Ufisadi wa Awamu ya 5: CAG Mstaafu Utouh alia na upigaji wa Trilioni 1.2, aitaka Serikali ieleze pesa zilikokwenda

Ufisadi wa Awamu ya 5: CAG Mstaafu Utouh alia na upigaji wa Trilioni 1.2, aitaka Serikali ieleze pesa zilikokwenda

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Nawasalimu kwa jina la JMT..

CAG Mstaafu Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Taasisi ya Wajibu Tanzania ameitaka Serikali kufanya uchunguzi na kuwatafuta wote waliotafuna pesa kiasi cha Trail.1.23 zilizoibuliwa na Mkaguzi wa ndio mwaka wa Fedha 2019/2020..

Utouh Amesema licha ya pesa hizo kukusanywa lakini hazikupelekwa Mfuko mkuu wa Serikali Hazina na pia kutojulikana matumizi yake..

Ni wakati muafaka sasa Wazalendo wa Chato na Sukuma gang kujitokeza hadharani kueleza kwa nini wameibia Watanzania waliowaaminisha kwamba wao sio majizi?

Huku ni kucheza na maisha ya Watanzania, nyie naambiwa muwe wazalendo wenzenu wanapiga pesa.

===

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wajibu Tanzania ameitaka Serikali kufanya uchunguzi na kuwatafuta wote waliotafuna pesa kiasi cha Trail.1.23 zilizoibuliwa na Mkaguzi wa ndio mwaka wa Fedha 2019/2020..

Vilevile, ameishauri serikali kuwawajibisha maofisa wote waliotajwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusika katika kashfa ya uteketezaji wa noti halali za Sh. bilioni 3.9 kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuchochea uwajibikaji na utawala bora.

Utouh aliyewahi kuwa CAG mwaka 2006 hadi 2014, alitoa rai hiyo jana jijini hapa wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Uwajibikaji ya Mwaka 2020/21 iliyoandaliwa na Taasisi ya WAJIBU kutokana na uchambuzi wa ripoti ya CAG kwa mwaka huo wa fedha.

Alisema Ibara ya 135 ya Katiba inataka fedha zote zinazokusanywa na serikali zipite kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali isipokuwa fedha zilizoamuliwa kwa mujibu wa sheria kupelekwa moja kwa moja kwenye miradi.

Alisema ripoti ya CAG kwa mwaka 2020/21 inaonyesha Sh. trilioni 1.254 zilizokusanywa na serikali, hazikuingizwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

"Hatumaanishi fedha hizi zimeliwa au zimeibwa, lakini hazionekani kwenye mfumo wa serikali. Wizara ya Fedha itafute utaratibu wa kuzipitisha fedha hizo kwenye mfumo unaotakiwa," alishauri Utouh.

Kwa kurejea ripoti yake ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kuu kwa mwaka 2020/21, CAG Charles Kichere, anabainisha namna ulivyo usuluhisho wa fedha zilizokusanywa na fedha zilizowasilishwa Mfuko Mkuu.

Anasema usuluhisho huo unaonyesha kuwa kwa mwaka wa fedha 2020/21, serikali ilikusanya Sh. trilioni 31.326 sawa na asilimia 89.8 ya makadirio yaliyoidhinishwa ya Sh. trilioni 34.879, hivyo makusanyo ya Sh. trilioni 3.553 (asilimia 10.19) hayakukusanywa.

CAG anafafanua zaidi kuwa kati ya makusanyo yote, Sh. trilioni 30.072 zilipokewa Mfuko Mkuu wa Hazina, hivyo kufanya utofauti wa Sh. trilioni 1.254.

BOT, TPA
Nipashe ilipotaka kujua jambo lililomshtua zaidi katika ripoti ya CAG kwa mwaka 2020/21, Utouh alitaja mambo mawili ambayo ni hasara ya mabilioni katika mradi wa uongezaji kina cha Bandari ya Tanga na kashfa ya uteketezaji wa noti zenye thamani ya Sh. bilioni 3.99 uliofanywa na maofisa wa BoT kinyume cha taratibu.

"Kuna vitu vinapaswa kushughulikiwa kwa nguvu kubwa pindi vinaporipotiwa na CAG na wananchi waone hatua zinazochukuliwa. Serikali ichukue hatua dhidi ya watendaji waliotajwa katika mambo haya ya Bandari ya Tanga na uteketezaji wa noti za BoT," alishauri.

NOTI ZA BOT
Kwa kurejea ripoti yake ya kwa mwaka 2020/21, CAG Kichere anasema alibaini tatizo alipokuwa anafuatilia tuhuma za ubadhirifu wa noti chakavu uliofanyika BoT kuanzia Januari 2017 hadi Desemba 2019.

Anasema alifanya ukaguzi maalum BoT baada ya ofisi yake kuombwa na Naibu Gavana (Utawala na Udhibiti wa Ndani) kufanya ukaguzi wa kiuchunguzi.

"Lengo la ukaguzi wangu lilikuwa ni kujua kiasi cha hasara ambacho Benki Kuu ilipata na watu waliohusika katika ubadhirifu huo. Kupitia uchunguzi wangu, nilibaini Benki Kuu ilipata hasara ya Sh. bilioni 3.99 kwenye urejeshaji wa noti chakavu.

“Kulingana na sera na miongozo ya Benki Kuu, noti chakavu ni noti halisi yenye kukosa sifa za kufanya malipo halali. Benki Kuu ina mamlaka ya kupokea na kurejesha thamani ya noti mbovu (chakavu) na kutoa noti mpya," anasema.

CAG anafafanua kuwa katika ukaguzi wake, alibaini BoT ilipokea noti za Sh. bilioni 4.17 ambazo ni noti 417,006 za Sh. 10,000 kati ya Januari 2019 hadi Septemba 2019, ambazo zilidaiwa kuwa ni chakavu ili zibadilishwe na kutolewa noti mpya.

Anasema katika uchunguzi wake, alibaini kuwa noti 1,427 zenye thamani ya Sh. milioni 14.27 zilikuwa safi na zinafaa na hivyo hazikuwa na sifa ya kuwa noti chakavu.Pia alibaini kuwa noti 16,187 zenye thamani ya Sh. milioni 161.87 zilikidhi vigezo vya kurejeshwa BoT na kutolewa noti mpya , wakati noti 399,392 zilizobaki zenye thamani ya Sh. bilioni 3.99 hazikuwa na vigezo vya kupewa noti mpya na zilipewa noti mpya kwa njia ya udanganyifu uliofanywa na maofisa wawili na watunza fedha wanne wa BoT.

BANDARI YA TANGA
Kuhusu kilichomshtua Utouh kwenye Bandari ya Tanga, CAG Kichere anasema alibaini mkandarasi aliyepewa kazi ya kuongeza kina cha bandari hiyo na Mamlaka ya Bandari (TPA), alimpa kazi hiyo mkandarasi mwingine bila kutoa taarifa kwa mamlaka.

Vilevile, CAG alibaini kufanyika malipo zaidi ya gharama halisi za mradi huo kwa Sh. bilioni 64.3, akipendekeza serikali ichukue hatua stahiki dhidi ya wahusika.CAG Kichere anafafanua kuwa TPA iliingia mkataba na mkandarasi mkuu wa Sh. bilioni 172.36 Agosti 3, 2019 wa muda wa mwaka mmoja hadi kufikia mwezi Agosti 2020 kwa ajili ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika Bandari ya Tanga.

Anabainisha kuwa mkataba huo pia ulijumuisha kufanya tathmini ya athari za kimazingira na kununua vifaa kwa ajili ya shughuli za bandari.CAG anasema kuwa kulingana na mkataba, gharama ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika Bandari ya Tanga ilikuwa ni Sh. bilioni 104.92 (asilimia 60 ya bei yote ya mkataba).

Hata hivyo, CAG anabainisha kuwa mnamo Agosti Mosi 2019, mkandarasi mkuu iliingia makubaliano na mkandarasi mbia kwa ajili ya kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli kwa bei ya mkataba dola za Marekani milioni 18.15, sawa na Sh. bilioni 40.46 kwa kipindi cha miezi 11 bila kutoa taarifa kwa TPA.

Katika uzinduzi wa Ripoti ya Uwajibikaji jana, Mweyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Daniel Sillo, alitoa rai kwa WAJIBU kushiriki kutoa maoni katika marekebisho ya sheria mbalimbali ikiwamo ya ununuzi na maboresho ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Japhet Hasunga, alishauri kupunguzwe muda wa taasisi kuwasilisha taarifa ya fedha kutoka miezi mitatu ya sasa hadi mwezi mmoja, pia CAG apunguze muda wa kuandaa ripoti kutoka miezi sita ya sasa, ili mjadala ufanyike kwa wakati.

Hafla ya uzinduzi huo ilihudhuriwa na viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali zikiwamo TAKUKURU, HakiElimu, Sikika, TRA, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, TMF, NAOT, TGNP, FCS, Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Msajili wa Hazina.
 
Katiba Mpya kama SHERIA mama itazuia TARATIBU MBOVU za uchotwaji Fedha Benki kuu KWA matumizi Binafsi kama inavotokea KILA awamu ya utawala NCHI HII!!

Rais atapunguziwa madaraka na hatokuwa na maamuzi Binafsi KUHUSU Taasisi za Fedha na kuteua Ndugu zake au WATU wa karibu yake Ili kuzitawala Fedha za umma kama ilivyo Sasa na AWAMU NYINGI zilizo pita!!


""Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!!!!
 
Unamwambia nani achunguze wakati hao hulindana?

Ile kamati iliyoundwa na Samia kuchunguza upotevu wa fedha uliotokea banki kuu wakati wa msiba wa Magufuli, mpaka leo hakuna majibu yaliyotolewa.
 
'
20220604_164240.jpg
 
Aliyekuwa makamu wa rais ,waziri mkuu na waziri wa fedha wa awamu ya 5 wakamatwe watueleze watanzania
 
Katiba Mpya kama SHERIA mama itazuia TARATIBU MBOVU za uchotwaji Fedha Benki kuu KWA matumizi Binafsi kama inavotokea KILA awamu ya utawala NCHI HII!!

Rais atapunguziwa madaraka na hatokuwa na maamuzi Binafsi KUHUSU Taasisi za Fedha na kuteua Ndugu zake au WATU wa karibu yake Ili kuzitawala Fedha za umma kama ilivyo Sasa na AWAMU NYINGI zilizo pita!!


""Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA""!!!!
Habari ndiyo Hiyo !! Matatizo makubwa yanaletwa na katiba mbovu maana mihimili yote inakuwa chini ya mhimili mmoja uliojichimbia chini Kweli Kweli !!
 
Unamwambia nani achunguze wakati hao hulindana?

Ile kamati iliyoundwa na Samia kuchunguza upotevu wa fedha uliotokea banki kuu wakati wa msiba wa Magufuli, mpaka leo hakuna majibu yaliyotolewa.
SSH na Serikali yake.
 
Aliyekuwa makamu wa rais ,waziri mkuu na waziri wa fedha wa awamu ya 5 wakamatwe watueleze watanzania
Kwani wao ndio walikuwa watoa maamuzi na kuidhinisha pesa?

Hivi Sukuma gang huwa mnatoa wapi ujasiri wa kuwasema watangulizi ikiwa mliiba pesa kwa kiwango hiki?

Uzuri hii ni jinai itakuja tuu kuibuliwa siku moja maana hata Escrow and the likes zilijulikana licha ya kufanywa awamu zilizopita.
 
Hivi hawezi kutaja kwamba hii ilichukuliwa na Fulani na hii ilichukuliwa na huyu?

Nae ametuacha njia panda tu?

Au marehemu amezikwa nazo?
Nani ataje? Unaelewa maana ya kuitisha uchunguzi? Hapo ndio utabaini waliogawana kama zike za Vijisenti vya kina chenge nk.
 
Hiyo miradi mikubwa aliyoanzisha JPM pesa ilitoka wapi? Maendeleo yameonekana hakuna haja ya kuuliza pesa iko wapi? Mtu mwenye maono akiamua kuleta maendeleo anachukuwa pesa yoyote ya karibu. Akiwashirikisha anaona anapoteza mda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Itafika tuu kipindi mtajibia ,wewe jifanye hamnazo,uzuri hiyo ni jinai ngoja Katiba mpya ije.
 
Kama zilipigwa na bado tukaona miundombinu na nchi ikaingia uchumi wa kati ni bora zaidi kuliko sasa ambapo tuko na siasa za royo tua na kugawa mitungi ya gesi
Ndio nasema wewe jifanye hamnazo jinai haiozi itafika kipindi mtaeleza zilikokwenda ngoja Katiba mpya ije.
 
Back
Top Bottom