Mkuu
neo1 kwanza nitoe shukrani kwako na kwa wadau wengine humu
JF kwa kuniamini na kunipa fursa ya ku-share nanyi kile kidogo ninachokijua kuhusu elimu ya nyota na anga.
Nimependa sana hii format ya kujibu maswali ya watu pale nilipoweza
(na siku zote nitakuambia kama kitu sikijui kuliko kukudanganya) kwa sababu hii ni aina ya ACTIVE LEARNING. Mtu ana dukuduku lake basi akipata ufafanuzi anajifunza kwa undani zaidi kuliko kama ningemwaga nondo tu za vitu mbalimbali bila kujua nani anataka kuzijua au hataki. Nimejaribu mara nyingi kupanua wigo wa maswali ya watu zaidi ya kile kilichoulizwa ili nielezee kiundani hata kile ambacho hakikuulizwa. Mfano ni swali la awali la mkuu
Mwamba028 alilouliza lililoufungua uzi huu.
Lakini nakubaliana na wewe kuwa katika topics nyingi tulizojadili humu inawezekana kuna vitu vya nyongeza vinavyoweza kusaidia watu wapate ufahamu zaidi. Kwa hapa nitajaribu kupitia hizi topics tangu mwanzo ili nione ni vitu gani vinavyohusiana na hizo topics ni vema kuvijua ambavyo hatujavijadili bado. Nitafanya hivi kwa nadra sana ili nisichoshe watu, lakini naahidi kufanya.
Astrology/Unajimu:
Bila ya kujifaragua niseme tu nina ufahamu wa ndani sana kuhusu uhusiano wa mipangilio ya jua/mwezi/nyota/sayari angani na maisha yetu sisi viumbe (binadamu, wanyama, mimea), matukio katika jamii, na matukio hapa duniani. Ingawaje mimi sio muumini wa dini yoyote ile lakini kutokana na ninachokiona katika utafiti wangu wa astrology saa nyingine nawaza kama kweli hakuna
"mkono" unaotuongoza katika maisha yetu. Tunaweza kuona kazi ya huo
"mkono" kwa kuangalia angani na kuzisoma nyota ipaswavyo. Najua dini nyingi zinapingana na elimu ya unajimu lakini kuna mengi yanayojitokeza ukijifunza Astrology yanayojieleza vinginevyo.
Nimekuwa mwepesi sana kujadili masuala ya Astronomy kwa sababu hii ni sayansi na anayekupinga unaweza kumshushia nondo za kisayansi zisizokua na utata. Astrology (Unajimu), kwa upande mwengine, ni mchanganyiko wa sayansi ya nyota na imani
(Science & Spirituality). Hapa sasa ndipo panaponiletea ugumu sana kuijadili astrology humu JF. Kuijadili humu itabidi kwanza nikufanye uamini ninachokijua bila ya mimi kuwa na scientific proof.
Mfano wa kweli: Sayari ya
Jupiter ni aina ya
"nyota ya jaha," nikimaanisha kuwa inakuletea bahati kubwa sana ikikutembelea kwenye
zodiac sign yako. Kwa sasa Jupiter iko kwenye constellation ya Libra (Mizani) na itakaa hapo kwa mwaka mmoja. Wale wote waliozaliwa katika nyota hii ya Libra (September 23 - October 22) basi watakuwa watu wenye bahati kubwa kupata mali, kazi, vyeo, n.k. katika miezi 12 ijayo. Sasa ni lini ufanye nini ku-maximize hii bahati itategemea siku, saa, na mahali ulipozaliwa (itatupa Natal Chart yako).
Tatizo ni kuwa ukiuendekeza sana huu utabiri unaweza kuwa mtumwa wa hizi nyota. Halafu pia sitajua nianzie wapi kuelezea unajimu bila kuonekana kama mganga wa kienyeji (Sangoma).
So, respectfully, I decline to discuss Astrology hapa JF. - Sorry.