Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Mkuu kifyatu, kama hautojali, naomba unisaidie nondo zote (notes) zinazohusu astrology.
 
Rangi nyekundu ya Mars ni shauri ya rangi ya udongo wake kama hapa duniani (red coffee soil) kwenye sehemu fulani.

Kufix atmosphere ndio mpango kamili (kuongeza hewa ya Oxygen). Huu ni mpango wa muda mrefu kwa kupanda miti. Katika kipind cha muda mfupi watategemea kutengeneza Oxygen yao kutokana na maji yaliyopo. Maana kubeba mitungi ya hewa kila uendapo.

Kuhusu gravity hii itabidi miili ya wakazi wa huko izoee tu gravity ndogo.

Miezi ya Mars haitaathiri maisha. Unafikiri kama kila usiku wetu tungekuwa na mbalamwezi tungechukia?

Ukiwa chini ya mwamba au pango kutakuwa na kivuli.
mkuu upo? nina vijiswali kidogo hapa
 
Nice to have you back Kifyatu
Kuna maswali huko juu niliuliza ila sikupata maelezo..ukiwa na muda naomba unisaidie majibu
 
Mkuu Kifyatu tueleze kuhusu kifaa kilichopo Jupiter.
Nini wanategemea kupata kwa muda huo ambapo kitakuwa huko!
Jupiter yenyewe Kama wana vyoeleza ni kuwa ni gas planet >Ina helium na hydrogen same as jua .sa mbona yenyewe It doesn't burn Kama jua??
 
Jupiter ingekuwa kubwa kidogo tu basi ingeweza kuwa jua (nikimaanisha nuclear fusion ingetokea na kutoa mwanga na joto kama jua letu). Kibiriti kinachowasha hii nuclear fusion (Hydrogen atom mbili kuungana na kuwa Helium + Nishati) ni GRAVITY. Gravity ikiwa kubwa ya kutosha basi hii chain-reaction inatokea tu yenyewe. Sasa hivi Gravity ya Jupiter haijafikia kiwango hicho (lakini ni kubwa kiasi cha kukandamiza carbon na kutengeneza Diamond. Yes, Jupiter ina mvua ya almasi).

Utafiti wa zamani ulipeleka chombo katika anga la Jupiter lakini kwa gravity yake kubwa hiki chombo kilikufa. Sasa hivi wanataka ku-orbit Jupiter na kuichunguza kwa remote-sensing. Off-course miezi ya Jupiter inachunguzwa kiundani sana kwa sababu kama kuna uhai kule basi utakuwa kwenye hii miezi.
 
Mkuu kifyatu, kama hautojali, naomba unisaidie nondo zote (notes) zinazohusu astrology.
Mkuu samahani sikukujibu swali lako naona wakati ule sikuliona.

Kama ambavyo Astronomy ni hobby yangu, hivyo hivyo Astrology (unajimu) pia ni hobby yangu. Hizi taaluma mbili nimejifunza sambamba na kiundani. Nimeamua kutojadili Unajimu hapa JF kwa sababu watu wengi wanaitumia vibaya taaluma hii. Kuna watu hawatoki nje asubuhi mpaka wasome nyota zao - hayo ni matumizi mabaya ya elimu hii (ingawaje watu wametengeneza utajiri kwa kutoa utabiri kwa watu).

Sasa mimi ninaitumiaje elimu hii ya Unajimu?
Mimi nafanya zaidi utafiti (Research) kuhusu uhusiano kati ya matukio (yaliokwisha pita) kwa watu (nikianza na mimi na watu wa karibu yangu), miji, nchi, dunia; na mipangilio ya jua, sayari, mwezi, na vinginevyo angani. Hii inanisaidia kuona kama ningeweza kutabiri matokeo kutokana na mipangilio wa nyota.

Kutokana na models nilizo nazo kwenye computer yangu ninaweza kuona kilichokuwa angani (nyota/sayari) as far back as wakati wa kuzaliwa kwa YESU (zaidi ya miaka 2,000 iliopita). Huu utafiti ninaoufanya unanijengea kitita cha elimu (knowledge base) ninayoweza kuitumia kutabiri matukio ya siku za usoni. Wanajimu wanaotabiri nyota wanatumia maelekezo ya wanajimu wa zamani. Ninachokifanya mimi ni kuona kama hawa wanajimu wa zamani walikuwa sahihi na kama ninaweza kuchangia katika hii pool ya ilmu ya unajimu.

Basi kutokana na ninachokifanya katika hii tasnia ya unajimu, siwezi kujibu swali lako kama ambavyo ungependa.

Samahani.
 
Mkuu Kifyatu nieleze kuhusu Goldilock zone.
Inaaminika ndo zone ina support life!!!.
Vp ziko ngap kwenye observable universe
 
Mkuu Kifyatu nieleze kuhusu Goldilock zone.
Inaaminika ndo zone ina support life!!!.
Vp ziko ngap kwenye observable universe
Goldilocks (yule mtoto wa kike aliepotea mwituni na kuingia kwenye pango la madubu au bears -- hadithi ya watoto wa shule za vidudu) zone ni zone ya kawaida (average zone). Katika universe kuna sehemu zenye extremes conditions (kama joto kali sana au baridi kali sana au gravity kubwa kama za blackholes) ambako uhai (kama wetu) hauwezi kushamiri. Lakini kuna sehemu chache (kama dunia yetu) ambako hali yake ni ya wastani (just right) kwa maisha kama yetu. Katika solar system yetu mpaka sasa bado hatujaona sehemu nyingine inayoweza ku-support maisha (kama yetu) isipokuwa hapa duniani kwetu - na pengine Mars. Hizi space missions nyingi zinatumwa kuona kama kuna sehemu nyingine tunakoweza kuishi.

Mimi naamini kuwa katika hii universe yetu yenye utitiri wa galaxies, nyota, na sayari ni lazima (law of probabilities) kutakuwa na sehemu nyingi tu zenye maandhari kama ya hapa duniani kwetu. Ni muda tu tunaohitaji kupaona.

Kuna Goldilocks Zones za aina ngapi?
Uwepo wa maisha lazima tuuangalie kwa mtazamo mwingine. Inawezekana kabisa kuna maisha katika sehemu nyingine kwenye hii solar system yetu (au kwengine) lakini sio kama maisha yetu sisi (carbon-based). Inawezekana kabisa kwamba kuna viumbe wengine wa aina tofauti (labda ni silicone-based au based on elements nyingine). Tumesikia riwaya za majini, aliens, n.k., wanaoonekana katika nyakati na mazingara tofauti. Kama hii ni kweli basi hizi Goldilocks zone zipo nyingi za aina tofauti (zone ya sisi binadamu, zone ya majini, n.k.).

Tukipanua uga wa kutafsiri maisha ni nini au ni kitu gani basi tunaweza kushangaa kuona kumbe kuna viumbe wa aina nyingi tu (na wengine tunaishi nao bali hatuwaoni tu) hapa duniani, solar system yetu, na universe.

Hapa ndipo panapoleta utamu wa sayansi.
 
Mkuu samahani sikukujibu swali lako naona wakati ule sikuliona.

Kama ambavyo Astronomy ni hobby yangu, hivyo hivyo Astrology (unajimu) pia ni hobby yangu. Hizi taaluma mbili nimejifunza sambamba na kiundani. Nimeamua kutojadili Unajimu hapa JF kwa sababu watu wengi wanaitumia vibaya taaluma hii. Kuna watu hawatoki nje asubuhi mpaka wasome nyota zao - hayo ni matumizi mabaya ya elimu hii (ingawaje watu wametengeneza utajiri kwa kutoa utabiri kwa watu).

Sasa mimi ninaitumiaje elimu hii ya Unajimu?
Mimi nafanya zaidi utafiti (Research) kuhusu uhusiano kati ya matukio (yaliokwisha pita) kwa watu (nikianza na mimi na watu wa karibu yangu), miji, nchi, dunia; na mipangilio ya jua, sayari, mwezi, na vinginevyo angani. Hii inanisaidia kuona kama ningeweza kutabiri matokeo kutokana na mipangilio wa nyota.

Kutokana na models nilizo nazo kwenye computer yangu ninaweza kuona kilichokuwa angani (nyota/sayari) as far back as wakati wa kuzaliwa kwa YESU (zaidi ya miaka 2,000 iliopita). Huu utafiti ninaoufanya unanijengea kitita cha elimu (knowledge base) ninayoweza kuitumia kutabiri matukio ya siku za usoni. Wanajimu wanaotabiri nyota wanatumia maelekezo ya wanajimu wa zamani. Ninachokifanya mimi ni kuona kama hawa wanajimu wa zamani walikuwa sahihi na kama ninaweza kuchangia katika hii pool ya ilmu ya unajimu.

Basi kutokana na ninachokifanya katika hii tasnia ya unajimu, siwezi kujibu swali lako kama ambavyo ungependa.

Samahani.

Asante shukrani.
 
halafu ningependa ugusie na constellation canis major kuna nyota yaitwa sirius inang'aa sana kuliko ile 'giant' VY sasa ipi ni kubwa hapo?
 
pia mkuu ungegusia uhusiano wa constellation sagittarius na katikati ya milkway yetu(black hole)
 
Back
Top Bottom