Ndio nimeibuka tu kutoka katika sunami la sikukuu. Familia raha lakini wanajua namna ya kukubana.
Ndio nimeanza kuandaa dondoo za maswala ya Quantum Physics. Ili kufanya hivi nimeona nianze mbali kidogo. Samahani kwa watakaochoshwa na marudio ya mambo wanayoyafahamu.
Nitagawanya haya maelezo katika makundi matatu:
- Physics ya vitu vikubwa au Classical/Newtonian Physics
- Umbile la Atom (ya kawaida na ilioko katika blackhole)
- Physics ya vitu vidogo (sub-atomic particles) au Quantum Physics/Mechanics
Baada ya hii elimu ya kawaida (general knowledge), nitafungua mjadala kuongelea mauzauza yaliyomo ndani ya Quantum Physics/Mechanics. Hapa tutajadili kama hii miujiza ya Quantum physics inaweza kuelezeka kwa kutumia dhana mbadala (uchawi, spirituality, nguvu ya mawazo, afterlife, n.k.). Je, sisi viumbe ni nani hasa? Yaani, tupo hapa duniani kiukweli au ni kiinimacho tu? Mimi sitakuwa mchangiaji mkuu katika hii sehemu, nitachokoza tu ili tupate maoni ya wataalam wengine. Hii elimu bado ni changa sana, sote tunaweza kujifunza kutoka kwa wenzetu hata kama hawakubobea katika sayansi. Dini, meditation, Astral projections, Ndoto, na hata uchawi utakaribishwa kuelezea kinachojulikana sasa na sayansi ya Quantum Physics.
Nitajaribu kuelezea katika lugha nyepesi ili tusiachane. Lakini natoa tahadhari, sasa tunaingia katika sayansi ya hali ya juu na mara nyingine nitategemea kuwa umefanya hata physics ya form 4 tu. Nitatumia Kiswahili muda wote lakini kuna sehemu kadhaa nitachanganya na kizungu (sio nyingi). Nikikukwaza mahala niulize haraka sana tusije tukakuacha kwenye mataa.
Naomba mnipe muda nijenge hizi hoja.
Mkuu
yonga na wengineo mnaoifahamu hii taaluma nakaribisha michango yenu. Mkiona napotoka au sijielezi vizuri naomba mnisahihishe mapema. Mimi sichukii usahihishwaji bali naukaribisha kwa hamu sana.