Ally Kombo
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 11,429
- 2,650
Kwahiyo huyo Ibrahimu wenu hii imani aliimaliza au hakuimaliza?
Na kama hakuimaliza ni nini lilikuwa jukumu lake?
Kwa mujibu wa maelezo yako haya Mussa huyu alikabiliana na wachawi ni kwanini nyie hamkabiliani na hawa wachawi wa sasa?
Kwanini alifufua na kuponya wagonjwa?
Kwanini unadanganya umma?
Mohammad alifumbua kitu gani kuhusu uumbaji wa dunia?
Mussa alishalizungumza hili kwenye Biblia zaidi ya miaka 3000 kabla ya Mohammad wewe unakuja kusema alifumbua fumbo la uumbaji?Hebu acha masikhara kijana
"Sisi" ni akina nani hao?
Halafu hii ni kauli ya nani?
Kuhusu Ibrahim As, Musa As na Yesu As: kazi yao walimaliza.
'Na hakika tulikwisha watuma 'Mitume' kwa kaumu zao (watu wao !) na wakawajia kwa hoja zilizo wazi. Tukawaadhibu wale waliofanya ukosefu (waliokataa na wakaendekeza maovu). Na ilikuwa haki juu yetu kuwanausuru Waumini (wale waliokubali na kufuata dini ya haki)
Qur'an: 30:47.
Kukabiliana na wachawi (Musa As) kufufua wafu na kutibu wagonjwa, hizi ni karama walipewa manabii ili kwadhihirishia watu wao (kaumu) kuwa wao ni Mitume !
kwa sasa elimu ya utabibu ni ya hali ya juu, hata magonjwa yasiyotibika, basi ufafanuzi unaweza kuupata ni kwa nini. Nchi za wajinga pekee ndizo zinazo hangaika na wachawi, na yeyote anayehangaika na wachawi yuko katika karne ya Musa.
Hizi ndizo hoja alizokuja nazo Muhammad SAW, ambazo ziko hai hata sasa !
'Na Yeye (Mwenyezi Mungu) ndiye aliyeumba usiku na mchana, na jua na mwezi vyote katika anga vinaogelea.
Qur'an:21:33.
'Tukaweka katika ardhi milima iliyothibiti ili isiwayumbishe.............
Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyohifadhiwa.........
Qur'an:21:31-32.
'Naye (Mwenyezi Mungu) ndiye aliye fanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya anayetaka kukumbuka, au kwa anaye taka kushukuru.
Na waja wa Arrahmann Mwingi wa Rehema (watu wa Mwenyezi Mungu) ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha (unyenyekevu) na wajinga wakiwasemeza (wao) hujibu: Salama !