Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Hii ni picha inayoonesha uwiano wa ukubwa wa sayari na baadhi ya nyota
Stars.jpg
 
Attachments

  • Star-sizes.jpg
    Star-sizes.jpg
    32.3 KB · Views: 293
Nimekuwa natafuta sana kuelewa hizo Blac holes lakini imekuwa ngumu kwangu kuelewa uje na lugha rahisi kwa sisi tusiojua physics kuelewa maana niliwahi kusoma sehemu kuwa black holes yaweza kumeza hata dunia sijui kama ni kweli.
Black holes hutokea pale nyota inapofikia mwisho wa maisha yake na kufa, hiyo nyota hugandamizwa na kupungua size kwa kuwa na umbo dogo hivyo kuwa na nguvu ya uvutano (gravity) kubwa zaidi.

Baada ya black hole kutengenezwa huanza kuvuta na kumeza vitu vilivyo karibu yake mfano huweza kuungana na black holes nyingine, humeza nyota nyingine hivyo kuzidi kukua na kupngezeka ukubwa.

Kutokana na ukubwa wa uwezo wake wa nguvu ya kuvuta vitu, hakuna kitu chochote kinachoweza kupenya ukiwemo mwanga. Mwanga unapoingia kwenye black hole hauwezi kupenya au kuwa reflected kutokana na nguvu ya uvutano iliyopo ndani hivyo basi kila kiingiacho hakiwezi kutoka.
 
Mkuu jua ndio nyota kubwa kuliko zote. So a sun is a star too
Msaada zaidi: just google ''Sun"

Yeah is the biggest star, and it produce its own light and heat.. sema sasa jua halisogea (halifanyi movement) lakini nyota zingine zinatembea angani pamoja na vimondo(comets)
 
Nimekuwa natafuta sana kuelewa hizo Blac holes lakini imekuwa ngumu kwangu kuelewa uje na lugha rahisi kwa sisi tusiojua physics kuelewa maana niliwahi kusoma sehemu kuwa black holes yaweza kumeza hata dunia sijui kama ni kweli.

Kama nilivyo ahidi ifuatayo ni ile nyongeza.

Nyota zinazaliwaje?
Kabla ya nyota kuzaliwa inaanza kama sayari ya kawaida wakati vumbi na hewa (sana sana hydrogen) ikijikusanya. Kadri hii hewa na vumbi vinavyoongezeka basi gravity nayo pia inaongezeka. Tukichukulia ukubwa/uzito wa jua letu kama kiwango (solar-mass) basi mkusanyiko wowote ule wa vumbi na hewa chini ya 0.013 solar-mass (1.3% ukubwa wa jua letu) hiyo itakuwa ni sayari (planet) tu. Kuanzia ukubwa wa 0.08 solar-mass na kuendelea gravity inakuwa kubwa sana (kilo moja hapa duniani ukiipeleka huko itakuwa na uzito wa kilo bilioni 100 na zaidi). Huu mgandamizo mkubwa wa gravity unafanya joto kupanda zaidi ya nyuzi milioni 15 celcius. Hili joto na mgandamizo wa gravity ndio kibiriti kinachofanya hydrogen ichanganyike ketengeneza helium na kutoa nguvu hizi za nyuklia (fusion). Hivi ndio jua linavyozaliwa.

Nyota zinakufaje?
Maisha ya nyota yanategemea sana na ukubwa wake. Nyota ndogo zinaishi muda mrefu sana (zinachoma hydrogen yake taratibu taratibu) kuliko nyota kubwa. Kwa mfano, nyota ndogo kama jua letu inategemewa kuwaka kwa miaka bilioni 10 wakati nyota kubwa sana kama Betelgeuse zinategemewa kuwaka kwa miaka million 10 tu.

Wakati nyota inawaka kunakuwa na uwiano (equilibrium) wa nguvu ya gravity na nyuklia. Gravity inakandamiza chini wakati milipuko ya nyuklia inasukuma vitu nje. Uwiano huu unaendelea hata baada ya hydrogen ikiisha. Baada ya hydrogen kuisha helium nayo italipuka kinyuklia kutengeneza Carbon na Oxygen. Baadae carbon nayo italipuka kunyuklia kutengeneza iron (chuma). Mara tu nyota inapoanza kutengeneza chuma (iron), mchezo umekwisha. Chuma ni kama maji yanayouzima huu mlipuko wa nyuklia mara moja. Milipuko ya nyuklia ikiacha, ule uwiano (equilibrium) wa gravity na nyukilia unakuwa haupo tena na gravity inashinda. Kila kitu huanguka chini na mlipuko mkubwa sana wa mwisho hutokea na mwanga mkubwa sana (super nova) huonekana.

Vitu viwili vinatokea wakati wa hii super nova. Kwanza, madini nzito zaidi ya chuma (iron) yanatengenezwa kama vile dhahabu, urani, nk. Hii ndio maana dunia yetu pamoja na sisi tunaitwa vumbi la nyota (star dust) kwa saababu kama hizi super nova zisingetokea basi dunia yetu na sisi tusingekuwepo. La pili linaliotokea baada ya kishindo (collapse) ni kuwacha tumba (core) ndogo sana lakini yenye uzito (density) mkubwa wa ajabu. Hii tumba ndio ijulikanayo kama BLACK HOLE.

(For correctness sake, not all stars die and turn into black holes. For instance, our sun is too small to turn into a black hole. When it dies it will collapse into a dense core with properties nowhere close to those of black holes)

Black holes na makaburi ya nyota.
Black holes zinazotokea baada ya nyota kubwa sana (super massive stars) ku-collapse ni vitu vya ajabu sana. Chupa moja ya bia (ujazo wa 0.5 lita) ya hii black-hole ina uzito wa zaidi ya tani 3,000,000,000,000. Gravity inayotokana na hizi black holes ni kubwa kiasi ya kumeza kitu chochote kile (majua, sayari, nk) kinachoikaribia. Hii gravity ni kubwa kiasi cha kumeza hata mwanga (even light cannot escape it) na ndio maana zinaitwa BLACKHOLE kwa sababu hazionekani (mwanga pia unamezwa). Kuwepo wa black hole kunajulikana tu kwa vitu inavyovimeza au vinavyo izunguuka. Usiku ukitoka nje angalia juu. Ukiona ukanda wa nyota nyingi basi huo ndio mkusanyiko wetu wa nyota (Galaxy yetu) unaoitwa MILKYWAY. Katikati ya hi
i galaxy yetu lipo hili black hole moja ambalo jua letu na nyota nyingine zote zilizopo kwenye hii galaxy yetu zinalizunguuka. Ukitaka kujua hii blackhole yetu iko wapi angalia juu na kama unaijua constellation ya Virgo basi usawa huo ndipo lilipo.

Natumaini hii itasaidia pa kuanzia katika kuzijua nyota.

cc. Mwamba028, 2013 Globu
Iron Lady
 
Black holes hutokea pale nyota inapofikia mwisho wa maisha yake na kufa, hiyo nyota hugandamizwa na kupungua size kwa kuwa na umbo dogo hivyo kuwa na nguvu ya uvutano (gravity) kubwa zaidi.
Baada ya black hole kutengenezwa huanza kuvuta na kumeza vitu vilivyo karibu yake mfano huweza kuungana na black holes nyingine, humeza nyota nyingine hivyo kuzidi kukua na kupngezeka ukubwa.
Kutokana na ukubwa wa uwezo wake wa nguvu ya kuvuta vitu, hakuna kitu chochote kinachoweza kupenya ukiwemo mwanga. Mwanga unapoingia kwenye black hole hauwezi kupenya au kuwa reflected kutokana na nguvu ya uvutano iliyopo ndani hivyo basi kila kiingiacho hakiwezi kutoka.

najaribu kufikiria tu(sio kisayansi) baada ya hizo nyota kumezwa huwa zinayeyushwa au zinaishiaga wapi? na je hilo black hole halina mwisho(nazungumzia kina chake) au mwisho wake ni upi?
 
Kama nilivyo ahidi ifuatayo ni ile nyongeza.

Nyota zinazaliwaje?
Kabla ya nyota kuzaliwa inaanza kama sayari ya kawaida wakati vumbi na hewa (sana sana hydrogen) ikijikusanya. Kadri hii hewa na vumbi vinavyoongezeka basi gravity nayo pia inaongezeka. Tukichukulia ukubwa/uzito wa jua letu kama kiwango (solar-mass) basi mkusanyiko wowote ule wa vumbi na hewa chini ya 0.013 solar-mass (1.3% ukubwa wa jua letu) hiyo itakuwa ni sayari (planet) tu. Kuanzia ukubwa wa 0.08 solar-mass na kuendelea gravity inakuwa kubwa sana (kilo moja hapa duniani ukiipeleka huko itakuwa na uzito wa kilo bilioni 100 na zaidi). Huu mgandamizo mkubwa wa gravity unafanya joto kupanda zaidi ya nyuzi milioni 15 celcius. Hili joto na mgandamizo wa gravity ndio kibiriti kinachofanya hydrogen ichanganyike ketengeneza helium na kutoa nguvu hizi za nyuklia (fusion). Hivi ndio jua linavyozaliwa.

Nyota zinakufaje?
Maisha ya nyota yanategemea sana na ukubwa wake. Nyota ndogo zinaishi muda mrefu sana (zinachoma hydrogen yake taratibu taratibu) kuliko nyota kubwa. Kwa mfano, nyota ndogo kama jua letu inategemewa kuwaka kwa miaka bilioni 10 wakati nyota kubwa sana kama Betelgeuse zinategemewa kuwaka kwa miaka million 10 tu.

Wakati nyota inawaka kunakuwa na uwiano (equilibrium) wa nguvu ya gravity na nyuklia. Gravity inakandamiza chini wakati milipuko ya nyuklia inasukuma vitu nje. Uwiano huu unaendelea hata baada ya hydrogen ikiisha. Baada ya hydrogen kuisha helium nayo italipuka kinyuklia kutengeneza Carbon na Oxygen. Baadae carbon nayo italipuka kunyuklia kutengeneza iron (chuma). Mara tu nyota inapoanza kutengeneza chuma (iron), mchezo umekwisha. Chuma ni kama maji yanayouzima huu mlipuko wa nyuklia mara moja. Milipuko ya nyuklia ikiacha, ule uwiano (equilibrium) wa gravity na nyukilia unakuwa haupo tena na gravity inashinda. Kila kitu huanguka chini na mlipuko mkubwa sana wa mwisho hutokea na mwanga mkubwa sana (super nova) huonekana.

Vitu viwili vinatokea wakati wa hii super nova. Kwanza, madini nzito zaidi ya chuma (iron) yanatengenezwa kama vile dhahabu, urani, nk. Hii ndio maana dunia yetu pamoja na sisi tunaitwa vumbi la nyota (star dust) kwa saababu kama hizi super nova zisingetokea basi dunia yetu na sisi tusingekuwepo. La pili linaliotokea baada ya kishindo (collapse) ni kuwacha tumba (core) ndogo sana lakini yenye uzito (density) mkubwa wa ajabu. Hii tumba ndio ijulikanayo kama BLACK HOLE.

(For correctness sake, not all stars die and turn into black holes. For instance, our sun is too small to turn into a black hole. When it dies it will collapse into a dense core with properties nowhere close to those of black holes)

Black holes na makaburi ya nyota.
Black holes zinazotokea baada ya nyota kubwa sana (super massive stars) ku-collapse ni vitu vya ajabu sana. Chupa moja ya bia (ujazo wa 0.5 lita) ya hii black-hole ina uzito wa zaidi ya tani 3,000,000,000,000. Gravity inayotokana na hizi black holes ni kubwa kiasi ya kumeza kitu chochote kile (majua, sayari, nk) kinachoikaribia. Hii gravity ni kubwa kiasi cha kumeza hata mwanga (even light cannot escape it) na ndio maana zinaitwa BLACKHOLE kwa sababu hazionekani (mwanga pia unamezwa). Kuwepo wa black hole kunajulikana tu kwa vitu inavyovimeza au vinavyo izunguuka. Usiku ukitoka nje angalia juu. Ukiona ukanda wa nyota nyingi basi huo ndio mkusanyiko wetu wa nyota (Galaxy yetu) unaoitwa MILKYWAY. Katikati ya hi
i galaxy yetu lipo hili black hole moja ambalo jua letu na nyota nyingine zote zilizopo kwenye hii galaxy yetu zinalizunguuka. Ukitaka kujua hii blackhole yetu iko wapi angalia juu na kama unaijua constellation ya Virgo basi usawa huo ndipo lilipo.

Natumaini hii itasaidia pa kuanzia katika kuzijua nyota.

cc. Mwamba028, 2013 Globu
Iron Lady

Asante kwa darasa hili
 
Mkuu Kifyatu I salute you
 
Last edited by a moderator:
najaribu kufikiria tu(sio kisayansi) baada ya hizo nyota kumezwa huwa zinayeyushwa au zinaishiaga wapi? na je hilo black hole halina mwisho(nazungumzia kina chake) au mwisho wake ni upi?

watu wengi wanadhani black hole ni shimo, kiuhalisia sio shimo bali ni sehemu katika space ambayo inamvutano mkubwa sana na kila kinachojaribu penya huvutwa na kuvunjwa vunjwa na kuwa part of the black hole.

kumbuka nyota zimetengenezwa na gases mkuu kwahiyo sio solid na nyota inapovuta na black hole uwa compressed na kuwa ndogo zaidi hii huifanya hiyo nyota kuwa na more gravity na hivyo hiyo gravity huongeza nguvu za hiyo black hole.

Black hole sio shimo kama wengi wanavyodhani bali imeitwa hivyo kwakuwa ni black kutokana na ukweli kuwa hata mwanga hauwezi penya.
 
Nini constelletion ya Virgo. Ufafanuzi kidogo. Vile vile hivyo vitu vinavyomezwa na Black hole huwa vinaishia wapi? Mkuu Kifyatu.

Constellation ya Virgo (au Mashuke) ni mkusanyiko wa nyota unaofananishwa na mwanamwali (Virgin). Kama uko Tanzania kwa sasa Virgo inajitokeza mashariki kuanzia saa moja usiku. Ikifika saa 6 na nusu usiku itakuwa utosini kwako. Kama uko sehemu nyingine duniani nitonye nitakueleza uangalie wapi.

Kwa hiyo kama unataka kujua blackhole yetu iko muelekeo gani, jua linapozama tu angalia mashariki ndipo ilipo au angalia straight up kwenye saa sita na nusu usiku. Wakati ukiiangalia hii constellation ya Virgo basi milkway galaxy yetu iko magharibi ya Virgo. Milkway galaxy huwezi kukosa kuiona (hasa usiku wa manane). Utaona nyota nyingi kama mtu amemwaga maziwa (hence milkway) huko angani.

Vitu vinavyomezwa na blackhole vinakuwa sehemu ya hiyo blackhole na inazidi kukua.
 
Kama nilivyo ahidi ifuatayo ni ile nyongeza.

Nyota zinazaliwaje?
Kabla ya nyota kuzaliwa inaanza kama sayari ya kawaida wakati vumbi na hewa (sana sana hydrogen) ikijikusanya. Kadri hii hewa na vumbi vinavyoongezeka basi gravity nayo pia inaongezeka. Tukichukulia ukubwa/uzito wa jua letu kama kiwango (solar-mass) basi mkusanyiko wowote ule wa vumbi na hewa chini ya 0.013 solar-mass (1.3% ukubwa wa jua letu) hiyo itakuwa ni sayari (planet) tu. Kuanzia ukubwa wa 0.08 solar-mass na kuendelea gravity inakuwa kubwa sana (kilo moja hapa duniani ukiipeleka huko itakuwa na uzito wa kilo bilioni 100 na zaidi). Huu mgandamizo mkubwa wa gravity unafanya joto kupanda zaidi ya nyuzi milioni 15 celcius. Hili joto na mgandamizo wa gravity ndio kibiriti kinachofanya hydrogen ichanganyike ketengeneza helium na kutoa nguvu hizi za nyuklia (fusion). Hivi ndio jua linavyozaliwa.

Nyota zinakufaje?
Maisha ya nyota yanategemea sana na ukubwa wake. Nyota ndogo zinaishi muda mrefu sana (zinachoma hydrogen yake taratibu taratibu) kuliko nyota kubwa. Kwa mfano, nyota ndogo kama jua letu inategemewa kuwaka kwa miaka bilioni 10 wakati nyota kubwa sana kama Betelgeuse zinategemewa kuwaka kwa miaka million 10 tu.

Wakati nyota inawaka kunakuwa na uwiano (equilibrium) wa nguvu ya gravity na nyuklia. Gravity inakandamiza chini wakati milipuko ya nyuklia inasukuma vitu nje. Uwiano huu unaendelea hata baada ya hydrogen ikiisha. Baada ya hydrogen kuisha helium nayo italipuka kinyuklia kutengeneza Carbon na Oxygen. Baadae carbon nayo italipuka kunyuklia kutengeneza iron (chuma). Mara tu nyota inapoanza kutengeneza chuma (iron), mchezo umekwisha. Chuma ni kama maji yanayouzima huu mlipuko wa nyuklia mara moja. Milipuko ya nyuklia ikiacha, ule uwiano (equilibrium) wa gravity na nyukilia unakuwa haupo tena na gravity inashinda. Kila kitu huanguka chini na mlipuko mkubwa sana wa mwisho hutokea na mwanga mkubwa sana (super nova) huonekana.

Vitu viwili vinatokea wakati wa hii super nova. Kwanza, madini nzito zaidi ya chuma (iron) yanatengenezwa kama vile dhahabu, urani, nk. Hii ndio maana dunia yetu pamoja na sisi tunaitwa vumbi la nyota (star dust) kwa saababu kama hizi super nova zisingetokea basi dunia yetu na sisi tusingekuwepo. La pili linaliotokea baada ya kishindo (collapse) ni kuwacha tumba (core) ndogo sana lakini yenye uzito (density) mkubwa wa ajabu. Hii tumba ndio ijulikanayo kama BLACK HOLE.

(For correctness sake, not all stars die and turn into black holes. For instance, our sun is too small to turn into a black hole. When it dies it will collapse into a dense core with properties nowhere close to those of black holes)

Black holes na makaburi ya nyota.
Black holes zinazotokea baada ya nyota kubwa sana (super massive stars) ku-collapse ni vitu vya ajabu sana. Chupa moja ya bia (ujazo wa 0.5 lita) ya hii black-hole ina uzito wa zaidi ya tani 3,000,000,000,000. Gravity inayotokana na hizi black holes ni kubwa kiasi ya kumeza kitu chochote kile (majua, sayari, nk) kinachoikaribia. Hii gravity ni kubwa kiasi cha kumeza hata mwanga (even light cannot escape it) na ndio maana zinaitwa BLACKHOLE kwa sababu hazionekani (mwanga pia unamezwa). Kuwepo wa black hole kunajulikana tu kwa vitu inavyovimeza au vinavyo izunguuka. Usiku ukitoka nje angalia juu. Ukiona ukanda wa nyota nyingi basi huo ndio mkusanyiko wetu wa nyota (Galaxy yetu) unaoitwa MILKYWAY. Katikati ya hi
i galaxy yetu lipo hili black hole moja ambalo jua letu na nyota nyingine zote zilizopo kwenye hii galaxy yetu zinalizunguuka. Ukitaka kujua hii blackhole yetu iko wapi angalia juu na kama unaijua constellation ya Virgo basi usawa huo ndipo lilipo.

Natumaini hii itasaidia pa kuanzia katika kuzijua nyota.

cc. Mwamba028, 2013 Globu
Iron Lady

Mkuu Kifyatu embu naomba ufafanuzi zaidi kwenye hiyo super nova na nn uhusiano wake na uwepo wa dunia, yan kwann umesema km supanova isingetokea basi dunia na sisi tusingekuwepo?
Then hizi nondo zako zina mahusiano yoyote na bing bang theory?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kifyatu embu naomba ufafanuzi zaidi kwenye hiyo super nova na nn uhusiano wake na uwepo wa dunia, yan kwann umesema km supanova isingetokea basi dunia na sisi tusingekuwepo?
Then hizi nondo zako zina mahusiano yoyote na bing bang theory?

Super-nova haina uhusiano na Big Bang Theory.

Sasa tuanze na Big Bang Theory.
Hii ni dhana inayosema kuwa mwanzo kabisa hakukuwa na kitu chochote isipokuwa nishati iliyokuwa sehemu moja ndogo sana (singularity). Ile nishati ililipuka (big bang - hakuna anaejua kwa nini ililipuka) na kwa kupitia nyenzo ziitwazo Higg's Boson hii nishati ilibadilika na kuwa element nyepesi sana ambayo ni hewa ya hydrogen. Hii hydrogen ilijikusanya kwa wingi na gravity ilipokuwa kubwa hydrogen ili-fuse kutengeneza helium katika mlipuko wa nyuklia (fusion) kama nilivyoainisha hapo awali.

Tatizo ni kuwa hii nyuklia fusion inaweza kutengeneza helium, carbon, oxygen na elements nyingine ambazo ni nyepesi kuliko iron (chuma). Chuma kikianza kutengenezwa tu basi hiyo nyuklia reaction inasimama. Kwa hiyo madini kama zinc, tin, gold, nk. ambazo ni muhimu mwilini mwetu na pia kwa matumizi mengine hizi hutengengenezeka tu wakati wa mlipuko wa supernova.

Baada ya supanova kutokea, tumba (core) inakuwa blackhole na vumbi vumbi lililosambaa linajikusanya makundi makundi na kutengeneza sayari kama dunia yetu.

Summary
Big bang ilibadilisha nishati (pure energy) kuwa hydrogen, hydrogen ilianzisha nyota. Nyota zikatengeneza element chache (mpaka kufikia chuma). Nyota ikifa na kutokea supernova basi elements nyingine nzito kuliko chuma zinatengezwa. Kwa hiyo maisha yetu kama tuyajuavyo sasa yametegemea sana super-nova explosions.

I hope imesaidia.
 
mkuu kifyatu mimi naomba kukurudisha nyuma
1. super nova ni nini na zinalipuka mara ngapi ili sisi tupate hizo faida zake
2. tunaonaje ama kujuaje kwamba supernova imetokea
3. blackhole na usalama wa dunia vimekaaje
4. UFO's ni nini?
samahani kama maswali yamekuwa mengi lakini hii mada imekuwa interesting kwangu kuliko bunge lla katiba!!
 
nyota ni ndogo sana kuliko dunia, ni kama mwezi. zinategemea mwanga wa jua. na nyota ulizoona zinazobadilika kutoka rangi kutokea ya blue kwenda ya kijani ni kutokana na kuzibwa na miti na bahari .na ukiona nyekundu ujue hapo kuna radi na mvua inanyesha.

Hahahahahahaaaaaa nimecheka hadi machozi yamenitoka dah. Kweli hii kali ya mwaka hahahaha
 
ha ha ha ha, mkuu with no offence wala nini , ni kwamba mleta uzi aliposema anaona nyota za rangi ya kijani, blue na red, niliona hayuko siriaz, ndio maana nikawaza nimjibu pasipo u-siriaz wowote.

Kwani binafsi sijawahi kuona nyota yenye rangi zaidi ya nyeupe ikiwa katika ile hali ya kubadilikabadilika kama mshumaa unaopigwa na upepo.(blinking)nimesoma ARTICLE KUHUSU RANGI ZA NYOTA, sehemu nyingine wanasema nyota zinaweza kuonekana za rangi ya blue, red -- hivyo nikaona nikubaliane naye kwamba alikuwa anamaanisha KWELI ANAONA UTOFAUTI HUO WA RANGI.
 
Kwa ufaham wangu mdogo UFO'S ni viumbe(Ailiens) ambavyo kwenye dunia yetu ya tatu havijawah kuonekana kutokana na tecnologia yao ambayo ni highly advanced na inaizd dunia ×100,
Kwa mara ya kwanza hivo viumbe vilionekana Marekani lakin mmarekan akadivert info kuwa hakuna kitu kama icho ili kuisoma zaid tecnology yao ili iwe yenye nguvu zaid kitecnolojia.
 
Hii mada imenifanya ni load mambo mengi ambayo mwanzo nilikuwa nayajua lakin nilikuwa siyaelewi likin leo nimeyaelewa zaid...!!
ila pia kuna mambo ambayo nilikuwa nataka kuelewa zaidi.

Hivii hii "THE BIG BANG THEORY" ni kweli ndio chimbuko la mwadaam yan Element au chembechembe ambazo binaadam ameumbwa nazo ni zao la hio Theory ¡¡¡
Na pia je kuhusiana na elimu ya nyota inavohusika kwenye utabiri, kutoa ishara ,Bahati na mengineyo Mfano mm kuna nyota tatu zimekaa mstari na nyingine kama umbo Pyramid ambazo ni tofauti na nyingine thou zina change position kutokana na rotation ya dunia, but kitu ambacho najiuliza how can i interprate that sign ni hayo 2 nilikuwa naomba kueleweshwa na sio kuyafaham.
 
Back
Top Bottom