Ufaransa atafunga magoli manne katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia kati yake na Morocco


Nakubaliana na wewe 100! Siyo rahisi kama anavyotaka kutabiri. Team kama Spain, Portugal siyo team rahisi kama mtoa mada alivyoziweka katika daraja ambalo Morocco kawafunga hao kirahisi. Ufaransa inatakiwa iwaheshimu sana Morocco na kwa kweli walistahili. Kwa Afrika nchi zingine kubwa kwenye mpira kama Nigeria, South Africa, Ghana, Egypt, Cameroun, Tunisia, Senegal, Algeria, Congo DR nk zijifunze spirit waliyoionesha Morocco
 

Chuki binafsi tu na wivu unamkumba huyu jamaa. Hata hivyo kaangukia pua
 
Kwa hiyo kipa kuokoa ni bahati?
Unachopaswa kujua hakuna bahati pasipo na uwezo. Bahati ipo ila bila uwezo huwezi kupata hiyo bahati, utapigwa za kutosha. Kipa kuokoa sio bahati ni uwezo. Timu kutengeneza shambulizi dk. Ya 117 na kufunga hakuna tofauti na timu iliyotengenza shambulizi dk.ya 40. Huwezi kusema Morocco wamefuzu semi fainal kwa sababu ya bahati tu, je miaka ya nyuma walikuwa hawafuzu kwa sababu ya kukosa bahati tu? Akina Senegal, Ghana, Tunisia , Cameroon wametolewa sababu ya kukosa bahati?
 
Katika maandishi yangu kila pahala nimeeleza kwamba Morocco ni timu nzuri na inatembea kwenye bahati katika michuano hii.

Brazil na Portugal wote wana timu nzuri lakini hawana bahati kama ilivyokuwa kwa Spain, Uholanzi na Japan.
 
Katika maandishi yangu kila pahala nimeeleza kwamba Morocco ni timu nzuri na inatembea kwenye bahati katika michuano hii.

Brazil na Portugal wote wana timu nzuri lakini hawana bahati kama ilivyokuwa kwa Spain, Uholanzi na Japan.
Timu nzuri maana yake imekamilika kila idara. Kipa kushindwa kuokoa penati maana yake hiyo timu ina upungufu kwenye nyanja hiyo. Wachezaji kupiga hovyo penati maana yake hiyo timu inaupungufu kwenye nyanja hiyo.
 
Morocco mjiandae kulala na viatu. Bado masaa 21 mbungi lipigwe.
 
Morocco hawataki watu wanafiki kama ww mechi ya Spain vs Morocco watu wote walishabikia Spain na hawakuipa nafasi ikaja Portugal vs Morocco kila mtu akasema ndio mwisho wake wakapita mkaanza unafiki wa kuwashabikia wakawakataa na leo tena mmeanza unafiki wote mnaipa nafasi France akishinda Morocco mtaanza tena unafiki wakuishabikia nikwambie tu yale maneno yote ya wachezaji wa MORROCO hayakuwa kwa bahati mbaya na ilikuwa kwasababu ya wanafiki wachache kama nyinyi mnaodhara Africa haiwezi kufanya chochote wanafiki wakubwa.
 
Mimi siwezi kushabikia morocco, wanacheza aina ya mpira nisioupenda. Leo watafungwa na ufaransa magoli manne.
 
full time watatoa draw, mfaransa anaenda kutolewa kwenye penalts
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…