Ufisadi uliotamalaki tangia aingie madarakani

Ufisadi uliotamalaki tangia aingie madarakani

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
~ Tozo kandamizi.

~ Ufisadi uliotamalaki tangia aingie madarakani.

~ Maisha kupanda bei, leo hii kula mlo mara mbili ni anasa. Maana maharage tu ni Tsh. 3,000.

~ Kufutia mafisadi makosa huku wasio na urafiki nae wakisota gerezani

~ Ndege za waarabu kushusha makontena hifadhi za taifa.
 

Attachments

  • 20230322_040554.jpg
    20230322_040554.jpg
    127.1 KB · Views: 3
Ila ninachojua ni kuwa Kuna timu Magufuli , wale walionufaika kwa kupora na kutesa kisa kujificha nyuma ya wanyonge.

Kundi lingine ni upinzani wa kina Mbowe, wanapiga jaramba kukamata Dola nao ni wajanja .....wanafanya Kila namna kuwa karibu na ikulu Ili katiba iweze kuandikwa itakayowapa fursa kushika Dola.

Kundi lingine ni chawa wa mama, hawana ubunifu Bali kutoa misifa tu KULINDA matumbo Yao. Kundi lingine ni wapinzani kama kina Zitto ambao karata zao ni ngumu kuelewa. Hawana mvuto kwa wananchi lakini nguvu zao ni mwenyezi Mungu ndiye ajuaye wanazisukuma wapi.

Kundi lililobaki ni kina sisi tunajazwa matumaini na uongo kibaoooo. Tukiweza kujitambua bc tutaweza kuona umuhimu wa katiba siyo eti itawanufaisha kina Mbowe la!Bali sisi ndio tutakua wanufaika.

Kupitia katiba nzuri tutaweza kuchagua viongozi tunaoendana nao na pia kuchukua hatua kuwawajibisha watakapotoka kwenye mistari ya Haki na maadili ya kiuongozi. Wakati ni wetu kudai katiba kwa nguvu zote bila kukoma.
 
February 2021 tembo huku kwetu walikuwa wengi sn na ilikuwa ni kawaida kukutana nao au kuja majumbani, now days kuona tembo imekuwa kazi ngumu kweli kweli.
 
Hatari sana.

Hawa wangekuwa Kenya wangeshaachia ngazi.

Sisi wanatuona mazuzu.
 
Ila ninachojua ni kuwa Kuna timu Magufuli , wale walionufaika kwa kupora na kutesa kisa kujificha nyuma ya wanyonge.
Hili ni kundi ambalo kama ulishawahi kuhakikisha kabisa kuwa lilikuwepo, basi ni kundi ambalo lilikuwa linafanya kazi kinyume na JPM, ili ionekane kuwa ni yeye na Serikali yake.

Chukulia mfano wa TL kumiminiwa risasi nyingi namna hiyo halafu wakati huo huo mtu mwenye mamlaka Bungeni anaamua kukata mshahara wake; huku akimnyina msaada wa matibabu!

Hii nchi tunaishi na baadhi ya watu ambaoo wanafanya mambo utafikiri ni majambazi na kwa nia ya kuichafua mamlaka ya nchi.
 
Wasijaribu kwa Mama. Mama amewekwa na Mungu; hatumchagua sisi!
 
Back
Top Bottom