Ufaransa atafunga magoli manne katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia kati yake na Morocco

Execute

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
3,000
Reaction score
7,336
Mwaka 2004 ugiriki walibeba kombe la mataifa ya ulaya wakati haikutarajiwa. Walikuwa wanafunga goli halafu wanarudi nyuma na kupaki basi. Hapakuwa na burudani kwasababu timu moja ndio ilikuwa inacheza peke yake huku nyingine ikizuia.

Morocco naona wameanza vizuri kwa kufuata mfumo kama ule isipokuwa tofauti ni kwamba wanashambuliwa sana na golikipa (Bono) amekuwa akiokoa jahazi. Pia mara kadhaa miamba ya goli imewaokoa.

Hatari katika lango la Morocco itapelekea magoli manne kufungwa katika mechi hiyo. Natarajia nao pia watapata walau goli moja wafute machozi.

Mbappe, Giroud, Griezman, Dembele.
 
Sio kazi ndogo jqpo watu wanajaribu kubeza ushindi wao ambao wamekuwa wakiupata ila wakumbuke sio rahisi

Morroco lazima tuwapongeze kwa hatua ya nusu fainali wanayokwenda kuishia
 
Watu mnaichukulia poa Sana Morocco , wanafungwa manne , wao wamekaa tuu, ufaransa wasipowaheshimu Morocco wanaenda kuchezea kichapo cha mbwa Koko , ni nidhamu Yao dhidi ya hawa waarabu ndo itawaokoa , Kwa mtu aliyeangalia mechi zote za Morocco , atakubali kuwa hakuna timu ya kuitisha Morocco , hata kama ikifungwa labda gap la goli moja tuu , na sio manne kama unavyotaka kutuaminisha
 
Morocco anawachezaji majeruhi 4 kwenye kikosi chake cha kwanza 1 kadi nyekundu moja
 
Mwaka 2004 ugiriki walibeba kombe la mataifa ya ulaya wakati haikutarajiwa. Walikuwa wanafunga goli halafu wanarudi nyuma na kupaki basi. Hapakuwa na burudani kwasababu timu moja ndio ilikuwa inacheza peke yake huku nyingine ikizuia.

Morocco naona wameanza vizuri kwa kufuata mfumo kama ule isipokuwa tofauti ni kwamba wanashambuliwa sana na golikipa (Bono) amekuwa akiokoa jahazi. Pia mara kadhaa miamba ya goli imewaokoa.

Hatari katika lango la Morocco itapelekea magoli manne kufungwa katika mechi hiyo. Natarajia nao pia watapata walau goli moja wafute machozi.

Mbappe, Giroud, Griezman, Dembele.
Wewe una chuki na wa Morocco, keanini usiache tu kazi ya utabiri baada ya kuumbuka kwenye uzi wako wa awali

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
 
Sio kazi ndogo jqpo watu wanajaribu kubeza ushindi wao ambao wamekuwa wakiupata ila wakumbuke sio rahisi

Morroco lazima tuwapongeze kwa hatua ya robo fainali wanayokwenda kuishia
Hata mimi nimewapongeza na kuonesha udhaifu wao.

Hapo ni nusu fainali na sio robo.
 
Watu mnaichukulia poa Sana Morocco , wanafungwa manne , wao wamekaa tuu, ufaransa wasipowaheshimu Morocco wanaenda kuchezea kichapo cha mbwa Koko , ni nidhamu Yao dhidi ya hawa waarabu ndo itawaokoa , Kwa mtu aliyeangalia mechi zote za Morocco , atakubali kuwa hakuna timu ya kuitisha Morocco , hata kama ikifungwa labda gap la goli moja tuu , na sio manne kama unavyotaka kutuaminisha
Timu kubwa zilizoshindwa kuifunga Morocco kwenye Kombe la Dunia hili ni Croatia, Belgium, Spain, Portugal. Si timu ya kubeza tena hii.
 
KIZAZI Cha utabiri.
KIZAZI Cha kamali.
KIZAZI Cha Zinaa.
KIZAZI Cha nyoka.

PUNGUZENI UTABIRI VIJANA MUDA HUWA UNATOA MAJIBU.
WAKATI NI MWALIMU MWEMA SANA
Mimi wala sifanyi betting. Raha ya mpira ndio hii kutaniana na kubeza mpinzani hapa na pale.
 
Wakati hao Morocco wanafungwa magoli 4 watakuwa wamekaa uwanjani, au na wenyewe watakuwa wanacheza kama hao Ufaransa?
Lazima watakuwepo uwanjani wakiona mbappe anapita kwa kasi, griezman na dembele wakipiga pasi za hatari huku giroud akifunga kwa vichwa.
 
Watu mnaichukulia poa Sana Morocco , wanafungwa manne , wao wamekaa tuu, ufaransa wasipowaheshimu Morocco wanaenda kuchezea kichapo cha mbwa Koko , ni nidhamu Yao dhidi ya hawa waarabu ndo itawaokoa , Kwa mtu aliyeangalia mechi zote za Morocco , atakubali kuwa hakuna timu ya kuitisha Morocco , hata kama ikifungwa labda gap la goli moja tuu , na sio manne kama unavyotaka kutuaminisha
Kombe la dunia 2018 watu walisema hivi hivi kuhusu Croatia lakini wakaishia kupigwa tatu mechi ya fainali.

Morocco amepita kwa bahati, waombe hiyo bahati iendelee kuwa upande wao maana kinyume na hapo wataogeshwa.
 
Wewe una chuki na wa Morocco, keanini usiache tu kazi ya utabiri baada ya kuumbuka kwenye uzi wako wa awali

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
Kwanini niwe na chuki? Mbona Brazil na Belgium pia nilisema wataondoshwa na hukuja kusema ni chuki? England pia nilisema ataondolewa na Ufaransa mbona hukusema ni chuki?

Tatizo lako unaingiza hisia za kidini wakati mimi nazungumzia mpira wa kitaalamu.
 
Timu kubwa zilizoshindwa kuifunga Morocco kwenye Kombe la Dunia hili ni Croatia, Belgium, Spain, Portugal. Si timu ya kubeza tena hii.
Upo sahihi, haitabezwa na ufaransa na ndio maana itafungwa 4
 
acha chuki mkuu

Back
Top Bottom