Kifyatu na wadau wengine habari zenu?
kwanza samahan sana kwa kuchelewa kuleta mrejesho hapa kuhusu Faida za rad hapa dunian na pili samahan kwa kusababisha baadh ya maswal na hoja kushindwa kukibiwa hapa kwa sababu ya kusubili majibu yangu kuhusu faida za radi,!
Naomba nikili kuwa nimeshindwa kupata hayo majawabu ya faida za rad labda kwa sababu ya uwezo wangu mdogo wa kucheza na mambo ya internet kwa sababu kila niki google kwa lugha ya kiswahil naona majibu yanakuja hayarizish na mengi yanakuja kwa njia za kidin na mimi sio mzur sana kwenye lugha za kisayans na hasa kwa kingereza.,
Ivyo bas nikawa najihis mwenye hatia endapo ningeamua kuwaletea majibu yasio na ujazo uliojitosheleza kwa watu wenye uelewa mkubwa humu kuliko mm kuhusu maswala ya kisayans na ivyoo ningekuwa sijawatendea haki sababu ningeshindwa kujibu maswali ambayo mngeniuliza,!'
naomba niwasilishe faida za rad japo sitokuwa na maelezo yaliojitosheleza so ntaomba mkuu Kifyatu atolee maelezo kama niko sahihi au laa,'
1) Mbolea
2)uwepo wa rad usababisha mvua kubwa sababu ya ule mkandamizo wa umeme
3)cabon
Uislamu na suala la radi + Sauti
Asante
baraka bb kwa mrejesho. Hujakosea kuhusu mbolea (na nitaelezea) lakini nitakupa alama ya
B+ kwa sababu hukuelezea:
- radi inatoaje mbolea na
- kwa nini radi pekee ndio ilioleta uhai wetu viumbe wote hapa duniani.
Mvua kubwa haisababishwi na radi bali radi husababishwa na mawingu mazito ambayo yanaleta mvua kubwa.
Sasa nielezee hizo point mbili za juu:
Radi inatoaje mbolea?
78% ya hewa yetu tunayopumua ni
Nitrogen. Hii hewa tunaivuta lakini hatuitumii (nikimaanisha tunaitoa kama tunavyoivuta). Tunatumia Oxygen tu kwa uhai wetu. Unaweza ukafikiria kuwa sasa faida ya hii Nitrogen ni nini?
Mimi na mkuu
neo1 tulizungumzia kitu kinachoitwa
plasma hapo awali. Wakati wa radi ule umeme na moto mkali wake unatengeneza plasma ya hewa yoyote ile inayoipitia. Lakini hasa hii plasma ya Nitrogen ni muhimu kwa sababu katika hali hiyo, nitrogen plasma ikianguka aridhini na mvua inakuwa rahisi kuchanganyika (react) na madini nyingine aridhini na kutengeneza
NITRATES. Ni hizi nitrates ambazo ndio
mbolea inayoweza kutumika na mmea kutengeneza chakula chake na kukua. Hewa ya Nitrogen kama ilivyo angani haiwezi kuchanganyika na madini aridhini kutengeneza Nitrates, inahitaji radi kutengeneza plasma ya Nitrogen kwanza.
Kwa nini radi pekee ndio ilioleta uhai wetu viumbe wote hapa duniani?
Ili mmea utengeneze
proteins unahitaji Nitrogen ambayo inaipata kama nitrates kutoka aridhini. Bila ya hizi nitrates basi mmea usingeweza kutengeneza proteins, na ungekufa. Wanyama wakila hii mimea wanachukua hizo proteins za mmea na kutengeneza protein zao. Bila ya hizi proteins za mimea, wanyama (viumbe hai pamoja na sisi binadamu) wa(tu)singekuwepo hapa duniani. Kwa hiyo mkuu
baraka bb, kila unapotunisha misuli yako basi uishukuru RADI kwa kuwezesha huwa na hizo proteins zilizojenga mwili wako.
Mars
Mkuu
neo1 uliuliza swali kuhusu sayari ya Mars na ni nini cha kufanya ili watu na mimea iwepo (or something like that). Nilikujibu kuwa tunahitaji kupanda miti kwa sababu 96% ya hewa yake ni
Carbon Dioxide inayohitajika na miti halafu miti itapumua
Oxygen tunayoihitaji sisi watu na wanyama. Lakini nilitoa ilani kuwa hewa ya Mars ina 2-3% Nitrogen. Nikasema hii inaweza kuleta utata kidogo. Nilimaanisha kuwa kama hii asilimia ndogo ya nitrogen itaathiri upatikanaji wa NITRATES za kutosha kupitia radi, nitrogen plasma na mvua. Sijui jibu sahihi la hofu yangu hii.