#COVID19 Ufaransa: Raia kuhitaji kibali maalum kwenda migahawani, baa n.k

 
Unaelewa maana ya Zamani??
Sijui wewe unaposema zamani labda una maana nyingine.
Hujui aliyekuwa akizuia chanjo kwa kusema chanjo ni mkakati wa mabeberu wa kuua waafrica??
Nimekwambia tena,hakuna sehemu kuna kiongozi amewahi kuzuia chanjo tz.
Kuhusu vifo hujiulizi why huyo huyo mzuia chanjo aligoma utoaji wa takwimu za kila siku either kwa wagonjwa wapya,waliopona na hata vifo
vifo vyote ni corona??
! Watu wengi tu waliugua na kupona kadhalika na vifo pia tangu May 2020
Kwahiyo wewe takwimu ulizitoa wapi kama alikuwa akizuia,na je kabla ya hapo wwatu walikua hawaugui na kufariki tz??
mzuia chanjo aliwahadaa mtembee kifua mbele huku wimbi la pili likizoa watu wengi January na February 2021.
Mimi ni miongoni mwa tuliotembea,tunatembea kifua mbele,sijafa bado.wewe ulikufa??
Kuhusu vifo vya Covid related nadhani urudi darasani ujue kuwa uwepo wa covid kwa mtu mwenye pre-existing comorbidities ni contributing factor na ndio chanzo kitakachotumia kucertify death ,
unaujua ukimwi???embu hubiri haya kuhusu ukimwi.
mtu kama alikua na DM au HIV leo hii kimbunga covid kikamvaa kwa sababu hakupata chanjo kwa wakati utasema amekufa kwa covid au DM?
Kama covid inaua wenye kinga hafifu,ingawa sina uhakika kama ni kweli,kwanini chanjo inasukumwa kilazima kwa watu wote??
Haihitaji kuwa na PhD kujua tu walikufa watu wengi sababu hakukua na uwazi na kukosekana kwa uwazi ndio tabia hata za CCM kwenye chaguzi !
mshangao wangu ni wewe takwimu za vifo vya corona umetoa wapi,na hazikuwa zikitolewa.
Kataa chanjo zurura hovyo ila covid ikikupata kama aliyesema ni futa tu pengine hutopata wasaa wa kuja hata kutoa ushuhuda..
Corona ipo,na maisha yapo,chagua moja la kushughulika nalo.
 
Hiih! Hivi kwa akili yako timamu kabisa Unafikiri Chanjo hii ni hiyari; Hiyari ya wapi?
Kweli Rais na viongozi wake waandamizi, waliokuwa wakipinga chanjo hii wakati wa utawala wa awamu ya V kwa nguvu zao zote, wamekubali kupokea Chanjo na kuchanja kwanza, halafu wewe mwananchi mwenzangu wa kawaida tu Unakatalia wapi?
Lugha iliyotumika ni ya kiungwana kuwavuta watu; lakini baada ya hapo, sharti kila mtanzania achanjwe. Unafikiri utalazimishwa kwa namna unavyodhani; wapi!
Ukitaka kununua au kuuza, utatakiwa kuonesha cheti kuwa umechanja Uviko-19; ukitaka kuendelea na ajira, sharti uwe umechanjwa; huduma hospitalini, benki, na kadhalika, lazima uwe umechanjwa aidha na Astra Zeneka, J&J, na chanjo yoyote unayoifahamu. Kwa shinikizo hizi na nyingine zinazofanana, utajikuta mwenyewe unahiyari kwenda kuchanja. Kwa hiyari yako mweenyewe!
Madhara yanayoambatana na chanjo hizi yanasemwa mengi. Ni Maombi pekee kwa Bwana Yesu Kristo ndiyo yanaweza kutuponya. Huwezi mwananchi wa kawaida kubishana na mamlaka, yaani Serikali.
Chanjo hii tofauti na zilizotangulia, pamoja na uzuri au ubaya wake, haiyumkiniki, imepokelewa kwa mitazamo hasi na watanzania kwa sababu mbalimbali.
Utakumbuka Serikali ya Awamu ya V ilipinga waziwazi juu ya Chanjo ya Uviko-19. Bahati mbaya au nzuri, Rais wetu wa sasa, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, baadhi ya mawaziri ktk wizara mbalimbali, viongozi wakubwa waandamizi, na kadhalika, walikuwa kitu kimoja na aliyekuwa Rais, marehemu JPM kupinga kabisa kabisa juu ya Chanjo hizi za Uviko-19.
Sasa, kimetokea nini wamefanya U-TURN ghafla? Watanzania lazima wawe na mashaka. Lazima waogope. Tena zipo conspiracy theory kuwa kule kuchanjwa tulikoshuhudia wakati wa uzinduzi wa Chanjo nchini na Rais SSH, ati, ilikuwa maigizo tu. Kiini macho. Watanzania tunajiuliza, iwapo ndivyo, Je, ni jambo gani lililo nyuma ya pazia au chini ya zuria?
Haya, ni Serikali awamu ipi tuiamini juu ya hili; Ni ile ya Awamu ya JPM au SSH?!
Anyway, ndugu jitahidi kujiandaa kisaikolojia, chanjo lazima utachanja tu, japokuwa itakuwa si kwa utashi wako. Utachanjwa kwa hiari hata kwa shinikizo.
 
Nimeongea kitaalam kumbe namuelewesha MATAGA !

Pole sana usichome chanjo , endelea kuamini Corona ni futa na chanjo ni mkakati wa kibeberu kupunguza waafrika kama mlivyolishwa uongo..

Hili litakuwa jibu langu la mwisho kwako

Mie niko nadunda miezi 5 sasa! Subiri kimbunga kikupate ndio utajua nchi imeweka kipaumbele kwenye nini kama V8 zinakua full tank ila hospital kuna muda hadi Paracetamol zinakua out of stock.
 
Wape faida lockdown ilikuwa kwa ajiri ya nini ili aweze kuona mwenyewe ni vp imesaidia.
Lockdown kazi yake kubwa ni kupunguza muingiliano wa watu hasa kuepusha mlipuko mfano mashabiki wa Finland walioenda Euro 2020 walivyorudi walileta mlipuko mkubwa so watu almsot elfu 2 wakasababisha tatizo kwa zaidi ya watu elfu 20000!!!

Sasa imagine hao elfu 2 wasingetoka nje ya Finland na wakabaki kwenye mitaa yao tu ni maisha mangapi yangepona???


However mnaozodoa lockdown ilipaswa msaidie je ni mbinu gani mbadala utaepusha maambukizo ya communicable disease tena kwa hewa bila kuzuia mikusanyiko?? Hvi bila lockdown unadhani wangekufa wangapi kma sio mara 10 ya pale!!
 
Mimi zijazodoa lockdown nimetaka utoe faida zake tu, sasa kwa faida kama hizo ndio nashangaa watu kupinga lockdown kwa nchi za africa.
 
Mimi zijazodoa lockdown nimetaka utoe faida zake tu, sasa kwa faida kama hizo ndio nashangaa watu kupinga lockdown kwa nchi za africa.
Kwa africa sio viable maana teknolojia ipo chini sana so uzalishaji ungeshuka but ulaya wana facility to work from home. Maadam chanjo wamepata so lockdown haina haja tena ssa anaposema lockdown imewashinda tumueleweje?
 
Kwa africa sio viable maana teknolojia ipo chini sana so uzalishaji ungeshuka but ulaya wana facility to work from home. Maadam chanjo wamepata so lockdown haina haja tena ssa anaposema lockdown imewashinda tumueleweje?
Labda ameangalia hali ya maambukizi na vifo kati ya nchi zilizoweka lockdown na ambazo hazijaweka lockdown, hivyo pengine labda ungemuwekea namba kuonesha nchi zilizoweka lockdown imesaidia vp kupunguza vifo hasa kama kwa wazee ambao ndio wahanga wakubwa.

Kwahiyo labda ungetumia namba sasa kumuonesha jinsi lockdown zilivyokuwa na tija badala ya kusema tu kama isingekuwa lockdown hali ingekuwa mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…