Ufanye ushiriki wako kwenye mitandao ya kijamii kuwa salama kwako na kwa wengine

Ufanye ushiriki wako kwenye mitandao ya kijamii kuwa salama kwako na kwa wengine

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Wakuu,

Natumai nyote mpo salama.

Mitandao ya kijamii kwa zama zetu hizi imekuwa mtindo wa maisha na nguzo muhimu ambayo inawasaidia watu kupata taarifa, burudani, elimu, furaha, ajira, marafiki, wapenzi n.k. Mitandao hii imekuwa na nguvu kiasi ambacho imeanza kuzingatiwa kama miongoni mwa hitaji la msingi la binadamu kwa sasa.

Wanaharakati mbalimbali wamejitokeza wakifundisha na kuhimiza matumizi salama ya mitandao hii kwa namna mbalimbali. Mfano, tunahimizwa kulinda akaunti zenye za mitandao ya kijamii kwa nywila (Password) imara na kutoziweka wazi kwa watu wengine Soma: Namna ya kutengeneza Nywila(Password) imara, Fanya haya kulinda Nywila (Password) zako. Harakati zote hizi zimekuwa zinalenga kuhakikisha matumizi ya mitandao ya kijamii yanakuwa salama kwa watu wote.

Mada yangu haitajikita kufundisha namna ya kulinda akaunti zetu za mitandao ya kijamii bali itatazama kwa uchache namna ya matumizi na ushiriki wetu katika mitandao hii.

Kimsingi, nimekuwa nikipita katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Instagram, Telegram, JamiiForums (kwa kutaja michache) nimebaini kuwa wapo watu wengi wanaotumia mitandao hii vibaya kwa kutoa maoni yanayoharibu na kudhalisha utu wa watu wengine pasipokuwa na uhitaji huu jambo linaloharibu amani ya wengine kushiriki katika mitandao hii kwa amani.

Nachotaka kukumbusha kuwa namna ya ushiriki wa watu katika mitandao hii imetofautiana sana. Kuna watu wengine mitandao hii imekuwa ni Maisha yao, imechukua nafasi kubwa katika saikolojia na mioyo yao. Kitu chochote kitakachoandikwa au kutumwa katika mitandao hii kinaathiri Maisha yao kwa namna moja au nyingine. Hivyo unapotoa maoni yako kuhusu jambo fulani iweke kwa namna ambayo haitoathiri utu wake.

Sambamba na hilo, unashauriwa kufikiria vyema kabla ya kufanya jambo lolote ikiwemo kutoa maoni, kutuma picha, video au kutumia maneno fulani ili yasije yakatumika vibaya dhidi yako na yakaathiri shughuli zako. Wapo watu ambao walikosa kazi, walipoteza heshima zao na nafasi zao kutokana na mambo waliyoyatuma kwenye mtandao miaka ya nyuma na wakasahau. Soma: Nguvu ya Mitandao ya Kijamii: Posti za miaka 6 iliyopita zamnyang'anya followers, zamkwamisha kushiriki Miss South Africa 2020 miss Bianca Schoombee.

Hivyo, huu ni ukumbusha na wito kuwa mimi na wewe tuwe makini na chochote tunachotuma au kuchangia katika mitandao ya kijamii ili kufanya ushiriki wetu uwe salama kwetu na kwa watumiaji wengine.

Nawatakia wakati mwema
 
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom