Ufisadi Nchini Tanzania. "Tujishikilie Vizuri Wameanza Tena"

Nimecheka sana. Abiria wote kwenye treni wananishangaa. Hadithi nyingine zinachekesha sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Jamhuri ya JF utapata taabu sana kuielewa, kwanza kitu ambacho inawezekana hawafahamu ni kwamba MATAJIRI WOTE WAPO CCM ama kwa kupenda au kulazimishwa na uhalisia na ulazima wa kutunza mali baada ya kuwa tajiri.

Sioni kwa nini ulalamike lábda uwe umechoka, sisi tupo tayari kula Ndafu kuanzia popote ama kichwani au mkiani.

Kwanza muda mrefu umepita mitaji yetu ilikuwa ikiongezeka kwa taratibu sana. Mungu kashusha baraka, mama huyo karudi nyumbani na mkungu wa ndizi.


Sent from my SM-T285 using JamiiForums mobile app
 
Kwan mwendazake tokea amefariki keshafikisha hata miez mitatu?so unachosema hapo ni kwamba watu walikuwa wanapiga Sana enz za mwendazake kama ni hivyo,sema tuh alikuwa anaminya uhuru wa kuelezea hayo mambo ndiyo maana ulikua huyaskii,we ulikuwa unaskia mapambio tuh yanayomuhusu yeye
 
Ninavyojua mimi ufisadi haujawahi kuisha wala kupungua ila ulizidi kwanzia 2015 mpaka sasa
 
Wakati wa marehemu gharama zilikuwa maradufu, ila watu kwa sababu ya ujinga waliaminishwa kuwa ubadhirifu ulikuwa umedhibitiwa kabisa.

Awaku ya 4 ilisaini makubaliano ya kujenga hosteli za chuo kikuu kwa shilingi bilioni 30. Mwendazake akasema kulikuwa na ufisadi. Akasema ameongea na wataalam, hosteli zitajengwa kwa bilioni 10.

Lakini kilichotokea ni kuwa hosteli zilijengwa kwa bilioni 54; na nyufa kila kona. Kijana aliyepiga picha alinyakuliwa na kusweka ndani. Hicho cha kuwanyima watu habari za kweli na kuwafunga midomo, ndicho kikubwa marehemu alifanikiwa.

Tuendelee kupbana na ubadhirifu maana hakuna awamu iliyoweza kuungamiza, japo tunajua ulishamiri zaidi wakati wa awamu ya 5 kwa sababu ulipaliliwa na Rais. Baadhi ya ubadhirifu alioufanya:

1) Kutumia fedha za umma kujenga uwanja mkubwa wa ndege kijijini, huku kandarasi ya ujenzi akimpa ndugu yake

2) Kutumia pesa ya umma kujenga hospitali ya rufaa ya kanda kijijini kwake, eneo lenye idadi ndogo ya watu kuzidi wilaya zote za mkoa wa Geita, huku mjini Geita, makao makuu ya mkoa wakiwa na hospitali ya kawaida

3) Kununua ndege bila ya kufuata taratibu za manunuzi

4) Kutumia pesa ya umma, kuhamisha baadhi ya wanyama pori toka mbuga ya Serengeti kupeleka mbuga ya Burigi iliyopo kijijini kwake

Na ubadhirifu mwingine mwingi ikiwa ni pamoja na kutumia msururu wa magari zaidi ya 70 wakati wa ziara zake.
 
Ufisadi ulikuwepo toka enzi za Magufuli..hata yeye alipiga Trillion 1.5. Na mpaka leo hatujui alienda kuziweka wapi?
 
Hapa mnajiaibisha bro, ulaji wa mwendazake ndiyo unawekwa wazi!! Hii nyumba kwamba imejengwa ndani ya mwezi mmoja!? Haiwezekani

Kikubwa tukubali kuwa Magufuli keshakwenda, kaingia mwingine ana mitizamo mingine na siasa nyingine!! Msimpe lawama ambazo hastahili, ndiyo maana mambo ya Air Tanzania kaamua ayaanike mapema ili serikali yake ikigoma kuchangia basi likifa msimtupie yeye lawama!! Yaelekea nae anawajua Watanzania vizuri
 
sorry huo ujenzi umeanza kipindi gani?
 
Umejifariji ee!? Endelea kubariki wezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…