Doubleg Malafyale
JF-Expert Member
- Feb 17, 2017
- 2,733
- 3,561
Hata kwenye mahindi kuna changamoto yake. Wewe unajua kununua na kuweka stooo tuu, aujui kuna wadudu kama panya, hali ya hewa na wengineo wanaweza wakaaribu hayo mazao. Kila kitu Kina changamoto. Tumia elimu kujibu maswala ya kielimu
Yeye katoa ushauri kazi kwako kufuata au kuachana nao
DSE ni kama unacheza kamali kwa bahati nzuri mm nipo kote mazao na niliwekeza kasenti kangu uko DSE
Kiufupi hakulipi aisee bei zinabadilika kama upepo,mapungufu mengine ni hawa brokers wa DSE unaweza ona hisa za kampuni ulizonazo zimepanda ukaamua kuuza,zoezi linachukua muda sana mpaka mwezi au zaidi adi ile bei iliyokushawishi uuze hisa zako utakuta imeporomoka
Mfano mzuri tarehe 4 ya mwezi august nilifanya process ya kuuza hisa zangu za kampuni Fulani niliwatumia Solomon brokers,aisee adi Leo wana mbwelambwela mpaka bei iliyonishawishi imeshuka kwa kifupi biashara ya hisa bongo ina discourage sana mkuu.
Kwenye mazao tunapoweka stoo huwa tunaweka dawa mpaka muda unaohitaji wewe kuuza na faida yake unaiona,na unauza kwa wakati ule unaodhani unafaa lakini DSE hill halipo unaweza hitaji kuuza Leo lkn process za brokers zikakusababishia hasara kwa sababu hawafanyi kwa wakati
Jamaa katoa ushauri ambao wewe utaamua kuufuata au kuachana nao haina haja ya kupanic maana Nina uhakika atakuwa na uzoefu wa hizo sehemu mbili ndo maana kashauri hivyo
Kwa kifupi ata Mimi simshauri MTU tena kuifungia pesa kule DSE bora izalishe kwenye biashara yeyote.lakini siyo DSE ambako huwezi kuipata pesa yako kwa wakati afu usalama wa ela ni mdogo kwa maana bei hazitabiriki na ukitaka kuuza hisa zako zoezi hailifanyiki kwa wakati
Mimi Nina mwezi sasa wana mbwelambwela tu
Asiyesikia la mkuu uvunjika guu