Ufahamu wasifu wa Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi

Ufahamu wasifu wa Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi

Umkilo

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2018
Posts
470
Reaction score
419
Uteuzi: Rais Magufuli amteua Dr. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG). Masaju ateuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu

=======

WAKATI Mwanasheria Mkuu wa Serikali mteule, Dk. Adelardus Kilangi, akitarajiwa kuapishwa leo Ikulu, jijini Dar es Salaam, wasifu wake unaonyesha ni mbobezi wa sheria za ngazi ya ndani na kimataifa, huku baadhi ya wadau wakimueleza kama mmoja wa watu makini.

Dk. Kilangi, ambaye anachukua nafasi ya George Masaju, aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahama Kuu, awali alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kituo cha Arusha.

Dk. Kilangi, naibu wake (DAG) atakuwa Paul Ngwembe, baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Gerson Mdemu, uteuzi wake kutenguliwa na kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Kabla ya uteuzi huo, Ngwembe alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance Regulatory Authority – TIRA).

Wasifu wa Dk. Kilangi

Dr. Kilangi alizaliwa Mkoani Geita na kusoma Shule ya Msingi Nyankumbu na Sekondari ya Sengerema (SESESCO) na Seminary za Nyegezi, Kibosho na Kipalapala na kisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia Shahada yakwanza hadi Uzamivu (PhD).

Wasifu wake uliochapwa kwenye mtandao wa Maktaba ya Umoja wa Mataifa (UN) ambao unahusu masuala ya sheria za kimataifa, unamtanabahisha Dk. Kilangi kama mbobezi wa sheria za kimataifa katika nyanja mbalimbali, zikiwamo sheria za madini na mafuta.

Dk. Kilangi, ambaye anatarajiwa kuapishwa leo Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam, katika utendaji wake wa masuala ya sheria amewahi kuwa Mjumbe wa Tume ya Sheria za Kimataifa ya Umoja wa Afrika kati ya mwaka 2009 hadi 2015.

Akiwa mmoja wa wajumbe thabiti wa tume hiyo, aliteuliwa kuwa rais na akaiongoza tume hiyo kuanzia 2012 hadi 2014.

Dk. Kilangi amebobea katika Sheria za kimataifa za madini na katika utumishi wake amewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino hapa nchini.

Pia amewahi kufundisha sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (Iringa), Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini – Dar es Salaam na Chuo Kikuu Huria.

Aidha, amewahi kuwa Meneja wa Mradi wa SAAT-Tanzania (Southern African Aids Trust) na Ofisa wa Mipango wa DANIDA na Mshauri wa Sheria wa Ubalozi wa Denmark hapa nchini.

Pia amewahi kufanya kazi kama Ofisa Mipango wa Mazingira, Haki za Binadamu na Jinsia katika asasi zisizo za kiserikali (NGO) na kuwa Mshauri wa Sheria wa Resource Mobilization Unit ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dk. Kilangi ni Mwanasheria wa Mahakama Kuu ya Tanzania, pia ni mwanachama wa Chama cha Wanasheria cha Afrika Mashariki.

Ameandika vitabu na makala mbalimbali kuhusu sheria, hususan eneo la sheria za ushirikiano wa kikanda, madini na sheria za kimataifa.

Amewahi kutoa ushauri na kufanya utafiti mahususi katika taasisi na mashirika ya maendeleo na maeneo ya mitaala na mipango ya maendeleo ya elimu.

Pia wasifu mfupi uliopo kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Linked in, mbali na uzoefu wake wa kazi, umetanabahisha kwamba, mwaka 2008 hadi 2013 alisoma Shahada ya Uzamivu wa Sheria ya Madini na Mafuta katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pia alipata Shahada yake ya Uzamili, akibobea masomo ya usimamizi wa taasisi za kimataifa, biashara na uwekezaji.
 
MR. ADELARDUS KILANGI Member and President, African Union Commission on International Law Dean of the Faculty of Law, St. Augustine University of Tanzania in Tanzania Adelardus Kilangi serves as member of the African Union Commission on International Law (2009-2015) where he was later elected the President (2012-2014).

He is also a Professor of international law, legal theory, and mining law at St. Augustine University of Tanzania in Tanzania. He previously taught law at Ruaha University College in Tanzania, Tumaini University - Dar es salaam College in Tanzania, and the Open University of Tanzania, also in Tanzania.

Prior to that, he served as Country Programme Manager for the Southern African Aids Trust in Tanzania, and Programme Officer for DANIDA as well as Legal Advisor to the Danish Embassy in Tanzania, respectively. He has also worked as Programme Officer to the Environmental, Human Rights Care and Gender Organization, a local NGO, while prior to that he worked as Legal Advisor with the Resource Mobilization Unit of the University of Dar es salaam in Tanzania.

He is an Advocate of the High Court of Tanzania, a member of the East African Law Society, and member of the Pan African Lawyers Union.

He has published a number of books and articles in law, specifically in the area of regional integration law, mining law, and general international law.

He has carried out a number of consultancies and research works especially in the area of institutional and organizational development, as well as the area of curriculum and academic programme development.
 
Ni mzaliwa na mkazi wa wilaya ya Sengerema mtaa wa Misheni almaarufu Soweto mkoani Mwanza akiwa mtoto wa kwanza katika familia.

Amesoma huko huko Mwanza na baadae alijiunga na masomo ya juu akisomea upadre pale Kipalapala - Tabora lakini hakufikia azma hiyo baada ya kufukuzwa darasa zima kwa kile kilichodaiwa kugoma kuosha sahani za kulia chakula(walikuwa wakimaliza kula utaratibu uliokuwepo walikuwa hawaoshi sahani walizolia na wapishi ndio walifanya kazi hiyo) Askofu akampa maelekezo Baba Gombera awaambie vijana wawe wanaosha sahani zao wenyewe. Baba Gombera(rector) alipowambia wakagoma na hivyo kufukuzwa darasa zima...

Badae alijiunga UDSM akasoma Sheria na amefanya kazi mashirika kibao ya kimataifa kabla hajajiunga na St. Augustine. Ni mtendaji mzuri sana na very charismatic.

Anao ndugu zake na wadogo zake kama Denis Sebugwao (nae mwanasheria) na mwingine ni Padre huko katika jimbo la Geita.

Ameoa na ana watoto
 
Du kwa elimu hiyo inaonyesha ukitaka atunge SHERIA ya mapato ya stendi ya Ubungo kuwa ukilipia kiingilio getini kuingia stendi basi HUDUMA ya choo ndani ya stendi utaipata bure ,SHERIA hii itamshinda
 
Huyu ni Human Rights activict mmoja hivi, haijui vizuri ofisi ya AG na ninamuonea huruma sana kwasababu atapata shida mno kwenye utendaji.

Mkuu anakosea kuwateua watu kushika nyadhifa maeneo ambayo hawana practice nayo. Shida itampata kwenye kujibu maswali bungeni, hakika atapata shida sana, atatakiwa kusoma sana sana la sivyo kitakuwa kichekesho.
 
huyu ni human right activict mmoja hivi, haijui vizuri ofisi ya AG na ninamuonea huruma sana kwasababu atapata shida mno kwenye utendaji. mkuu anakosea kuwateua watu kushika nyadhifa maeneo ambayo hawana practice nayo. shida itampata kwenye kujibu maswali bungeni, hakika atapata shida sana, atatakiwa kusoma sana sana la sivyo kitakuwa kichekesho.

huwezi kuleta mabadiliko kwa kutumia watu waliokalili mifumo iliyofeli. unahitaji mtu anayeweza kuseti dira na kutazama system iliyoko chini yake ina act vipi?

wanaoijua ofisi hiyo wengi wamekwisha ota sugu na mambo ya ovyo wanayaona ya kawaida maana walishayazoea.

ni bora kuleta mtu anayefikiri nje ya mifumo yao waliyojenga ndani ya ofisi.
 
Huyu ni Human Rights activict mmoja hivi, haijui vizuri ofisi ya AG na ninamuonea huruma sana kwasababu atapata shida mno kwenye utendaji.

Mkuu anakosea kuwateua watu kushika nyadhifa maeneo ambayo hawana practice nayo. Shida itampata kwenye kujibu maswali bungeni, hakika atapata shida sana, atatakiwa kusoma sana sana la sivyo kitakuwa kichekesho.
Wacha kukariri mkuu.

Hajaanza hata kufanya kazi ushatabiri atafeli, sema ulitaka apewe nani?
 
Back
Top Bottom