UFISADI: $350 million stolen from Tanzanians in Vodacom scandal


Hapo pia kunanikwaza sanaa pia. Ni akheri mbongo mwenzio apige hyo hela cz itabaki hapa hapa nyumbani. Maendeleo na ajira zitakuwepo hapa hapa nyumbani.
 
Nilitaka kushangaa kama huyu MD wa TIB asingekuwa na skendo za rushwa na ufisadi. Huyu jamaa tena PCCB wamuangalie na ningekuwa nipo pccb ningekuwa nishatupa lupango huyu jamaa na washirika wake hapo TIB.
 
Nchi inaharibiwa na wachache tunashindwa na Burundi walioweza kuandamana. Nchi hii kila kukicha utasikia EPA mara ESCROW sasa Vodacom halafu watu tunaendelea na maisha kama kawa.
Hivi sisi Watanzania tumelogwa na nani???
Hapa kuna watu wa kukamata na kuwekwa ndani uchunguzi uendelee then mahakamani baada ya hapo hukumu.
Ila tukindelea kuleana hivi ndio maana kila mtu anataka madaraka ili alinde alichoiba na aendelee kuiba zaidi.
 
Huyo baba yake Fred LOWASA ndo anataka urais duu uhakika NI urahisi maana madili yake ya ufisadi yatakuwa rahisi
 

tofautisha akili na nguvu mimi naona hawa wanazo nguvu tumewaweka pale juu kwasababu wanazo pesa nyingi sana wana backup kubwa sana, wana controol vyombo vya usalama basi wanaweza kuamua kufanya wanachoweza, wanaweza wakaiba wanavyo weza, huu wizi wa vodacom siyo waakili ukilinganisha na ule wa balali
 
Hapo pia kunanikwaza sanaa pia. Ni akheri mbongo mwenzio apige hyo hela cz itabaki hapa hapa nyumbani. Maendeleo na ajira zitakuwepo hapa hapa nyumbani.

Yap si unajua jamaa ni mabingwa wa kupractice "Spider Web Economy".. Kinachoingia kwenye circle yao huwa hakitoki na kitazunguka humohumo kwenye jumuiya yao.. Heri ya wabongo zitafika mpaka kwa wale wenye hali ngumu na kidogo tutaona unafuu humu mtaani.. U can imagine mabilioni yote hayo yaliyoibiwa ila bado pesa mtaani ni shida. Zinaenda wapi sasa?? Maana serikalini hazipo na huku mtaani pia ni shida tupu
 
Watawala wa nchi hii wakifa ni jambo la kushukuru mungu badala ya kusikitika.
 
UFISADI MKUBWA ZAIDI YA EPA NA TEGETA
ESCROW WA BILIONI 675 KUPITIA VODACOM HUU
HAPA. FRED LOWASA AHUSISHWA $350 MILLION
(675 BILLION SHILLINGS) STOLEN FROM
TANZANIANS IN VODACOM SCANDAL Tycoons
Tanil Somaiya & Rostam Aziz implicated in the
scam • Vodacom Tanzania MD Rene Meza receives
$5 million bribe to keep silent • Tax worth over
121.5 billion/- evaded in the deal • PCCB, TCRA,
TRA caught napping in massive fraud bigger than
EPA and Escrow combined A staggering $350
million (over 675 billion shillings) was stolen from
Tanzanians in a massive scandal involving the sale
of pirated electronic recharge vouchers from
Vodacom Tanzania to customers.
 
Public washing of dirty linens will be order of the day until the general election is over! The state organs are expected to continue slumbering!
 
Rene ni mshenzi.bana
alikuja.na.mikwara.hatari.nakujifanya kubana.mianyaaa.yamamaaaa.
.le mpakawatu wakaondoka
 
Sasa toka 2007 kwann mcseme mnasema leo , hapo anatafutwa Lowasa hatudanganyk kirais babanguuuuuu
 
Hii combination ya rostam na lowassa daah noma sana
Sasa hawa wazee wa madili ndo wapewe nchi haaahaaaaa
Kweli watanzania tutakoma
 
Huu ndiyo unafiki mkubwa sana, siku zote mlikuwapi kuleta hizo taarifa? Mnasubiri uchaguzi ndiyo mlete mambo! Salimu, watu walivyogundua kuwa atapita; walimchafua na tukamkosa kwenye urais sababu hizo hizo za kuchafuliwa.
 
Baada ya kusoma hii habari nashindwa kuelewa ni nani hasa mmiliki wa kampuni hii ya voda.

Hata huyo CEO nae kaajiriwa na nani?

Group inayotajwa hapa ndio wamiliki wa kampuni hii ya voda?

CEO huyu ni mmoja wa wamilliki hao au nae ni mwajiriwa tu?

Kama ni mmoja wa wamiliki,ina maana kawageuka wenzake?

Wenye kampuni wamelala usingizi?

Serikali yetu nayo haijali mapato yaliyopotea kama kodi?

Fikra na sababu za watu kufanya mapinduzi katika mataifa yao zitaendelea kuwepo tu licha ya mapinduzi kupigwa vita duniani kote
 
Hizo pesa ni za voda au ni za umma? Nauliza tuu jmn..

Swali zuri sana. Tatizo watu wanashadadia tu. Hapa sisi kama wananchi ni kukomalua hio 121 bill tax evasion. Hayo mengine sioni yanatuhusu vipi.
 
Tafakari hii habari ukiangalia kwa kina haina ukweli wowote kwa ajili moja kuu, hivi airtime tunazoweka kwenye cimu zetu zikiisha ci mpaka ununnue nyingine na mnara ci unasoma itakuwaje fraud wakati matumizi yako ya cimu yako recorded kwenye system ya voda na mwisho wa mwaka kampuni ya voda inatoa tarifa za makusanyo ya mapato kutokana na kile walichokiuza ,hasara hii yote voda wangeshafunga kampuni siku nyingi ,hapa inabidi tuje na hoja kila miaka mitano kwanini makampuni ya nje yanayofanya biashara tanzania yanabadilisha majina kwa ajili ya kukwepa kodi.kwa mfano tritel to zain to airtel hapo ndio tutajua kodi kiasi gani cha kodi kinakwepwa
 

Tushafika huku mkuu!!!!
 
na vodacom si ingekufilia mbali mazee....tuache kujenga chuki kwa data za kutunga..... na mbona hujatuambia taifa lilipoteza kodi kiasi gani?
 
Hii mambo ungetuandikia kwa kiswahili tungechangia vizuri haya ukiacha kodi kwa ufupi nimeona kaibiwa mkaburu mmiliki wa vodacom siyo watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…