Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Sante mkuu Kifyatu kwenye kuzunguka nimekutana na mada zaman kulikuwa na kimondo kikubwa kinakuja kugonga dunia...pengine ndo ingekuwa mwisho wa maisha!!,Kwa Bahati nzur our brother Jupiter Kwa sababu ya Gravity pull yake kubwa kwnye solar system he pulled it away!!!,wazungu tokana na iyo incident wakaitengenezea movie Armageddon ya bluce wills..je since then as dunia tumejipanga au tumejianda kujihami if incident like that if happens again au our brother is out there[emoji6]??
 
Jupiter inatusaidia sana kuepusha asteroids kutugonga. Lakini Jupiter pia saa nyingine inasaidia kutuletea meteors (mfano kutoka Mars) hapa kwetu.

Kuna program nyingi tu zinazo-track na kutupa taarifa ya hizi Asteroids zinazoweza kutugonga. Pia kuna mikakati mingi tu ya kuepushana na majabari yanayotuelekea sisi kutuangamiza. Anza na hii link hapa chini utapata mengi zaidi ya ninachoweza kuelezea.

Asteroid impact avoidance - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Asante mkuu kwa kushukuru.

Galaxy yetu (milkway nilioiweka hapo chini) ni spiral galaxy (ina mikia). Katikati ya hii galaxy ndipo lilipo hilo blackhole letu. Sisi (jua na solar system yetu) tuko kwenye moja ya mikia ya hii galaxy mbali kabisa na center. Kwa hiyo kama jua halituzibii tunaweza kuiona karibuni galaxy yetu yote usiku.
images

Mkuu samahani kwa usumbufu naomba kupata ufafanuzi

Umesema hapo katikati ndipo lilipo blackhole mbona sasa panaonekana ndipo panapong'aa kuliko sehemu yeyote ya hiyo picha.

Tukukumbuke mkuu blackhole haipigiki picha..yaani ni totally invisible.

Sasa nilipoiona hii picha na ulichosema nikastuka kidogo mkuu.
 
Ilipo blackhole yenyewe hapaonekani (mwanga unamezwa na hii blackhole). Lakini karibu na hiyo blackhole kunakuwa na mkusanyiko mkubwa (concentration) ya nyota zinazoizunguuka hii blackhole. Mradi zipo kwenye orbits zao basi haziwezi kumezwa. Zikisesereka tu kuangukia kwenye blackhole basi zinamezwa pamoja na mwanga wake.
 
Mkuu Kifyatu naomba nikusumbue tena kwa suali jengine.
Je imekuaje ikatokea sisi wanadamu ndio tukawa hapa kwenye sayari ya dunia ambako imekuwa kwetu rahisi kimazingira kuishi?.
Kwa nini tusingejikuta kwenye Jupiter huko au Uranus au hata kwenye sayari yeyote katika hii solar system yetu?.
 
Hiki ndicho wanachofanya wanasayansi ya anga kuona kama kuna sayari nyingine kwenye solar system yetu inayo-support life. Mpaka sasa bado hawajaona dalili za uhai.

Lakini pia utafiti unaendelea kuona kama kuna solar systems nyingine zaidi ya hii yetu ambazo zina sayari zenye vigezo kama vya dunia yetu na pengine kukawa na maisha. Mimi naamini sayari kama hizo zipo nyingi tu - nikimaanisha kuna uhai sehemu nyingine katika hii universe.

Mara nyingi wanasayansi wanatafuta dalili za uhai unaofanana na sisi. Inawezekana kuna viumbe (hapa duniani kwetu, au kwenye sayari au solar system nyingine) ambao hawafanani na sisi kimaumbile (yaani sio carbon-based kama sisi). Viumbe (kama robot zetu) ambao ni silicon-based wanaweza kuwepo lakini sisi hatuwatafuti. Inawezekana wakawa viumbe wasioonekana hapa hapa duniani (kama jini) lakini tunashindwa kuwasiliana nao. Labda tujikite zaidi katika kutafiti ukweli wa hawa majini na maisha yao (kama kweli wapo). Ajira nzuri sana hii kwa waganga wa kienyeji.
 
Ilipo blackhole yenyewe hapaonekani (mwanga unamezwa na hii blackhole). Lakini karibu na hiyo blackhole kunakuwa na mkusanyiko mkubwa (concentration) ya nyota zinazoizunguuka hii blackhole. Mradi zipo kwenye orbits zao basi haziwezi kumezwa. Zikisesereka tu kuangukia kwenye blackhole basi zinamezwa pamoja na mwanga wake.
Ni kama mtu anavuka sehemu kwa kutumia kamba huku chini kukiwa na korongo kubwa sana
 
Mkuu Kifyatu naomba nikusumbue tena kwa suali jengine.
Je imekuaje ikatokea sisi wanadamu ndio tukawa hapa kwenye sayari ya dunia ambako imekuwa kwetu rahisi kimazingira kuishi?.
Kwa nini tusingejikuta kwenye Jupiter huko au Uranus au hata kwenye sayari yeyote katika hii solar system yetu?.
Mkuu Kifyatu

Naomba urejee kulijibu hili swali tena kama hutojali maana nmeona kuna kipengele ambacho ni muhimu sana kimerukwa hapo

Kwanini sisi binadamu tukajikuta tuko sayari hii ya dunia na si Jupiter?
 
Usijali mkuu nitajaribu kudadavua zaidi hii mada. Sote tuko hapa JF kujifunza.

1. super nova ni nini na zinalipuka mara ngapi ili sisi tupate hizo faida zake
Super nova inapolipuka hutengeneza black hole na vumbi linalobaki hujikusanya na kutengeneza sayari kama dunia yetu. Baada ya hizi sayari kutengenezwa basi zinapitia process ya evolution. Kama sayari ina vigezo vizuri kama dunia yetu (joto, maji, nk.) basi maisha yanaweza kuanza kwa hii njia ya evolution (from simple amino acids, to DNA, to one-celled organisms, to multi-celled creatures to humans, animals, fish, etc.)
Mkuu,
kwanini ni sayari ya Dunia ndio yenye vigezo vya kuweza kuishi watu? wakati sayari kama Dunia nyingi zimetengenezwa tokana na Black holes? Mkuu huoni kama mwanadamu yuko very specific? structures and spiritual? Ina maana DNA Peke yake imemfanya awe jinsi alivyo?
 
Mkuu Kifyatu

Naomba urejee kulijibu hili swali tena kama hutojali maana nmeona kuna kipengele ambacho ni muhimu sana kimerukwa hapo

Kwanini sisi binadamu tukajikuta tuko sayari hii ya dunia na si Jupiter?
Kwa jibu la ki-imani tunaweza kusema Mungu mwenyewe ametuweka hapa duniani. Mimi si mbobezi wa imani za dini kwa hiyo nitashindwa kuitetea dhana hii.

Lakini ki-sayansi, gravity ya Jupiter ni kubwa kiasi ya kwamba tukienda huko tungekandamizwa na kuwa kama chapati. Kuna chombo (probe) walioipeleka NASA ndani ya Jupiter. Baada ya muda mfupi wa kutuma taarifda za upepo mkali na vimbunga, ilizima haraka sana ilipo-register gravity ya hali ya juu sana.

Hii haina maana hakuna uhai ndani ya Jupiter, la, bali sio wa viumbe kama sisi. Kama tunataka mahala pengine tunapoweza kuishi sisi katika hii solar system yetu basi inabidi pawe na vigezo vinavyofanana na hapa kwetu. Ndio maana wanasayansi wamejikita kupeleka watu Mars kwa sababu kuna uwezekano wa kutengeneza maandhari ya sisi kuishi.

Sijui kama nimelijibu swali lako?
 
Mkuu,
kwanini ni sayari ya Dunia ndio yenye vigezo vya kuweza kuishi watu? wakati sayari kama Dunia nyingi zimetengenezwa tokana na Black holes? Mkuu huoni kama mwanadamu yuko very specific? structures and spiritual? Ina maana DNA Peke yake imemfanya awe jinsi alivyo?
Mimi binafsi sina ugonvi na imani za kidini. In fact, falsafa yangu mimi ni kutokupuuzia dhana yoyote ile. Hii ni kwa sababu sayansi bado inashindwa kuelezea mambo mengi sana - kama hili swali lako.

Kwa maono yangu ni kuwa hii universe ni kubwa sana na tunachungulia katika kasehemu kadogo sana (solar sysytem yetu) kutafuta dalili za viumbe wengine. Nina imani kubwa sana kuwa somewhere kwenye hii universe yetu kuna viumbe wengine. Wanaweza wasifanane na sisi kimaumbile, kiakili, nk., lakini naamini wapo. Ni muda tu tunaouhitaji ili tuwa(vi)gundue viumbe hawa.

Je na huko pia ni mkono wa Mungu? Kama wewe ni wa imani basi universe yote ametengeneza Muumba kwa hiyo utakuwa unauliza jibu.
 
Kifyatu na wadau wengine habari zenu?

kwanza samahan sana kwa kuchelewa kuleta mrejesho hapa kuhusu Faida za rad hapa dunian na pili samahan kwa kusababisha baadh ya maswal na hoja kushindwa kukibiwa hapa kwa sababu ya kusubili majibu yangu kuhusu faida za radi,!

Naomba nikili kuwa nimeshindwa kupata hayo majawabu ya faida za rad labda kwa sababu ya uwezo wangu mdogo wa kucheza na mambo ya internet kwa sababu kila niki google kwa lugha ya kiswahil naona majibu yanakuja hayarizish na mengi yanakuja kwa njia za kidin na mimi sio mzur sana kwenye lugha za kisayans na hasa kwa kingereza.

Ivyo bas nikawa najihis mwenye hatia endapo ningeamua kuwaletea majibu yasio na ujazo uliojitosheleza kwa watu wenye uelewa mkubwa humu kuliko mm kuhusu maswala ya kisayans na ivyoo ningekuwa sijawatendea haki sababu ningeshindwa kujibu maswali ambayo mngeniuliza,!

naomba niwasilishe faida za rad japo sitokuwa na maelezo yaliojitosheleza so ntaomba mkuu Kifyatu atolee maelezo kama niko sahihi au laa,'
1) Mbolea
2)uwepo wa rad usababisha mvua kubwa sababu ya ule mkandamizo wa umeme
3)cabon

Uislamu na suala la radi + Sauti
 
Mimi binafsi sina ugonvi na imani za kidini. In fact, falsafa yangu mimi ni kutokupuuzia dhana yoyote ile. Hii ni kwa sababu sayansi bado inashindwa kuelezea mambo mengi sana - kama hili swali lako.

Kwa maono yangu ni kuwa hii universe ni kubwa sana na tunachungulia katika kasehemu kadogo sana (sola sysytem yetu) kutafuta dalili za viumbe wengine. Nina imani kubwa sana kuwa somewhere kwenye hii universe yetu kuna viumbe wengine. Wanaweza wasifanane na sisi kimaumbile, kiakili, nk., lakini naamini wapo. Ni muda tu tunaouhitaji ili tuwa(vi)gundue viumbe hawa.

Je na huko pia ni mkono wa Mungu? Kama wewe ni wa imani basi universe yote ametengeneza Muumba kwa hiyo utakuwa unauliza jibu.
mkuu me naamini hapo kwenye black hole ndio source ya kila kitu,na pengine Mungu ndipo anapoishi
 
Kifyatu na wadau wengine habari zenu?

kwanza samahan sana kwa kuchelewa kuleta mrejesho hapa kuhusu Faida za rad hapa dunian na pili samahan kwa kusababisha baadh ya maswal na hoja kushindwa kukibiwa hapa kwa sababu ya kusubili majibu yangu kuhusu faida za radi,!
Naomba nikili kuwa nimeshindwa kupata hayo majawabu ya faida za rad labda kwa sababu ya uwezo wangu mdogo wa kucheza na mambo ya internet kwa sababu kila niki google kwa lugha ya kiswahil naona majibu yanakuja hayarizish na mengi yanakuja kwa njia za kidin na mimi sio mzur sana kwenye lugha za kisayans na hasa kwa kingereza.,
Ivyo bas nikawa najihis mwenye hatia endapo ningeamua kuwaletea majibu yasio na ujazo uliojitosheleza kwa watu wenye uelewa mkubwa humu kuliko mm kuhusu maswala ya kisayans na ivyoo ningekuwa sijawatendea haki sababu ningeshindwa kujibu maswali ambayo mngeniuliza,!'
naomba niwasilishe faida za rad japo sitokuwa na maelezo yaliojitosheleza so ntaomba mkuu Kifyatu atolee maelezo kama niko sahihi au laa,'
1) Mbolea
2)uwepo wa rad usababisha mvua kubwa sababu ya ule mkandamizo wa umeme
3)cabon

Uislamu na suala la radi + Sauti
Asante baraka bb kwa mrejesho. Hujakosea kuhusu mbolea (na nitaelezea) lakini nitakupa alama ya B+ kwa sababu hukuelezea:
  • radi inatoaje mbolea na
  • kwa nini radi pekee ndio ilioleta uhai wetu viumbe wote hapa duniani.
Mvua kubwa haisababishwi na radi bali radi husababishwa na mawingu mazito ambayo yanaleta mvua kubwa.

Sasa nielezee hizo point mbili za juu:

Radi inatoaje mbolea?
78% ya hewa yetu tunayopumua ni Nitrogen. Hii hewa tunaivuta lakini hatuitumii (nikimaanisha tunaitoa kama tunavyoivuta). Tunatumia Oxygen tu kwa uhai wetu. Unaweza ukafikiria kuwa sasa faida ya hii Nitrogen ni nini?

Mimi na mkuu neo1 tulizungumzia kitu kinachoitwa plasma hapo awali. Wakati wa radi ule umeme na moto mkali wake unatengeneza plasma ya hewa yoyote ile inayoipitia. Lakini hasa hii plasma ya Nitrogen ni muhimu kwa sababu katika hali hiyo, nitrogen plasma ikianguka aridhini na mvua inakuwa rahisi kuchanganyika (react) na madini nyingine aridhini na kutengeneza NITRATES. Ni hizi nitrates ambazo ndio mbolea inayoweza kutumika na mmea kutengeneza chakula chake na kukua. Hewa ya Nitrogen kama ilivyo angani haiwezi kuchanganyika na madini aridhini kutengeneza Nitrates, inahitaji radi kutengeneza plasma ya Nitrogen kwanza.

Kwa nini radi pekee ndio ilioleta uhai wetu viumbe wote hapa duniani?
Ili mmea utengeneze proteins unahitaji Nitrogen ambayo inaipata kama nitrates kutoka aridhini. Bila ya hizi nitrates basi mmea usingeweza kutengeneza proteins, na ungekufa. Wanyama wakila hii mimea wanachukua hizo proteins za mmea na kutengeneza protein zao. Bila ya hizi proteins za mimea, wanyama (viumbe hai pamoja na sisi binadamu) wa(tu)singekuwepo hapa duniani. Kwa hiyo mkuu baraka bb, kila unapotunisha misuli yako basi uishukuru RADI kwa kuwezesha huwa na hizo proteins zilizojenga mwili wako.

Mars
Mkuu neo1 uliuliza swali kuhusu sayari ya Mars na ni nini cha kufanya ili watu na mimea iwepo (or something like that). Nilikujibu kuwa tunahitaji kupanda miti kwa sababu 96% ya hewa yake ni Carbon Dioxide inayohitajika na miti halafu miti itapumua Oxygen tunayoihitaji sisi watu na wanyama. Lakini nilitoa ilani kuwa hewa ya Mars ina 2-3% Nitrogen. Nikasema hii inaweza kuleta utata kidogo. Nilimaanisha kuwa kama hii asilimia ndogo ya nitrogen itaathiri upatikanaji wa NITRATES za kutosha kupitia radi, nitrogen plasma na mvua. Sijui jibu sahihi la hofu yangu hii.
 
Back
Top Bottom