mkuu unaweza ukatuelezea kidogo kuhusu hii van allen radiation belt lpo vipi na hatari yake ipoje kwa vitu vinavyotoka au kuingia duniani
Swali lako ni fupi lakini naona linahitaji maelezo ya kina kulijibu. Kama kawaida maelezo mengi ya kitaalamu unaweza kuyapata kwenye mitandao. Hapa ngoja nijaribu kueleza kimatumbi.
Sayansi kavu kavu:
Kuna uhusiano wa karibu sana kati ya
umeme (electricity au flow of electrons) na
smaku (magnetism). Kama ukiwa na smaku yenye nguvu halafu ukaleta charged particles kama protons au electrons basi hizi charged particles zitakamatwa na kubaki katika magnetic field ya hii smaku. Hii, kwa kifupi, ndiyo sayansi ya
van Allen belts.
Sayari zenye nguvu za smaku:
Sayari nyingi, kama dunia yetu, zina smaku
(magnet) kubwa sana katikati yake
(hii husababishwa na chuma kilichoyeyuka ndani ya dunia kwa moto na kuzunguuka kama uji unaochemka kutoka kaskazini kwenda kusini). Hii smaku katikati ya dunia yetu
(au sayari nyingine) inaipa dunia mionzi ya smaku
(magnetic field) kutoka kasikazini mpaka kusini. Ni hii magnetic field ndiyo inayoweza kutufanya tutumie dira
(campus) kujua kaskazini au kusini ni wapi. Ni hii hii magnetic fields ndio inayokamata charged particles angani na kutengeneza hizi van Allen belts.
Van Allen Belt(s):
Jua letu linatoa mionzi na upepo wa hii mionzi
(radiations & radiation storms) kuelekea pande zote. Sasa kama ilivyo
radi inavyotengeneza
plasma (ionized gas - rejea mabandiko kuhusu plasma humu kwenye huu uzi) hii mioinzi kutoka kwenye jua ikifika hapa duniani basi inazaba hewa yetu na hii hewa inakuwa ionized
(charged particles kama protons na electons). Huu ukanda wenye hizi charged particles
(kuanzia 1,000 mpaka 60,000 km kwenda juu) ndio unaojulikana kama
van-Allen belt (uligunduliwa 1958 na mwanasayansi wa kiMarekani mwenye hili jina). Kila sayari yenye ukanda wa mionzi ya smaku
(magnetic field) basi utakuwa na hizi van-Allen belts.
Faida /Athari ya hizi van Allen radiation fields.
Sisi hapa duniani tuna bahati sana kuwa na hizi van-Allen belts kwa sababu mionzi mingi ya hatari kwa maisha yetu inamezwa au kuelekezwa kuizunguuka dunia na kuendelea na safari yake nje ya dunia yetu kwa sababu ya hizi van-Allen belts au zones. Tusingekuwa na smaku aridhini na hizi van Allen belts basi hewa yote ingepeperushwa nje ya dunia yetu na huu upepo wa jua na maisha hapa duniani yasingekuwepo kabisa.
Kwa sababu van Allen belt ina charged particles, basi chombo kinachokuwa kwenye hii belt lazima kijikinge (shield) ama sivyo mitambo yao ya ki-elektroniki inaweza kuharibiwa. Kuna wakati hii belt inaweza kukuwa mpaka kufikia orbits za satelite zetu na kuleta madhara. Vyombo vyote vinavyotumwa angani (
wanajua uwepo wa huu ukanda hatarishi na) hujikinga ipaswavyo.
I hope hii imesaidia.