Ila ninachojua ni kuwa Kuna timu Magufuli , wale walionufaika kwa kupora na kutesa kisa kujificha nyuma ya wanyonge.
Kundi lingine ni upinzani wa kina Mbowe, wanapiga jaramba kukamata Dola nao ni wajanja .....wanafanya Kila namna kuwa karibu na ikulu Ili katiba iweze kuandikwa itakayowapa fursa kushika Dola.
Kundi lingine ni chawa wa mama, hawana ubunifu Bali kutoa misifa tu KULINDA matumbo Yao. Kundi lingine ni wapinzani kama kina Zitto ambao karata zao ni ngumu kuelewa. Hawana mvuto kwa wananchi lakini nguvu zao ni mwenyezi Mungu ndiye ajuaye wanazisukuma wapi.
Kundi lililobaki ni kina sisi tunajazwa matumaini na uongo kibaoooo. Tukiweza kujitambua bc tutaweza kuona umuhimu wa katiba siyo eti itawanufaisha kina Mbowe la!Bali sisi ndio tutakua wanufaika.
Kupitia katiba nzuri tutaweza kuchagua viongozi tunaoendana nao na pia kuchukua hatua kuwawajibisha watakapotoka kwenye mistari ya Haki na maadili ya kiuongozi. Wakati ni wetu kudai katiba kwa nguvu zote bila kukoma.