Ufisadi wa Awamu ya 5: CAG Mstaafu Utouh alia na upigaji wa Trilioni 1.2, aitaka Serikali ieleze pesa zilikokwenda

Hivyo mahakama inaendeshwa na malaika, au ina capability za kimamlaka, lazima chombo kimoja kiwe baba wa yote, hata IWEJE.
 

Anapoteza muda kufuata sheria? Kwani hizo fedha zilikuwa za mshahara wake?
 
Katiba ikiwa bora hata huyo anayewachekea watu atawajibishwa yeye !! Maana kwa mapungufu yaliyopo kwa sasa kwenye hii katiba watu huwa wanafikia kusema nani wa kumfunga paka kengele ? Hapo ujue mapungufu yaliyopo ni makubwa sana !! Hata Mwalimu Nyerere aliliona hili na akatahadharisha !!
 

Iwapo katiba mpya itapatikana kwa kukaa mezani bila machafuko, huku chama kinachobaka chaguzi kikiwa bado madarakani na kusimamia mchakato wa katiba, sioni katiba mpya ikitekelezwa kama inavyotakiwa. Na hapa ndipo ilipo jeuri ya wale wanaosema kwani katiba mpya lazima waifuate? Bila machafuko, ama nchi kupinduliwa na kuanza mifumo upya, sioni hiyo katiba mpya ikitekelezwa ipaswavyo.
 
Awamu ya Ngosha kulikuwa na upigaji sana... Sema watu walikuwa wanaogopa kusema ili jemedari aonekane kadhibiti wizi...
Kwani Uzi umesema yeye ndo alichukia pesa au ni maafisa? Ina maana ubadhirifu unaofanyika sasa unauhusisha moja kwa moja na waliopo sasa?
 
Huyu ndiyo mbovu kuliko wote, kama alijua hivyo kwanini alishindwa kutengeneza katiba bora?

Nyerere hakuwa muumini wa demokrasia, na yeye ndio muasisi wa hii mifumo mibovu ya kiutawala. Yeye ndio alisimamia katiba hii ya rais Mungu mtu ambayo ndio msingi wa matatizo yote hadi leo. Bila machafuko, au nchi kupinduliwa, sioni kansa ya katiba hii mbovu kuondoka hata ikija katiba mpya.
 
Aliyefanya haya yote ni Jiwe, acheni kuzunguka mbuyu kama vile hamjui kuwa jamaa alikuwa Wuzi
 
Kwani Uzi umesema yeye ndo alichukia pesa au ni maafisa? Ina maana ubadhirifu unaofanyika sasa unauhusisha moja kwa moja na waliopo sasa?

Rais ndio msimamizi mkuu wa fedha za nchi hii. Matumizi mabovu au mazuri ni kutokana na maagizo yake kwa taasisi za kimamlaka za usimamizi wa fedha hizo. Hakuna uwezekano wa pesa za umma zipotee bila maelezo huku rais akiwa hajui kinachoendelea nyuma ya pazia. Kama inawezekana kupotea fedha nyingi hivyo sawa na bajeti nzima ya Zanzibar na rais asijue, sasa yuko madarakani kufanya nini?
 
Aliyefanya haya yote ni Jiwe, acheni kuzunguka mbuyu kama vile hamjui kuwa jamaa alikuwa Wuzi

Hilo liko wazi kuwa jiwe ndiye alipiga fedha zile, na hii ndio sababu ya CAG Assad kufanyiwa zengwe baada ya kuweka mambo haya wazi.
 
Majizi ya Tanzania yanaiba huku yanatisha watanzania wasiseme! Mwendakuzimu aungue awe majivu ikiwezekana waliohusika katika hujuma hii wapatikane tupate angalau fursa ya kuwaadhibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…