Ighombe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 1,181
- 675
Maelezo mazuri!....Naonba utufafanulie hapa ya kuwa ni kitu gani kingine utafiti wa kisaysnsi umebaini kuwa huenda kikaangamiza dunia?.Kuna Sayari mojawapo siikumbuki nilisoma mahali kuwa inapigwa sana na vimondo je kwa nature ya mifumo ya sayari hili haliwezi kutokea kwa Dunia yetu?Hii itatokea for sure, labda dunia yetu iangamizwe na kitu kingine kabla ya siku hiyo ya mwisho.
Jua letu kwa sasa linachoma hewa ya Hydrogen kutengeneza Helium. Itachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii Hydrogen. Hydrogen ikimalizika itaanza kuchoma helium kutengeneza element nyingine nzito.
Jua litakapoanza tu kutengeza chuma (Iron) basi hilo jiko la nuklia linakufa mara moja na kishindo kikubwa kitatokea (soma maelezo yangu ya awali kuhusu Super-Nova katika uzi huu huu). Jua letu halitakufa kwa kishindo kikubwa kama cha supernova bali kitatosha kutimua vumbi lenye joko kali litakaloimeza Mecury, Venus, sisi (Earth) na hata kuikaribia Mars.
Jibu rahisi la swali lako ni "NDIO", dunia yetu itakujamezwa na jua siku moja (hakuna utata hapa). Lakini itachukua mabilioni ya miaka kufikia huko.
Kwa sasa, wewe jivinjari tu na moja moto moja baridi ukijua wazi kuwa wewe, watoto wako, wajukuu, vilembwe, nk. wataamka kila asubuhi yao na kiliona jua kama lilivyo leo.
Cc kifyatu!