Ufaulu wa elimu ya Tanzania unanipa mashaka sana kila kukicha

Ufaulu wa elimu ya Tanzania unanipa mashaka sana kila kukicha

APo wenzako wanafurahia Mtoto wao kufeli ili wamuozeshe wapate mahari ya Ng'ombe au ulidhani wanasherekea nn?
Wanafurahia mtoto amepata alama za walau kwenda chuo!
Wao siwanajua certificate ni D mbili
Sasa hiyo D ya dini itasaidia nini?
Wazazi nao ni vilaza
 
Kuna wazazi hapa nyumbani wamefanya sherehe binti yao kupata dvn 4 ya 33.
Ilibidi niyaangalie hayo matokeo, nikakuta ana D mbili tu ya Kiswahili na Elimu ya kiislamu.
Nikaishia kuwasikitikia..!
Baada ya mwaka watagundua jinsi gani the are so screwed 🤣
 
Hizo private zina siri nyingi mkuu! Usiwe mwepesi wa kuamini hayo matokeo! Ninakijua ninachokisema! Hizo ni biashara na biashara ni matangazo, na matangazo ni gharama! Mtoto analipa milion 8 alafu asipate one???
Licha ya private mkuu, kwa sasa ni kama serikali imeamua kuwafurahisha wazazi kwa kufaulisha watoto wao. Kwa mfano ukiyaangalia kwa umakini haya matokeo daraja ambalo limefauliwa kwa wingi ni division four ambayo inabaki ni jukumu la mzazi kumpambania mwanae na vyuo hivi vya kati. Kwahiyo serikali inatwisha zigo wazazi kwa kiwazawadia watoto wao division four nadhani kuna miaka inakuja hakutakuwa na mwanafunzi anayepata division zero kwasababu akipewa D mbili tu serikali ina hasara gani. Bila Ccm kutoka madarakani taifa hili litachafuliwa sana.
 
Hizo private zina siri nyingi mkuu! Usiwe mwepesi wa kuamini hayo matokeo! Ninakijua ninachokisema! Hizo ni biashara na biashara ni matangazo, na matangazo ni gharama! Mtoto analipa milion 8 alafu asipate one???

Mimi nimesoma shule za Serikali mwanzo mwisho na nilifanya mitihani mara kadhaa ikijumuisha hizo shule za private. TUKIACHA KUPOTOSHA shule za private wapo Serious haswa. Waalimu wa masomo yote wapo na wanasimamiwa kwelikweli na MATOKEO YA KILA DARASA YANAPIMWA Wanafundisha muda wa ziada ikifika mwezi wa 7/8, watoto wamesha maliza syllabus ya mwaka husika wana fanya marudio na maswali.

Pamoja na kwamba sio private zote; nyingine zina unga unga tu....
Ila Ujue matokeo kwao ndio yanawafanya waendelee kuwepo sokoni wakati huku kwingine hata usipokuwa na matokeo utakuwepo tu!
 
Ndugu yangu, (Umeniwahi🙂 Nimekaa leo na mimi nikijiuliza swali hilo hilo kuwa kwani elimu ya Tanzania sasa ikoje (kwa mantiki ya kuwa imerahisishwa kwa kisasi gani.
Nakumbuka miaka ya 80's huko let say shule yenye graduate 200 wa Form 4 unaweza kuta Div 1 may be 13,, Div 2 labda 35, Div 3 may be 50 (and still selected to Form 5), Div 4 - 80 (these are still selected to go to colleges) and may be 20 ( Div 0)

Siku hizi naona Class ya graduate 150 unakuta 75-80 Div 1, halafu Div 2 - 50, Div 3 -25, Div 4 =6-8, Na Div 0 (Nothing🙂

Hii trending imekuwa ikinipa shida sana kuielewa kwamba tatizo ikuwa ni sisi watoto wa siku hizo ama hawa ma GenZ ndio wenye uelewa mpana kushinda sisi🙂?

Lakini pia cha ajabu ni kuwa watoto waofutiwa mitihani trending yao ni kubwa sana na hii ni (indicator) kwamba things are not right somewhere,...It looks like cheating during exams has been very rampantly.

My two cents contribution.
Ningeshauri hii sekta ya elimu isiongozwe na wanasiasa! (Waziri asiwe mbunge, awe mtaalamu wa hiyo sekta, aajiriwe baada ya kufanyiwa usaili !
 
Sasa mbona hawatuwekei hizi habari za shule za masifuri....Wanatu habarisha tu na Ma Div 01 za 07. Zamani si rahisi kuona Div 1 za 07. Tanzania nzima Div 1 za 07 zilikuwa zinahesabika. Siku hizi darasa moja karibia 50% wanapata Div 01 ya 07 (shule moja). Unajiuliza hii ni copy & paste au ni really exam ya Baraza la Mitihani Tanzania?

Zamani Div 3 bado unaweza kwenda Form 5 na kama ni Form 6 inakupeleka Chuo. Na zamani kulikuwa na program ya kupangiwa kufundisha miaka 2 kabla ya kwenda chuo. Hivyo kama umesoma PCM mfano unakwenda kufundisha Math, Physics na Chemistry O level na hata A level wakati mwingine ukisubiria kwenda chuo na Div 3 Form 6. Na unamkuta mtu amekomaa anamwaga 'terial' sio la mchemchezo🙂
Angalia St. Francis au Tabora boys one za 7 au tuseme single digit ni nyingi kuliko one zingine lakini kuna kipindi kwenye top ten unaweza kuta one za 7 hata 6 au 8 lakini kwa sasa dah
 
Kuna wazazi hapa nyumbani wamefanya sherehe binti yao kupata dvn 4 ya 33.
Ilibidi niyaangalie hayo matokeo, nikakuta ana D mbili tu ya Kiswahili na Elimu ya kiislamu.
Nikaishia kuwasikitikia..!
APo wenzako wanafurahia Mtoto wao kufeli ili wamuozeshe wapate Ng'ombe au ulidhani wanasherekea nn?
Wanafurahia mtoto amepata alama za walau kwenda chuo!
Wao siwanajua certificate ni D mbili
Sasa hiyo D ya dini itasaidia nini?
Wazazi nao ni vilaza
Ukute litoto limewadanganya watoto kuwa limefaulu vizuri...Waambie ukweli wazazi hao kuwa mtoto wao hamna kitu kafeli
 
Kuna wazazi hapa nyumbani wamefanya sherehe binti yao kupata dvn 4 ya 33.
Ilibidi niyaangalie hayo matokeo, nikakuta ana D mbili tu ya Kiswahili na Elimu ya kiislamu.
Nikaishia kuwasikitikia..!
Hii ndo shukuru kwa kila jambo
 
Mimi nimesoma shule za Serikali mwanzo mwisho na nilifanya mitihani mara kadhaa ikijumuisha hizo shule za private. TUKIACHA KUPOTOSHA shule za private wapo Serious haswa. Waalimu wa masomo yote wapo na wanasimamiwa kwelikweli na MATOKEO YA KILA DARASA YANAPIMWA/evaluated. Wanafundisha muda wa ziada ikifika mwezi wa 7/8, watoto wamesha maliza syllabus ya mwaka husika wana fanya marudio na maswali.
Ukweli sikumbuki kama kuna hata somo moja la sayansi nililosoma na kumaliza Syllabus kwa ukamilifu miaka yote ya shule?
Mfano; Nikiwa shule ya msingi (shule niliyosoma miaka hiyo) ningemalizaje Syllabus wakati Mwalimu wa hesabu kunatopic hazijui kabisa?
Pamoja na kwamba kuna madhaifu ILA huko private wapo Serious!
Ni kweli unachokiongea ila mimi nimefundisha hizo shule naelewa sio kwamba sijui kinachofanyika huko! Hela ni jibu la kila kitu
 
Yaani mnaona watoto wengi kufeli mitihani ndio kielelezo cha elimu bora… khaaa mnaajabisha…!
 
Maswali mengi huwa yanarudiwa rudiwa miaka na miaka, na hii inapelekea wakufunzi/walimu kuwafundisha namna ya kuyajibu hayo maswali.
Ata huko vyuoni pia, wanafunzi pia wanajikita kwenye kujibu maswali yanayojirudia rudia; ndio maana waki hitimu elimu yao wanashindwa kukabiliana na changamoto za kimazingira, ikiwemo kutengeneza ajira.​
 
Hizo private zina siri nyingi mkuu! Usiwe mwepesi wa kuamini hayo matokeo! Ninakijua ninachokisema! Hizo ni biashara na biashara ni matangazo, na matangazo ni gharama! Mtoto analipa milion 8 alafu asipate one???
Umemaliza kila kitu.
Uzi ufungwe.
 
Hizo private zina siri nyingi mkuu! Usiwe mwepesi wa kuamini hayo matokeo! Ninakijua ninachokisema! Hizo ni biashara na biashara ni matangazo, na matangazo ni gharama! Mtoto analipa milion 8 alafu asipate one???
Kweli kabisa,lkn serikali hailioni hilo?wapi tunaenda sasa,siku hizi imekuwa ni kawaida mtoto kutoajirika pamoja na kuwa na ufaulu mzuri,kumbe practical he have nothing,,hili ndo tatizo la siasa kuingilia utaalamu,,wanachofanya ni sawa na uwanjani gori kupanuliwa ili iwe rahisi kwa mfungaji,,hawatoi maswali fikirishi hii leo.
 
Maswali mengi huwa yanarudiwa rudiwa miaka na miaka, na hii inapelekea wakufunzi/walimu kuwafundisha namna ya kuyajibu hayo maswali.
Ata huko vyuoni pia, wanafunzi pia wanajikita kwenye kujibu maswali yanayojirudia rudia; ndio maana waki hitimu elimu yao wanashindwa kukabiliana na changamoto za kimazingira, ikiwemo kutengeneza ajira.​
That's true
 
Back
Top Bottom