ni mzaliwa na mkazi wa wilaya ya sengerema mtaa wa misheni almaarufu soweto mkoani mwanza akiwa mtoto wa kwanza katika familia..amesoma huko huko mwanza na baadae alijiunga na masomo ya juu akisomea upadre pale kipalapala tabora lakini hakufikia azma hiyo baada ya kufukuzwa darasa zima kwa kile kilichodaiwa kugoma kuosha sahani za kulia chakula( walikuwa wakimaliza kula utaratibu uliokuwepo walikuwa hawaoshi sahan walizolia na wapishi ndio walifanya kazi hiyo) askofu akampa maelekezo baba gombera awaambie vijana wawe wanaosha sahan zao wenyewe..baba gombera(rector) alipowambia wakagoma na hivyo kufukuzwa darasa zima...
badae alijiunga UDSM akasoma sheria na amefanya kazi mashirkka kibao ya kimataifa kabla hajajiunga na St Augustine.ni mtendaji mzuri sana na very charismatic..anao ndugu zake na wadogo zake kama Denis Sebugwao (nae mwanasheria) na mwingine ni padre huko katika jimbo la geita..ameoa na ana watoto