio kama huu ,hivyo niwazi kjwa Mungu yupo na ni muweza wa hayo yoote
 
Asante sana Kifyatu. [emoji1417]

I think Kifyatu ameelezea vyema kuhusiana na dark matter na dark energy but kuna vitu vya kuongezea vingi ambavyo niliwahi kuangalia hizi makala nikajifunza zaidi.

Makala fupi

Makala ndefu ambayo ina elimu nzuri zaidi

Pia kuna makala nyingi sana kuhusiana na ulimwengu mtu anaweza kujifunza hata kama hana background ya sayansi. Zipo illustrated vizuri na wanasayansi wahusika wanajibu vyema kuendana na what science knows.
 
Asante sana mkuu Apollo kwa hii nyongeza. Imefafanua zaidi.

Mkuu kama una links za hizi video mbalimbali za sayansi ya anga ingekuwa vizuri ungetuwekea wadau tujifunze zaidi. Natanguliza shukrani.
 
Mkuu Kifyatu mimi nina ombi,
Kama unakuwa na kitu unapenda kutufundisha au ku-share na sisi jambo tafadhari tufundishe....hatuwezi kuwa na maswali pengine ya kutosha kufanya u kashare na sisi vitu vya Ulimwengu na changamoto zake
Pia unaweza ku-share na sisi kidogo kuhusu astrology katika upande wako..maana ww unaisoma astrology kisasa sio kama zaman...
Pengine tufaham mipangilio ya nyota na kujua zaidi yajayoooo,
Kama utapenda hata Kuanzisha Darasa la haya mambo!,me ntakuwa mwanafunzi wako mwaminifu!
Kifyatu
naungana na wewe..[emoji18] [emoji18]
 
Asante sana mkuu Apollo kwa hii nyongeza. Imefafanua zaidi.

Mkuu kama una links za hizi video mbalimbali za sayansi ya anga ingekuwa vizuri ungetuwekea wadau tujifunze zaidi. Natanguliza shukrani.

Asante kwa Shukran.

Makala nyingi zipo YouTube. Ni nzuri sana. Ukiwa na bandwidth nzuri unaweza kutazama sana.

Kama kuna mada ambayo mtu atataka makala yake nitampatia. Nyingi nilidownload na huwa naangalia makala kila siku, nikiwa na free time.

Asante.
 
Mkuu me naomba link ya cosmos:a spacetime odyssey ya Neil de Tyson yenye quality ya 720 au 1080!
Nimetafuta YouTube sikupata .
 
Mkuu kifyatu shukrani kwa kunitoa tongotongo machoni lakini inasemekana kuna wanasayans ambao waliwai kufika mwezini miaka ya nyuma ingawa jambo hili limekua likipingwa na wanasayansi wengine sijui hili kwa upande wako upo upande gani?
 
Mkuu hakuna utata kuwa wanaanga (astronauts) wa kimarekani walitua kwenye uso wa mwezi mara kadhaa. Nakumbuka wakati haya matukio yakitokea (nilikuwa tayari nadunda hapa duniani) kulikuwa na mijadala mikubwa sana vijiweni kuhusu ukweli wake. Kuna wale waliokuwa wanasema kuwa kuna mbingu saba na mwezi uko mbingu ya tatu na kuwa ni uongo kuwa Apollo -11 (chombo kilichotua mwezini na watu, sio mkuu Apollo ) ilitua mwezini. Ilivukaje hizo mbingu zote tatu mpaka kufika mwezini - waliuliza. Ukweli umebakia palepale kuwa walitua. Na sasa wanapanga safari ndefu zaidi kupeleka watu sayari ya Mars.

Kwa hiyo ukiniuliza upande wangu ninaonaje, wala sifikirii mara mbili, watu wamekwisha tua kwenye uso wa mwezi.

Utani:
Comedian wa kiingereza hapo nyuma walikuwa wanawadhihaki watani wao wa jadi, wa-irish, kuwa na wao wanaunda chombo cha kuwapeleka watu kwenye jua - ikifika usiku.
 
Back
Top Bottom