Ufahamu mfuko wa uwekezaji UTT

Hata kwenye mahindi kuna changamoto yake. Wewe unajua kununua na kuweka stooo tuu, aujui kuna wadudu kama panya, hali ya hewa na wengineo wanaweza wakaaribu hayo mazao. Kila kitu Kina changamoto. Tumia elimu kujibu maswala ya kielimu

Yeye katoa ushauri kazi kwako kufuata au kuachana nao
DSE ni kama unacheza kamali kwa bahati nzuri mm nipo kote mazao na niliwekeza kasenti kangu uko DSE

Kiufupi hakulipi aisee bei zinabadilika kama upepo,mapungufu mengine ni hawa brokers wa DSE unaweza ona hisa za kampuni ulizonazo zimepanda ukaamua kuuza,zoezi linachukua muda sana mpaka mwezi au zaidi adi ile bei iliyokushawishi uuze hisa zako utakuta imeporomoka

Mfano mzuri tarehe 4 ya mwezi august nilifanya process ya kuuza hisa zangu za kampuni Fulani niliwatumia Solomon brokers,aisee adi Leo wana mbwelambwela mpaka bei iliyonishawishi imeshuka kwa kifupi biashara ya hisa bongo ina discourage sana mkuu.

Kwenye mazao tunapoweka stoo huwa tunaweka dawa mpaka muda unaohitaji wewe kuuza na faida yake unaiona,na unauza kwa wakati ule unaodhani unafaa lakini DSE hill halipo unaweza hitaji kuuza Leo lkn process za brokers zikakusababishia hasara kwa sababu hawafanyi kwa wakati

Jamaa katoa ushauri ambao wewe utaamua kuufuata au kuachana nao haina haja ya kupanic maana Nina uhakika atakuwa na uzoefu wa hizo sehemu mbili ndo maana kashauri hivyo

Kwa kifupi ata Mimi simshauri MTU tena kuifungia pesa kule DSE bora izalishe kwenye biashara yeyote.lakini siyo DSE ambako huwezi kuipata pesa yako kwa wakati afu usalama wa ela ni mdogo kwa maana bei hazitabiriki na ukitaka kuuza hisa zako zoezi hailifanyiki kwa wakati

Mimi Nina mwezi sasa wana mbwelambwela tu
Asiyesikia la mkuu uvunjika guu
 
UTT kuna risk ndogo zaidi kuliko DSE.

Kwa uzoefu wangu wa UTT (niko mfuko wa Jikimu) faida iko around 9 -11% kwa mwaka. Hivyo ni mahali pa faida zaidi kwa uwekezaji wa muda mrefu wa fedha kuliko benki.

Kulinganisha uwekezaji katika hisa au UTT na biashara za kawaida ni tenge.
Biashara za kawaida huambatana na risk kubwa sana kulinganisha na UTT



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo ni wazi biashara za kawaida zina faida kubwa zaidi ukifanikiwa.

Ila ifahamike kuwa wafanyabiashara wakubwa pia huwekeza sehemu ya fedha zao katika mifuko kama ya UTT kwa sababu ya risk ndogo, japo faida ni kidogo ukilinganisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kwenye mahindi kuna changamoto yake. Wewe unajua kununua na kuweka stooo tuu, aujui kuna wadudu kama panya, hali ya hewa na wengineo wanaweza wakaaribu hayo mazao. Kila kitu Kina changamoto. Tumia elimu kujibu maswala ya kielimu
M sijalazimisha afanye biashara tajwa,nilichofanya ni kuonesha njia tu kwani biashara ziko nyingi.Kwangu Mimi kama Nina milioni 2 ni bora inifie kwenye biashara ambayo ninauhakika wa kupata faida Mara mbili kuliko kuwapelekea watu then wanipangie gawio LA kunipa au kutonipa.

Mwaka Jana nilinunua shamba LA mikorosho kwa 2.5 ml bahati mbaya nilipata majanga ya kuugua hivyo nikashindwa kulihudimia.Nikamuachia jirani yangu kwa makubaliano atakachopata chochote atanipatia,then alivyovuna akaniletea laki 5 pamoja na changamoto lukuki.Sasa were na pesa yako ya kuunga kanunue hisa za Voda uone kama utakuwa huru n pesa yako.N ushauri hivyo si lazima kuukubali.
 
Ok

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
Chinchilla, hivi ninaweza kuwekeza masoko ya nje nikiwa hapa hapa Tz? Kama ni possible procedure zake zipoje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu, nimepata kitu ktk maelekezo yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi faida yake inapatikanaje? Ukicompare na hao DSE?

Sent using Jamii Forums mobile app
Faida inapatikana kutokana na kushuka au kupanda kwa hisa zilizopo kwenye hicho kikapu, so kwa mfano UTT ilipanda kwa kasi sana mwanzoni kwa vile walinunua hisa nyingi za CRDB mwanzoni na CRDB ilipanda sana, ila sasa CRDB imetermeka vikali so nategemea growth ya UTT nayo itapungua unless wamebadilisha idadi ya hisa za CRDB katika kikapu chao.

UTT ni "diversified" zaidi ya kununua hisa moja, so inakuwa sio rahisi kupanda au kushuka kwa kiasi kikubwa kama hisa inavyoweza kwa vile ni mchanganyiko wa assets mbalimbali zikiwemo assets ambazo zina fixed income kama bonds ambazo zao lake linajulikana kwa mwaka.
 
Wasalaam Wakuu wa jukwaa hili!

Nimeingia kwenye mtandao wa UTT UMOJA TRUST ila sijaambulia chochote, maana wetumia technical terms tu.

Napmbeni please mwenye uelewa juu ya mfuko wa Umoja anisaidie kufahamu faida na hasara za mfuko huo.

Nipo mbali na ofisi zao, ndo maana nimetafuta msaada hapa.

Karibuni mnisaidie
---------
Michango ya wadau:

 
Ni Mifuko ya uwekezaji wa pamoja,

Yaaani,

Kwa kuwa watu wengi hawana UTAALAMU wa UWEKEZAJI wala PESA NYINGI za kuwekeza hususani kwenye TREASURY BILLS, GOVT BONDS, HISA nk, hivyo mnakusanya PESA zenu hapo UTT ili ziwe nyingi ( Kulingana na kitu unachotaka ukipate ) then wao UTT wanao WATAALAMU wa masuala ya FEDHA UWEKEZAJI hivyo watatafuta MAHALI pazuri pa kuwekeza hizo PESA Zenu iwe kwenye HISA DSE, BONDS, TREASURY BILLS n.k na likipatikana GAWIO huko walikowekeza ndio na wewe unapewa, wakila HASARA na wewe UNAKULA.

- Nimejaribu kueleza kwa lugha rahisi, naamini umenielewa.
 
SAFI SANA MKUU, LABDA HII MIFUKO INAWEZA IKAWA NI SEHEMU YA KUTUNZIA PESA ZAKO AU, NI KAMA BANK TU
 
SAFI SANA MKUU, LABDA HII MIFUKO INAWEZA IKAWA NI SEHEMU YA KUTUNZIA PESA ZAKO AU, NI KAMA BANK TU
Exactly, ila kupata pesa zako kila utakapokuwa unazihitaji itategemea na aina ya mfuko uliowekeza. UTT siyo kama BANK maana BANK wanakata mno pesa
 
Wakipata hasara na wewe???? Duh ! Ngoja nifuge kuku tu
Hata kwenye kufuga kuku kuna MDONDO. Hakuna biashara isiyo na risk. The higher the risk, the higher the return.

- Tena hao UTT wamekupunguzia risk kwa kuDIVERSIFY pesa zako.
- Kuna watu wanawekeza wenyewe DIRECTLY kwenye HISA, BONDS, n.k na hawaogopi kupoteza
 
Mkuu inao
Mkuu inaonekana we mtaalamu wa masuala haya, ntahitaji msaada zaidi kutoka kwako
 
Suala la hasara kwa mwanchama wa UTT huwa halipo,maana faida kila mwaka hutolewa.wao wana mifuko mingi na uwekezaji wao ni mkubwa na mpana lazima kuna mali watapata faida nso maana nao hiyoa gawio
 
Suala la hasara kwa mwanchama wa UTT huwa halipo,maana faida kila mwaka hutolewa.wao wana mifuko mingi na uwekezaji wao ni mkubwa na mpana lazima kuna mali watapata faida nso maana nao hiyoa gawio
Yes, ni kweli. Niliweka tu hasara ila najua ni ngumu kupata. Ila ikitokea wakapata hasara na wewe utaathirika pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…