Swali zuri sana mkuu na wala usiombe radhi. Niko tayari kukuingiza ndani ya ulimwengu wa Kifyatu. Nami nakuomba radhi kwa jibu refu.
Kuna makundi ya aina tatu ya watu:
- Wanaoamini uwepo wa Mungu - Theists
- Wasioamini uwepo wa Mungu - Atheists
- Wasiojua na wanatafuta ukweli uko wapi - Agnostics
Wana sayansi wengi wapo kwenye hili kundi la tatu - Agnostics. Mimi ni agnostic mmojawapo.
Universe:
Unajua, ukiangalia ukubwa wa, na complexity ya, huu uimwengu wetu bado huwezi kuuelezea, hata kwa kutumia sayansi, kuwa ulianzaje. Kulikuwa na nini kabla ya
big bang? Je hii
Higgs boson (wanaiita
God particle) ni ishara ya kisayansi ya uwepo wa Mungu? Unaona. Kuna maswali mengi sana ambayo sayansi bado haiwezi kuyajibu. Kwa hiyo mwanasayansi yeyote yule anaesema yeye ana uhakika Mungu hayupo basi huyo ninamtilia mashaka na hiyo elimu yake.
Dini:
Mimi naziona dini kama vyama vile. Kila moja inavutia upande wake na kujigamba kuwa wao wanamuelewa Mungu kiundani kuliko wengine na kutoa masharti chungu tele ya kuwa muumini. Mimi nimeamua kutoyumbishwa na hizi dini mbalimbali na maelezo yao. Sasa ukiangalia composition ya dini unakuta ina sehemu mbili.
Dini = Spirituality (matumaini au hope au "ucha mungu") + Culture (mila na desturi)
Spirituality ni ile hali ya kuwa na matumaini kuwa utafanikiwa. Hata watu wasio na dini lakini wakiwa katika matatizo watategemea kuwa miujiza (mizimu, lady luck, n.k.) itatokea wasalimike. Watu hawa pia watanunua tiketi za bahati-nasibu wakitegemea watakuwa na bahati siku hiyo ya kushinda. Hii hali ya matumaini kuwa kuna kitu kitaiingilia kutatua matatizo yako ndio SPIRITUALITY.
Kwa wale wenye dini basi hii spirituality wanailinganisha na uwepo wa Mungu mwenye uwezo wote. Binadamu wote wanayo hii spirituality (awe na dini au sio). Ndio njia kuu ya sisi binaadamu tunayotumia kupambana na matatizo ya maisha kisaikolojia (coping mechanism).
Culture au mila/desturi ndiyo inayotengeneza dini.
- Uislam = Spirituality + mila za kiarabu
- Ukristo = Spirituality + mila za kizungu/kiyahudi
- Judaism = Spirituality + mila za kiyahudi
- Na kadhalika.
Kwa hiyo ukiondoa mila/desturi katika hizi dini basi dini zote zitafanana. Jaribu kufikiria.
Kwa mfano, kama wewe ni mwarabu basi mila/desturi za kabila lako ndio hizo hizo mila/desturi za dini yako. Ikiwa hivyo basi dini kwako ndio mwenendo wa maisha (a way of life) na hujilazimishi. Kwa wengine wote inabidi tujilazimishe tu (kuvaa hijab, kuswali ukielekea Makkah kwa kiarabu, kutokula nguruwe, n.k.) ili tuwe waislam.
Mara nyingi ufuasi wa dini unategemea ulivyokuzwa. Hata wanasayansi, kama wamekuwa katika familia zenye misimamo mikali wa kidini wataamini uwepo wa Mungu kufuatilia imani walizokuzwa nazo.
Mimi:
Hivyo basi mimi katika maisha yangu ni
Spiritual lakini sio
Religious. Hiki ndicho nilichomaanisha niliposema "
sina dini".
Natumaini umenielewa.