Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

mkuu supernova ya mwisho ilitokea lini na kwanini inaweza kukatika miaka hatuoni supernova wakati zipo nyota zilishazeeka tokea miaka mingi nyuma ambapo kwa miaka hii tuliopo kwa speed ya mwanga wake tugeshuhudia supernova nyingi tu?
supernova kubwa ya mwisho iliyotokea tuliona mwanga wake mwaka 1987 na inaitwa supernova 1987A,mwanga wake mpaka kufika hapa duniani ulitumia miaka 160,000 kwa hiyo nyota yake ili pasuka miaka 160,000 iliyopita ila sisi tumekuja kujua mwaka 1987
 
mkuu supernova ya mwisho ilitokea lini na kwanini inaweza kukatika miaka hatuoni supernova wakati zipo nyota zilishazeeka tokea miaka mingi nyuma ambapo kwa miaka hii tuliopo kwa speed ya mwanga wake tugeshuhudia supernova nyingi tu?

Supernova ya mwisho kurekodiwa kwa mujibu wa Wiki ya Supernovae History ilionekana January 22 2014.

Supernova bila shaka zipo nyingi, ila uwezo wetu wa kuzifuatilia unakuwa mdogo. Kumbuka ingawa supernovae ziko bright sana - zingine zinaweza kuwaka mpaka nyota ikaonekana mchana, kama nyota ipo karibu- lakini nyota nyingi zipo mbali sana.

Pia kuna nyota chache ambazo ziko mbali nasi sana kiasi kwamba mwanga wake hautatufikia daima, na hivyo, hata zinavyopata supernova hatutajua. Hizi nyota zinakuwa hivi kwa sababu ukijumlisha umbali wake kutoka kwetu na effect ya "expansion of the universe" (kupanuka kwa space) mwanga wa nyota hizi hata kama unasafiri kwa kasi ya mwanga, hautaweza kutufikia, kwa maana ya kwamba, kadiri mwanga unavyosafiri kutaka kutufikia ndivyo expansion of the universe inavyozidisha umbali kati yetu na nyota hizi, remember the expansion of the universe is dependent on distance, with more distant galaxies moving away from us faster than galaxies that are closer to us.

This actually complicates the entire concept of distance. For more go this Cornell piece.

How do we define distance in an expanding universe? (Intermediate) - Curious About Astronomy? Ask an Astronomer

Last supernova

History of supernova observation - Wikipedia, the free encyclopedia

On January 22, 2014, students at the University of London Observatory spotted an exploding star SN 2014J in the nearby galaxy M82 (the Cigar Galaxy). At a distance of around 12 million light years, the supernova is one of the nearest to be observed in recent decades.[67]
 
Me nimedata hapo tu jupiter inanyesha mvua ya almasi???
Tafuta hata ungo wa bibi tuzamie ndugu tutarudi mabilionea!! Si nasikia ungo kufumba na kufumbua unakuwa ushavuka bara hadi bara!!! It means speed yake si ya kawada tunaweza kufika bro
 
Supernova ya mwisho kurekodiwa kwa mujibu wa Wiki ya Supernovae History ilionekana January 22 2014.

Supernova bila shaka zipo nyingi, ila uwzo wetu wa kuzifuatilia unakuwa mdogo. Kumbuka ingawa supernovae ziko bright sana - zingine zinawza kuwaka mpaka nyota ikaonekana mchana, kama nyota ipo karibu- lakini nyota nyingi zipo mbali sana.

Pia kuna nyota chache ambazo ziko mbali nasi sana kiasi kwamba mwanga wake hautatufikia daima, na hivyo, hata zinavyopata supernova hatutajua. Hizi nyota ziakuwa hivi kwa sababu ukijumlisha umbali wake kutoka kwetu na effect ya "expansion of the universe" (kupanuaka kwa space) mwanga wa nyota hizi hata kama unasafiri kwa kasi ya mwanga, hautaweza kutufikia, kwa maana ya kwamba, kadiri mwanga unavyosafiri kutaka kutufikia ndivyo expansion of the universe inavyozidisha umbali kati yetu na nyota hizi, remember the expansion of the universe is dependent on distance, with more distant galaxies moving away from us faster than galaxies that are closer to us.

This actually complicates the entire concept of distance. For more go this Cornell piece.

How do we define distance in an expanding universe? (Intermediate) - Curious About Astronomy? Ask an Astronomer

Last supernova

History of supernova observation - Wikipedia, the free encyclopedia

On January 22, 2014, students at the University of London Observatory spotted an exploding star SN 2014J in the nearby galaxy M82 (the Cigar Galaxy). At a distance of around 12 million light years, the supernova is one of the nearest to be observed in recent decades.[67]
Roho imeniuma kusoma hapo kuwa aliyeona hilo tukio ni mwanafunzi!! Daaah!! Wenzetu wanasoma aiseee
 
Katika sayansi ya particle physics (chembe chembe ndogo ndani ya atom) wanasayansi wameona uwezekano wa kuwepo na chembe (particles) zinazokinzana na chembe za kawaida. Tumejifunza kuwa atom ina
  • Protons
  • Neutrons
  • Electrons
Antimatter ina chembe zinazokinzana na hizi za kawaida
  • Anti-protons
  • Anti-neutrons
  • Positrons (Anti-electrons)

Ilivyo ni kuwa Antimatter ikikutana na matter ya kawaida basi zinajimaliza na matokeo yake ni nishati tupu kufuatia kanuni za Albert Einstein kuwa:
Nishati E = mC-squared.

Kwa hiyo kama una antimatter ya kutosha kwenye chombo cha usafiri angani basi kazi yake ni kumeza matter inayokutana nayo njiani na unapata nishati isiyokuwa na ukomo kwa safari yako. Tatizo ni kuwa mpaka sasa wanasayansi hawajaweza kuwa na antimatter ya uhakika (stable).

Cha muhimu kujua ni kuwa swala la antimatter limetoka kwenye nadharia na sasa kilichobaki ni sayansi tu ya kuikusanya ya kutosha. Hii ni kazi ngumu sana na sidhani kama sisi na vizazi vyetu vitabahatika kuweza kutumia hii nishati ya antimatter.
mkuu unaweza ukatuelezea kidogo kuhusu hii van allen radiation belt lpo vipi na hatari yake ipoje kwa vitu vinavyotoka au kuingia duniani
 
Napoangaliaga angani wakati wa usiku huwa naona nyota zingine ambazo hazina mwanga wa rangi moja,yan inabadilika badilika mara nyekundu,kijan,bluu.
Je hizi nyota ni za aina gani? mana kuna mtu katika stori za utoto alinambia eti zile ni satelaiti
Pia nyota chanzo chake cha mwanga ni kipi?
Karibuni wadau wa Sayansi ya anga
Thank you
 
Supernova ya mwisho kurekodiwa kwa mujibu wa Wiki ya Supernovae History ilionekana January 22 2014.

Supernova bila shaka zipo nyingi, ila uwzo wetu wa kuzifuatilia unakuwa mdogo. Kumbuka ingawa supernovae ziko bright sana - zingine zinawza kuwaka mpaka nyota ikaonekana mchana, kama nyota ipo karibu- lakini nyota nyingi zipo mbali sana.

Pia kuna nyota chache ambazo ziko mbali nasi sana kiasi kwamba mwanga wake hautatufikia daima, na hivyo, hata zinavyopata supernova hatutajua. Hizi nyota ziakuwa hivi kwa sababu ukijumlisha umbali wake kutoka kwetu na effect ya "expansion of the universe" (kupanuaka kwa space) mwanga wa nyota hizi hata kama unasafiri kwa kasi ya mwanga, hautaweza kutufikia, kwa maana ya kwamba, kadiri mwanga unavyosafiri kutaka kutufikia ndivyo expansion of the universe inavyozidisha umbali kati yetu na nyota hizi, remember the expansion of the universe is dependent on distance, with more distant galaxies moving away from us faster than galaxies that are closer to us.

This actually complicates the entire concept of distance. For more go this Cornell piece.

How do we define distance in an expanding universe? (Intermediate) - Curious About Astronomy? Ask an Astronomer

Last supernova

History of supernova observation - Wikipedia, the free encyclopedia

On January 22, 2014, students at the University of London Observatory spotted an exploding star SN 2014J in the nearby galaxy M82 (the Cigar Galaxy). At a distance of around 12 million light years, the supernova is one of the nearest to be observed in recent decades.[67]
mkuu hivi hii speed ya mwanga unaopita kwenye hewa au maji ni sawa na unapopita kwenye vacuum au anga za juu?? au speed inatofautiana?
 
mkuu unaweza ukatuelezea kidogo kuhusu hii van allen radiation belt lpo vipi na hatari yake ipoje kwa vitu vinavyotoka au kuingia duniani
Swali lako ni fupi lakini naona linahitaji maelezo ya kina kulijibu. Kama kawaida maelezo mengi ya kitaalamu unaweza kuyapata kwenye mitandao. Hapa ngoja nijaribu kueleza kimatumbi.

Sayansi kavu kavu:
Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya umeme (electricity au flow of electrons) na smaku (magnetism). Kama ukiwa na smaku yenye nguvu halafu ukaleta charged particles kama protons au electrons basi hizi charged particles zitakamatwa na kubaki katika magnetic field ya hii smaku. Hii, kwa kifupi, ndiyo sayansi ya van Allen belts.

Sayari zenye nguvu za smaku:
Sayari nyingi, kama dunia yetu, zina smaku (magnet) kubwa sana katikati yake (hii husababishwa na chuma kilichoyeyuka ndani ya dunia kwa moto na kuzunguuka kama uji unaochemka kutoka kaskazini kwenda kusini). Hii smaku katikati ya dunia yetu (au sayari nyingine) inaipa dunia mionzi ya smaku (magnetic field) kutoka kasikazini mpaka kusini. Ni hii magnetic field ndiyo inayoweza kutufanya tutumie dira (campus) kujua kaskazini au kusini ni wapi. Ni hii hii magnetic fields ndio inayokamata charged particles angani na kutengeneza hizi van Allen belts.

Van Allen Belt(s):
Jua letu linatoa mionzi na upepo wa hii mionzi (radiations & radiation storms) kuelekea pande zote. Sasa kama ilivyo radi inavyotengeneza plasma (ionized gas - rejea mabandiko kuhusu plasma humu kwenye huu uzi) hii mioinzi kutoka kwenye jua ikifika hapa duniani basi inazaba hewa yetu na hii hewa inakuwa ionized (charged particles kama protons na electons). Huu ukanda wenye hizi charged particles (kuanzia 1,000 mpaka 60,000 km kwenda juu) ndio unaojulikana kama van-Allen belt (uligunduliwa 1958 na mwanasayansi wa kiMarekani mwenye hili jina). Kila sayari yenye ukanda wa mionzi ya smaku (magnetic field) basi utakuwa na hizi van-Allen belts.

Faida /Athari ya hizi van Allen radiation fields.
Sisi hapa duniani tuna bahati sana kuwa na hizi van-Allen belts kwa sababu mionzi mingi ya hatari kwa maisha yetu inamezwa au kuelekezwa kuizunguuka dunia na kuendelea na safari yake nje ya dunia yetu kwa sababu ya hizi van-Allen belts au zones. Tusingekuwa na smaku aridhini na hizi van Allen belts basi hewa yote ingepeperushwa nje ya dunia yetu na huu upepo wa jua na maisha hapa duniani yasingekuwepo kabisa.

Kwa sababu van Allen belt ina charged particles, basi chombo kinachokuwa kwenye hii belt lazima kijikinge (shield) ama sivyo mitambo yao ya ki-elektroniki inaweza kuharibiwa. Kuna wakati hii belt inaweza kukuwa mpaka kufikia orbits za satelite zetu na kuleta madhara. Vyombo vyote vinavyotumwa angani (wanajua uwepo wa huu ukanda hatarishi na) hujikinga ipaswavyo.

I hope hii imesaidia.
 
Swali lako ni fupi lakini naona linahitaji maelezo ya kina kulijibu. Kama kawaida maelezo mengi ya kitaalamu unaweza kuyapata kwenye mitandao. Hapa ngoja nijaribu kueleza kimatumbi.

Sayansi kavu kavu:
Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya umeme (electricity au flow of electrons) na smaku (magnetism). Kama ukiwa na smaku yenye nguvu halafu ukaleta charged particles kama protons au electrons basi hizi charged particles zitakamatwa na kubaki katika magnetic field ya hii smaku. Hii, kwa kifupi, ndiyo sayansi ya van Allen belts.

Sayari zenye nguvu za smaku:
Sayari nyingi, kama dunia yetu, zina smaku (magnet) kubwa sana katikati yake (hii husababishwa na chuma kilichoyeyuka ndani ya dunia kwa moto na kuzunguuka kama uji unaochemka kutoka kaskazini kwenda kusini). Hii smaku katikati ya dunia yetu (au sayari nyingine) inaipa dunia mionzi ya smaku (magnetic field) kutoka kasikazini mpaka kusini. Ni hii magnetic field ndiyo inayoweza kutufanya tutumie dira (campus) kujua kaskazini au kusini ni wapi. Ni hii hii magnetic fields ndio inayokamata charged particles angani na kutengeneza hizi van Allen belts.

Van Allen Belt(s):
Jua letu linatoa mionzi na upepo wa hii mionzi (radiations & radiation storms) kuelekea pande zote. Sasa kama ilivyo radi inavyotengeneza plasma (ionized gas - rejea mabandiko kuhusu plasma humu kwenye huu uzi) hii mioinzi kutoka kwenye jua ikifika hapa duniani basi inazaba hewa yetu na hii hewa inakuwa ionized (charged particles kama protons na electons). Huu ukanda wenye hizi charged particles (kuanzia 1,000 mpaka 60,000 km kwenda juu) ndio unaojulikana kama van-Allen belt (uligunduliwa 1958 na mwanasayansi wa kiMarekani mwenye hili jina). Kila sayari yenye ukanda wa mionzi ya smaku (magnetic field) basi utakuwa na hizi van-Allen belts.

Faida /Athari ya hizi van Allen radiation fields.
Sisi hapa duniani tuna bahati sana kuwa na hizi van-Allen belts kwa sababu mionzi mingi ya hatari kwa maisha yetu inamezwa au kuelekezwa kuizunguuka dunia na kuendelea na safari yake nje ya dunia yetu kwa sababu ya hizi van-Allen belts au zones. Tusingekuwa na smaku aridhini na hizi van Allen belts basi hewa yote ingepeperushwa nje ya dunia yetu na huu upepo wa jua na masiha hapa duniani yasingekuwepo kabisa.

Kwa sababu van Allen belt ina charged particles, basi chombo kinachokuwa kwenye hii belt lazima kijikinge (shield) ama sivyo mitambo yao ya ki-elektroniki inaweza kuharibiwa. Kuna wakati hii belt inaweza kukuwa mpaka kufikia orbits za satelite zetu na kuleta madhara. Vyombo vyote vinavyotumwa angani (wanajua uwepo wa huu ukanda hatarishi na) hujikinga ipaswavyo.

I hope hii imesaidia.
hapo nimekupata sana shukrani mkuu
 
Swali zuri sana hili.

Cha kwanza kufahamu ni kuwa kupatwa kwa jua hutokea mwezi ukiwa mchanga (ukiwa karibu na jua), na kupatwa kwa mwezi hutokea wakati mwezi ni full moon (mbali kabisa na jua).

Kitu kingine cha kufahamu ni kuwa jua linapatwa kila mwezi (mwezi mchanga). Kinachotokea ni kuwa hiki kivuli cha mwezi kama hakiangukii ardhini basi sisi hatuoni kuwa jua limepatwa.

Kama dunia invyozunguuka katika mhimili wake basi ukichora msitari kati ya jua na mwezi, huu mstari sio siku zote unaigusa dunia yetu. Ni pale tu myumbo wa dunia utakapoiweka iguswe na huu mstari ndipo eclipse inapotokea.

Hii inatokana na kuwa kama ukichora bapa (au plane) ya dunia inavyolizunguuka jua, na ukichora plane ya mwezi inavyoizunguuka dunia, hizi planes mbili sio sawa. Ni nyakati chache tu ndio kivuli cha mwezi kinapoweza kuangukia duniani na tunaweza kuzitabiri hizi tarehe za eclipses.

Naomba ufafanue zaidi mkuu Kifyatu..
Natamani sana kujua ni jinsi gani hicho kivuli cha mwezi haki angukii kwenye dunia yetu. Na naomba unisaidie kujua ni jinsi gani mwezi unazunguka dunia. Asante
 
Mwezi unaizunguuka dunia kwa sababu umekamatwa na nguvu za mvutano (gravity) za dunia.

Lakini kiukweli, kwa sababu mwezi pia una gravity yake ingawaje ni ndogo kulinganisha na dunia yetu basi huu mzunguuko wa mwezi pia huifanya dunia iyumbe. Ni kama wewe uchukue jiwe zito ulifunge kamba halafu ulizunguushe. Lile jiwe litakuzunguuka lakini tukikuangalia wewe mzunguushaji tutakuona unasesereka pia. Hali hii inafanya bapa (plane) ya mzunguuko wa mwezi kubadilika badilika kulingana na bapa la mzunguuko wa dunia kwenye jua (Dunia hailiyumbishi jua kwa kiasi kama mwezi unavyoiyumbisha dunia).

Ni hizi tofauti za haya mabapa (planes) mawili (la dunia kulizunguuka jua na mwezi kuizunguuka dunia) ndio unaofanya ni mara chache tu kivuli cha mwezi kuangukia duniani.
 
Roho imeniuma kusoma hapo kuwa aliyeona hilo tukio ni mwanafunzi!! Daaah!! Wenzetu wanasoma aiseee
Kazi kama hizi mara nyingi hupewa research student. Kuna nyota nyingine zinavumbuliwa mpaka na amateur astronomers, wenyewe professionals wapo katika kutatua matatizo makubwa zaidi kufanya mahesabu huko, halafu wanakwambia angalia hapa utaona kitu.
 
mkuu hivi hii speed ya mwanga unaopita kwenye hewa au maji ni sawa na unapopita kwenye vacuum au anga za juu?? au speed inatofautiana?
Inategemea na medium.

Ona

Molecular Expressions Microscopy Primer: Physics of Light and Color - Speed of Light in Transparent Materials: Interactive Java Tutorial

javalightspeedfigure1.jpg
 
Kimondo ni kinatokana na nn?? Ni mara nyingi jion huwa naona kama yote au kitu kama nyote chenye mwanga mwekundu kitoka upande mmoja na kudondoka upande mwingine...bila kuona desitination...
 
Mkuu kifyatu hapa kwenye mvua ya almas!!!! Ni nini kinasababisha hiyo mvua maana duuuh mvua ya almasi!!!!!!!!!!
 
Kwa ajili ya ukubwa wa Jupiter, gravity yake (presha) na joto angani ni zaidi ya presha na joto chini ya dunia yetu iliyotengeneza almasi zetu. Kwa hiyo madini ya carbon iliyoko ndani ya Jupiter inakandamizwa na kugeuka almasi (kama ilivyo hapa duniani kwetu).

Kwa kuwa jupiter imejaa hewa zaidi, hii almasi inayotengenezwa kwenye anga la Jupiter huanguka kama mvua. Sisi hatuwezi kwenda huko na kuichota kwa sababu mtu (tumeumbwa na carbon nyingi) ukiingia kwenye anga la Jupiter na wewe utageuzwa kuwa "jiwe" au almasi.
 
Sayansi tamu sana ukiijua aisee

Hongera mkuu Kifyatu
 
Back
Top Bottom