Ufalme wa CHUMA usioshikamana na udongo siku za mwisho, ni ufalme wa aina Gani huu?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Imeandikwa katika siku za mwisho, kutainuka ufalme/ utawala uliofananishwa na CHUMA kilichojaribu kushikamana na udongo, lakini ilishindikana kuchanganyika na kushikamana.

Kwamba, Daniel chapter 2, verse 43: Na kama vile ulivyokiona kile CHUMA kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya " NAFSI" zao Kwa mbegu za WANADAMU, lakini hawatashikamana.

Wajuvi wa mambo haya waje kufafanua, ufalme/ utawala huo ujao, ni ufalme/utawala wa aina Gani?

Karibuni 🙏
 
Soma hapo uliposoma mpaka mwisho utaelewa.....falme zenye nguvu na dhaifu zitajaribu kushikamana lkn haitawezekana...soma historia pia, lkn pia unaweza kusoma kitabu cha Daniel na siku zetu kuna ufafanuzi mujarabu, ukiwa na nia thabiti njoo inbox nikueleweshe vizuri...and I offer u a piece of token, it's a book, read it.
 
Attachments

Utawala wa chuma au chuma kiliwakilisha utawala wa Kirumi katika ile sanamu aliyoiota Mfalme Nebukadreza.
Utawala wake ulipokoma kama ktk verse hiyo ya 43 paliibuka jitihada za kutaka kuunganisha tena tawala ili ziutawale ulimwengu kupitia ndoa, ndipo utaona watawala mfano wa kifalme katika nchi kama france na Uingereza wakijaribu kuwaoza vijana wao ili kupitia ndoa waweze kuunganisha mataifa yao lkn kama maandiko yalivyosema haijawezekana mpk leo, hata umoja waliojaribu kuunda nao tumeshuhudia miaka ya hivi karibuni Uingereza ikijitoa hii inathibitisha usahihi wa kilichoandikwa ktk Maandiko kwamba haitawezekana kuungana

Kinachosubiriwa ni jiwe kuja kuivunja sanamu na kuanzisha utawala wa Kristo
 
" Watashikamana NAFSI zao Kwa mbegu za WANADAMU lakini hawatashikamana"

Umeelewaje hapo?

NAFSI Kwa mbegu za WANADAMU🤔
 
Nje kidogo na karibu kidogo na hii verse. Kuna Utawala utaibuka.. Utawala huo ni wa Kidini na Serikali.
Na hii si Dini nyingine bali Islam.
Hao wanaofananishwa na CHUMA ambao watajaribu kushikamana NAFSI zao na wanadamu,

Ni kina nani hao , kabla ya kushikamana NAFSI zao na wanadamu, walikuwa katika form ipi?

Hii ni Siri kubwa!!
 
Mkuu, usifadhaike, kula nyama yako vizuri na beer yako, huko wala hautafika, hautatoboa, usijipe stress tu zisizo na kichwa wala miguu
 
Biblia imeandikwa kwa mapenzi ya watu ambao walitaka kusikia wanachokipenda, na kuona wanachokipenda.

Kabla ya kuundwa kwa biblia kulikuwako na nakala nyingi za stories mbalimbali ambazo zilielezea maisha ya watu kabla, na baada ya vizazi vilivyopita.

Baada ya kuibuka kwa hizi tawala za vizazi vya kihuni yaani kuanzia 2000 iliyopota mpaka sasa hasa hawa wazungu, walileta uhuni wa kutaka kuutawala ulimwengu mzima, huku TOOL nambari moja ya kutawala ikiwa Dini, pia tool nyingine ni Elimu, sasa katka Dini walitumia imani na mafundisho ya jamii zilizoishi ktk DOLA na Falme Kongwe duniani KutoKa Afrika,

Na stories hizi walizikusanya na kuunda kitabu kimoja ambacho walikiandika na kutunga stories kama wapendavyo wao, huku wakibadiri ramani za matukio, wahusika wa hizo stories bila kusahau majina ya wahusika, mahala pa matukio.

KItendo hiki kitafsiriwe kama uhujumu na ujambazi wa UTU wa mtu kuubadili na kuutumia kwa maslahi ya kishenzi.

Uongozi wa Rumi na baadae hao wakatolic ndio hawa walioleta version za hii biblia ambayo imejawa matukio mengi ya uongo, kuanzia kitabu cha mwanzo mpaka Ufuno ni stories zilizobadilishwa matukio, hivyo basi hakuna hata tukio moja litakalotokea.

Mtasubiri sana, mtangoja sana, hakuna litakalotokea, mjue kuwa si ninyi wa kwanza kujaribu kuelewa hayo matukio yaliyoelezewa na biblia, vizazi na vizazi walijaribu wengine kubashiri matukio ya dunia wakifananisha na biblia lkn hakuna hata moja lililotimia na hakuna litakalotimia,

Wapo wanaomsubiri Yesu kupitia hilo taifa la israel ya uongo hapo middle east, nao wajue wanapoteza muda, yesu hatorudi, mtasubiri sana, mmetega masikio na macho sehemu zisizo sahihi hivyo tegemeeni kusikia makelele tupu.

Ukisoma maandiko Original kabisa ambayo wazungu waliyabadiri na kuunda hizo biblia, yalitabiri mambo ambayo yalitokea na yanaendelea kutokea kama vile👇

👉 Kuwekwa utumwani kwa watu weusi, uzao wa watu weusi kusambaa dunia nzima, kutawaliwa kwa watu weusi kiroho more than 400years(stori waliyoCopy na kuunda story ya waisrael utumwan misri),

👉Ujio wa Mkombozi wa Pili kwa watu weusi atakayerudisha maarifa, elimu na historia ya watu weusi iliyoibwa&kubadirishwa,

👉Kutokea Vuguvugu la waafrika kuanza kuamka na kuzikana imani&dini zilizotumika kuwashikilia, kugawanywa kwa Ardhi ya Afrika kwa watu weupe,

👉Anguko la Falme kubwa zilizowai kuwepo Afrika Kusin, Afrika magharibi, Afrika mashariki, Afrika ya Kati, na Afrika kaskazini,

👉Kuibuka kwa shida za kutengenezwa dhidi ya Afrika kama vile vita, magonjwa, njaa, ukame, mifumo ya siasa,elimu& dini,
👉jaribio la kufuta Rangi nyeusi kupitia mapandikizi ya watu weupe Afrika kaskazini, mashariki, kusini na magharibi ambako kuna uvamizi wa kupandikizwa wa watu weupe uliwekwa makusudi ili usambae afrika nzima na kuleta uzao chotara nje ya Uzao Original mweusi.

👉Kuibuka kwa vita ya mwisho dhidi ya watu weusi na baadhi ya watu weupe watakao ungana na watu weusi(story ambayo dini zenu zinaita vita vya Amagedon, wengine wanaita sijui Gogu na magogu, wengine wanaita vita ya3 ya dunia) uhalisia wake ni kuwa pale Afrika siku ikiukataa huu utumwa na mifumo ya watu weupe, hao white-men watashirikiana kutaka kupambana na bara la Afrika, kwa bahat mbaya haitowezekana.

Na hayo ndio baadhi ya matukio yaliyotabiliwa na maandiko ya mababu wa kale ambayo hao Miungu wenu wazungu na waarabu waliyachakachua na kuunda story zao zao uongo.

Niprove wrong kupitia Ufunuo au utabiri wowote wa Quran/Biblia uliotabiriwa na ukatokea tuone nani muongo.
 
Attachments

  • 1720465232542.jpg
    1720465232542.jpg
    148.5 KB · Views: 9
Salaam, Shalom!!

Imeandikwa katika siku za mwisho, kutainuka ufalme/ utawala uliofananishwa na CHUMA kilichojaribu kushikamana na udongo, lakini ilishindikana kuchanganyika na kushikamana.

Kwamba, Daniel chapter 2, verse 43: Na kama vile ulivyokiona kile CHUMA kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya " NAFSI" zao Kwa mbegu za WANADAMU, lakini hawatashikamana.

Wajuvi wa mambo haya waje kufafanua, ufalme/ utawala huo ujao, ni ufalme/utawala wa aina Gani?

Karibuni 🙏
Tanganyika inasimama kama ufalme wa chuma yaani ufalme wenye Nguvu . Zanzibar inasimama kama ufalme wa udongo yaani ufalme dhaifu .

Watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu lakini hawatashikamana ; maana yake ndoa (muungano ) kati ya Tanganyika na Zanzibar itavunjika .

Umoja unataka kila mmoja kuwa makini kwa upande wake na kuchangia thamani tofauti tofauti kwa nafasi yake. Lakini kuna kila dalili ya wazi kuwa mke (Zanzibar) amesahau masharti ya ndoa na anatenda kinyume na masharti ya ndoa yanavyotaka . Hivyo kuna jiwe litaipiga ndoa hii na kusababisha mume (Tanganyika) kutengana na mke (Zanzibar) wake . Baada ya kutengana , Tanganyika utakuwa ni ufalme wenye nguvu.
 
CCM
 
Utawala wa chuma au chuma kiliwakilisha utawala wa Kirumi katika ile sanamu aliyoiota Mfalme Nebukadreza.
Utawala wake ulipokoma kama ktk verse hiyo ya 43 paliibuka jitihada za kutaka kuunganisha tena tawala ili ziutawale ulimwengu kupitia ndoa, ndipo utaona watawala mfano wa kifalme katika nchi kama france na Uingereza wakijaribu kuwaoza vijana wao ili kupitia ndoa waweze kuunganisha mataifa yao lkn kama maandiko yalivyosema haijawezekana mpk leo, hata umoja waliojaribu kuunda nao tumeshuhudia miaka ya hivi karibuni Uingereza ikijitoa hii inathibitisha usahihi wa kilichoandikwa ktk Maandiko kwamba haitawezekana kuungana

Kinachosubiriwa ni jiwe kuja kuivunja sanamu na kuanzisha utawala wa Kristo
Najua Sio wewe kwa Akili zako ila Roho Mtakatifu kakufunulia ufahamu huu hakika wewe ni 3 Angels message
Lord bless you blood!
 
Tanganyika inasimama kama ufalme wa chuma yaani ufalme wenye Nguvu . Zanzibar inasimama kama ufalme wa udongo yaani ufalme dhaifu .

Watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu hawatashikamana maana yake ndoa (muungano ) kati ya Tanganyika na Zanzibar itavunjika .

Umoja unataka kila mmoja kuwa makini kwa upande wake na kuchangia thamani tofauti tofauti kwa nafasi yake. Lakini kuna kila dalili ya wazi kuwa mke (Zanzibar) amesahau masharti ya ndoa na anatenda kinyume na masharti ya ndoa yanavyotaka . Hivyo kuna jiwe litaipiga ndoa hii na kusababisha mume (Tanganyika) kutengana na mke (Zanzibar) wake . Baada ya kutengana , Tanganyika utakuwa ni ufalme wenye nguvu.
Maneno yanaaumba trust me huu ni Unabii unautoa na maneno yako hayatakarudia bure Maana Bwana ni Mwaminifu kwa kila amtumainiye!
Shalom!
 
Tanganyika inasimama kama ufalme wa chuma yaani ufalme wenye Nguvu . Zanzibar inasimama kama ufalme wa udongo yaani ufalme dhaifu .

Watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu hawatashikamana maana yake ndoa (muungano ) kati ya Tanganyika na Zanzibar itavunjika .

Umoja unataka kila mmoja kuwa makini kwa upande wake na kuchangia thamani tofauti tofauti kwa nafasi yake. Lakini kuna kila dalili ya wazi kuwa mke (Zanzibar) amesahau masharti ya ndoa na anatenda kinyume na masharti ya ndoa yanavyotaka . Hivyo kuna jiwe litaipiga ndoa hii na kusababisha mume (Tanganyika) kutengana na mke (Zanzibar) wake . Baada ya kutengana , Tanganyika utakuwa ni ufalme wenye nguvu.
Mmezoea mizaha sana nyie Vijana....Punguza mizaha itaku cost one day
 
Tanganyika inasimama kama ufalme wa chuma yaani ufalme wenye Nguvu . Zanzibar inasimama kama ufalme wa udongo yaani ufalme dhaifu .

Watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu lakini hawatashikamana ; maana yake ndoa (muungano ) kati ya Tanganyika na Zanzibar itavunjika .

Umoja unataka kila mmoja kuwa makini kwa upande wake na kuchangia thamani tofauti tofauti kwa nafasi yake. Lakini kuna kila dalili ya wazi kuwa mke (Zanzibar) amesahau masharti ya ndoa na anatenda kinyume na masharti ya ndoa yanavyotaka . Hivyo kuna jiwe litaipiga ndoa hii na kusababisha mume (Tanganyika) kutengana na mke (Zanzibar) wake . Baada ya kutengana , Tanganyika utakuwa ni ufalme wenye nguvu.
Kuna UKWELI hapa ingawa umegeuza, Tanga yika ni udongo, Zenz Chuma🤔
 
Back
Top Bottom