Ufaransa yaikopesha Tanzania zaidi ya Tsh. bilioni 500 kwa miradi ya REA na maji Mwanza

Ufaransa yaikopesha Tanzania zaidi ya Tsh. bilioni 500 kwa miradi ya REA na maji Mwanza

Huwezi kujiuliza kwa nni siku hizi tunapata mikopo mingi na wanatoa kwa wakati, tofauti na zamani wanatoa mikopo kisha hawaitoi mpaka kipindi kinaisha?
Pamoja na yote bado anayo haki ya kupongezwa kwa kuzisimamia.

Unajua terms za huo mkopo mpaka useme zinakuja kwa wakati? Ungekuwa unajua vipengele vya huo mkopo wangalau. Hivi huku kanda ya kusini mbona sioni ikipatiwa miradi ya bei kubwa kama huko kanda ya ziwa? Kuna nini kanda ya ziwa sasa hivi?
 
Ufaransa anavyoyanyanyasa Mataifa ya Africa Magharibi, mkopo wake utakuwa na riba kubwa sana.
 
Chanzo RFA habari

Leo Bwana Dotto James kapokea mkopo mpya wa zaidi ya shilingi bilioni 500 toka ufaransa kwa ajili ya miradi ya umeme wa REA na miradi ya maji jijini mwanza.
Mkuu, kwa mkopo huu hawataitwa tena mabeberu bali wafadhili au wadau wa kudumu wa maendeleo kama siyo marafiki wa muda mrefu wenye kulitakia mema taifa letu.
 
U.S yenyewe wanadaiwa.iwe kwa kukopa ama vinginevyo.TZ kama taifa tunasonga mbere kwa mbere.
 
Tunaomba na sisi kata ya Lugulu tukumbukwe kwakupatiwa umeme huo maana kata yote hakuna kijiji hata kimoja chenye umeme ,kuna kijiji cha kanza , vumba, na lugulu Tunakuomba Raisi wetu JPM utukumbuke umefanya mambo makubwa sana hili nijambo dogo sana kwako
 
Yaan manina nchi yetu inapoishi kwa kunustiwa yaan nchi inalasirimali yakutosha lakin tegemez.. sijui wazee wtu akina nyerere walikosea wapi..
 
Ukiwa tajiri lazima ukope, pesa zako unaweka akiba, maana Akiba haiozi.
Cheki ulivyokimbia shule sasa,Interest za Mikopo vs Interest za kwny fixed deposit zipi ni kubwa?
 
Kama Deni hili litakuwa na riba ndogo nitafurahi kulilipa maana linaenda kuleta athari chanya kwa Ndugu zetu wa vijijini
 
Hapo Rea tayari hiyo pesa imetoka ikaenda alafu ikakata Kona kusikojulikana... Hiyo miradi ya maji mwanza haishi... Nilidhania Ni kwaajiri ya Tabora kuunganishwa na maji Safi kutoka ziwa Victoria..
Mwanza hali ya maji bado si stable sana hasa ukitoa Mwanza jiji.
 
Cheki ulivyokimbia shule sasa,Interest za Mikopo vs Interest za kwny fixed deposit zipi ni kubwa?

Serikali huwa hazikopi kutegemea interest ili wapate faida, Serikali huwekeza lakini sio kwenye fixed deposit kama unavyofikiria wewe hizo ni biashara za watu/people ambao hawana uwezo wa kuchapisha pesa. Serikali zinaweka kwenye rasilimali kwa mfano watu/people. Vile vile Serikali huweka kwa mfano dhahabu nk.

(Tanzania wameanza hivi sasa kuweka gold na nafikiri Tanzanite kwa sababu haipo mahali popote duniani, hivyo wakiwa makini wanaweza baadaye kuiuza kwa bei ya juu sana. Vitu adimu huuzwa kwa bei kubwa. (Wakati dunia inakuwa na matatizo bei ya gold inapanda kwa sababu wenye pesa wanakimbilia kuwekeza kwenye ''safe heaven.'')

BTW Kiwango chako cha shule ni kipi mkuu?
 
Unajua terms za huo mkopo mpaka useme zinakuja kwa wakati? Ungekuwa unajua vipengele vya huo mkopo wangalau. Hivi huku kanda ya kusini mbona sioni ikipatiwa miradi ya bei kubwa kama huko kanda ya ziwa? Kuna nini kanda ya ziwa sasa hivi?

Hapa tuanazungumzia mkopo hatuzungumzii hiyo kanda sijui ya kusini, pia ujue huo mkopo haujatoka sasa kusini na kanda ya ziwa vinatoka wapi?

Pia uache mambo ya ukanda, ukitaka ukanda muulize membe pesa za gadafi alipeleka wapi?
 
Back
Top Bottom