Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Huwa sipendi kuzungumzia mambo ya imani hasa yanayozungumzia habari ya Yesu Kristo. Lakini kwa hili la kufufua watu imenitia mashaka, kuna watu wengi misukule walijitokeza kwenye mkutano wa Gwajima, baadhi wanasema walikufa miaka 15/20 iliyopita, moja akasema ametoka mortuary alikuwa amekufa wiki mbili zilizopita. Kilichonifanya niwe na mashaka ni jinsi waliofufuliwa hawajulikani kwa mtu yeyote. Nilidhani mtu aliyefufuka angesema yeye ni fulani, alikuwa anafanya kazi sehemu fulani, na ndugu zake ni fulani na fulani, ama balozi wake ni fulani na alikuwa anasali kanisa fulani au msikiti fulani. Bahati mbaya hakuna hata moja aliyejitokeza akajitambulisha.

Mimi nadhani Gwajima alikuja na misukule yake kuwadanganya watu. Kama kweli amefufua watu hebu tujiulize hao watu wako wapi kama siyo amewachukua?

Mungu atupatie maarifa na hekima ya kutambua

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mkuu nakubaliana na wewe lakini nasisitiza kwamba Kwa Mungu hakuna lisilo wezekana ila hili linalofanyika lazima serikali iwajibike kwa sababu hata wakati wa YESU haya yalifanyika lakini kwa utaratibu tofauti;
1. Yesu alipomfufua Lazaro watu wote walimwona na ndugu zake wali mwona na alikwenda kufanya ufufuo kwenye Kaburi la Lazaro hakukuwa na Hardakadabra.\
2.Yesu alipomfufua yule Bintio alimfufua na kumkabidhi kwa Bwana wake na kuwaagiza wampe chakula.
3.Yesu alipo Muonea huruma mama mjane aliye kuwa akilia baada ya akijana wake wa pekee kufariki aligusa lile Jeneza
na Kijana akaamka aka mkabidhi kwa mama yake.

Hii inaondosha dhana ya utapeli hili la kila siku kufufua Misikule ....kwanza Misukule ninini? ni utapeli na kucheza na akili zawatu.
 
Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha.. Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa.. Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma, Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa! Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa.. hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!! Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..
Kuna mchungaji huko Kenya hivi sasa yuko mahakamani kwa ajili ya haya na kibaya zaidi ni mwanamke jana dereva wake alikuwa anatoa ushahidi jinsi wanavyodanganya kwa kuwaleta watu kanisani kuja kushuhudia uongo na kulipwa hela inabidi na hapa TZ tuwaangalie vizuri hawa wachungaji wetu naamini kuna ka mchezo mchafu kanatendeka hapa.
 
tuwache kuingiza neno la mungu
kwenye ushabiki usiokuwa na mpango Mungi@kama unakataa kitu kataa kwa neno mimi neno la mungu linaniambia nikimwamini nitafanya zile kazi yesu alikuwa anazifanya tena na kubwa zaidi ya hapo sioni koza kunyanganya mchawi mtu na kuleta kwa yesu
kwani watu wanaopinga tu kwa akilizao ndio mwisho wa akili zao

Watu waliofufuliwa na Yesu wanajulikana kwanini wa Gwajima hawajuilkani?
 
Mimi ni Mkatoliki lakini ninayeamini YESU aliyesema kwa imani hata milima itang'oka sembuse haya?
Pondeni wachungaji lakini acheni kulimit uwezo wa Mungu.
Mleta mada ungesema huamini kama wale misukule kweli nisingeshangaa lakini futa kauli ya kutoamini miujiza kwavile huoni kanisani kwako.Mimi kwenye mikutano ya Karistimatic nimeshuhudia miujiza mizito hivyo sishangai uwezo wa Mungu.

hakuna anayebisha kweli uwezo wa Mungu ni mkubwa lakini hawa watu jinsi wanavofufua misukule naona kama wanacheza na mind za watu tyu hakuna lolote,kwa upande wangu nina wasiwasi siamini kirahisi hivo.
 
hivi wanaofufuliwa ni lazima wawe misukule? Mbona hawaendi motuary kufufua walo kufa
 
Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha..
Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa..

Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma,
Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa!

Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa..
hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!!

Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..
Majibu ya SAA YA UFUFUO NA UZIMA

-
- Ndugu wana JF
- Nawasalimu kwa lugha, kabila na mitindo yenu pia

- Ikumbukwa mnamo Jumatatu ya October 14[SUP]th[/SUP], mwaka huu kama siku 27 zilizo pita, -saa kumi na dk 25, Kupitia jukwaa hili hili ndugu yetu mpendwa kiwatengu -alituletea maada hapa inayosema Ufufuaji wa Misukule!! Inatofauti gani na Maigizo?.-

- Maada yake hii ilionekana kupenya miongoni mwa wanajamvi wengi, kiasi cha watazamaji 4,444 na zaidi ya wachangiaji 221, waliojaza zaidi ya kurasa 12 za jamvi hili. Nawapongeza Moderators kwa kuruhusu uwazi huu wa taarifa ndani ya Jukwaa hili Nguli la kifikra na ni imani yangu kwamba basi Mtatoa Muda mwingine huu kwa ajili ya Saa ya Ufufuo na Uzima kufafanua baadhi ya hoja lakini pia kujibu maswali mbalimbali kwa sababu Saa ya Ufufuo na Uzima Tupo na hata siku moja hatujawahi kuwa na kigugumizi kumjibu kila mtu mwenye wazo, dukuduku au swali juu ha huduma yetu.maana-

- 1Petro 3: 15 -Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.

- Kwa neno hilo basi Saa ya Ufufuo na Uzima tukaona hapana shaka ni vema basi tukatafuta muda muafaka ingawa kidogo tuweze kuelezea na kujibu kila anaye taka kuuliza Juu ya Tumaini la Imani yetu wa dini, kabila na dhehebu lolote. Ingwawa Muda wetu ni Kiduchu mno, Tumekuwa na Mikutano mikubwa yenye ishara kubwa za miujiza iliyoanzia Mjini Arusha tarehe septemba 27 hadi Octoba 10 kwenye viwanja vya wazi vya Relini, UNGA LIMITED. Nikupe picha ZA -mkutano wetu wa Arusha,-

- -View attachment 120505 View attachment 120506

- Ambapo watu wengi walifunguliwa, Misukule kurudishwa na Uponyaji mkubwa wa magonjwa kiasi wakazi wengi wa Arusha hawakupenda huduma hii iondoke Mkoani mwao Mtu mmoja mjini hapo mwenye ekari zaidi ya nane akatoa eneo lake bure ili Huduma hii iendelee jijini Arusha maeneo ya Engosheraton, Sokini 1, Unga limited ambapo mpaka sasa huduma inaendelea hapo.-
- Opereshini ya Saa ya Ufufuo na Uzimaikaendelea mjini Moshi kwenye Viwanja vya wazi vya Mashujaa, October 20-27 Moshi nikupe pia picha mbili za mkutano wa Moshi..
View attachment 120508 View attachment 120511


--
- ..
- ‘
- Maajabu yalizidi mno hapo Moshi, maelefu ya watu waliyashuhudia maajabu hayo lakini lililotia fora ni kurudishwa kwa misukule ambao waliwekwa strategy kwa ajili ya Kukamua ng’ombe wakati wa kurudi machungani au asubuhi, misukule hao wanasema wao kazi yao ilikuwa wakati masaa ya jioni ng’ombe wanakaribia kukamuliwa wao bila kuonekana na binaadam wa kawaida huenda kuiba maziwa kwa kuwakamua ng’ombe hao. Na mwenye maziwa akija kukamua ng’ombe anaambulia patupu iwe jioni au asubuhi na kuwalaumu watunza ng’ombe labda wameruhusu ndama akanyonya kumbe misukule weshaiba. Sio lengo langu kuongelea shuhuda tele za misukule hao lakini mkutano ulifurika mno kiasi Yule Mangi mashuhuri wa Kilimanjaro, aliyegombea Kiti cha urais Kipindi kile na mwalimu Nyerere nadhani tunaakiba ya Historia hiyo akajitolea Jengo kubwa sana ambalo hapo awali lilikuwa Godown kubwa mno maeneo ya Pasua, Moshi Mjini karibu na machinjio kuu ya Mji, -ambapo umati wa watu ulimiminika baada ya tarehe za mkutano kuisha hapo uwanjani na kuelekea Ndani ya jengo hilo ambapo -Huduma inaendelea hapo hadi sasa.-

--
- Hatujaishia hapo, sasa Saa ya Ufufuo na Uzima Tunaikabili Tanga kuanzia tarehe 24[SUP]th[/SUP] mwezi huu wa 11, tutakuwa Tanga Viwanja vya Tangamano hapo mjini. Tanga sio mbali kila mwenye dukuduku na maswali tafadhali aje ajionee mwenyewe. Aione misukule na ikiwezekana aihoji apendavyo. Ikumbukwe tanga ni mojawapo ya miji mkongwe kuliko yote katika Historia ya nchi yetu ukiacha Zanzibar, Tanga iliundwa mji tokea 1891, Ikumbukwe jina Tanganyika limetokana na kata Moja Iliyoko mji wa Tanga inayoitwa Tanganyika, Tulipaki msafara na kupiga -picha Eneo hilo tafadhali niionyeshe..
View attachment 120513

--
- Hivyo kwenye historia ya nchi hii -Tanga ina uzito mKubwa lakini Uchawi na ushirikina huupoteza -mji kwenye mstari wa mafanikio. Tembea yetu Tanga tumeona watoto wadogo machizi wengi tukiuliza sababu wakaazi wanasema wazazi wao wamewafanya hivyo. Lakini tunaiombea Tanga na tunaamini Kuanzia tarehe 24 mkutano utapoanza Tanga watu hawa watafunguliwa na naomba stay tuned kusikia kile Mungu atachofanya ndani ya Mji huu. Jambo hili ni chanda cha Mungu ni la wazi na kila mtu aweke bidii kulijua.-

--
- Ahsante kwa kunivumilia kusoma Mukhtasari wa Shughuli za Saa ya Ufufuo na Uzima si lengo langu hasa ila ningependa kukushirikisha na nashukuru sana kwa Muda wako kuwa nami hadi sasa . Wewe ni wa thamani Kuu. Labda sasa nieleze hasa kile kiini cha Hoja ambacho kilikuwa lengo la Sred.. Misukule.. -why misukule..-

--
- Kimsingi Misukule Kila mtu anajua ni nini, ama kwa tafsiri ngeni au mpya sote tunajua msukule ni nini atayesema hajui msukule ni nini huyu atakuwa ni mbishi na sidhani kama tuna nafasi na wabishi. Lakini kwa tafsiri nyepesi msukule ni Roho zinazotangatanga, zinazoishi nje ya miili au ndani ya miili mingine. Mwanadamu ni nini, mwanadamu ni Roho inayokaa ndani ya nyumba na nyumba inaitwa Mwili. Mwanadamu anaweza kuwa ndani ya mwili au nje ya mwili embu ona kweli hii kwenye biblia-
--
- 1thesalonike5:23 -Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
- -
- Tunaelewa kwamba mwanadamu ana mwili, nafsi na roho..lakini Roho ndio itiayo uzima mwili haufai kitu. Basi kifo ni nini, Kifo ni Utengano kati ya Roho na mwili. Roho inaondoka mtu akifa inaenda pahala na the body decay. Nadhani kweli hii wote tunaifaham. Niseme wazi tu kwamba watu wote kufa tutakufa, penda usipende na kufa kwetu ni faida na Kuishi ni Kristo. Lakini kuna neno jingine la Mungu embu litafakari kutoka Kwenye Kitabu cha ufunuo uone jambo hili la ajabu kabisa..
Ufunuo 18:

11 -Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;-
-12 -bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito -chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, -na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha -pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha -chuma, na cha marimari;-
-13 -na mdalasini, na iliki, na uvumba, -na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, -na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho -za wanadamu.



--
- Tunagundua kumbe kuna biashara wajanja huwa wanafanya kimashetani, na moja ya bidhaa hizo ni Miili na Roho zetu wanadamu. Kumbe na Roho za wanadam is among commodities deals within those people thought themselves clever. Kumbe kuna watu wameibiwa Roho, wameibiwa miili Biblia inasema. Ndio maana basi ukaja ufunuo kwenye Isaya 42:22 -Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na -kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; -wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana -asemaye, Rudisha.

--

- Kwa maana kama hiyo basi saa ya Ufufuo na Uzima, na kila mwenye Moyo huu tunaungana kwa kazi hii ya Kuwarudisha haoo walioibiwa. Baadhi ya wachungaji wa Moshi na Arusha nao wameanza kurudisha misukule na shuhuda ni Nyingi sana.-

--
- Basicall Misukule iko ya aina nyingi lakini leo niongelee tatu tu wa sentensi fupi nisikuchoshe
--
- 1:- Watu ambao -tunadhani wamekufa kwa mapenzi ya Mungu kumbe wamechukuliwa kiuchawi. Tunazika -migomba, vinu na madude mengine huku tukiwa tumechezewa macho. Ni kama -mazingaombwe vile, mtu anachoma mkuki kichwani na anatembea akidai yeye ni profesa bingwapotea -na ataonyesha mazingaombwe hayo sehemu fulani kwa kiingilio lakini -kibaolojia jambo hilo haliwezekani. Ni kuchezea macho watu tu ambacho wachawi -wanafanya na tukiomba wanadamu wenzetu hawa wanarudi. Zipo dalili tele utaziona -msibani, kama ndugu yako amechukuliwa kichawi. mfano -jeneza zito kuliko kawaida, gari kukataa kwenda, mwili wa marehemu -mreefu sana kuliko kawaida na mauzauza mengi msibani. Ukiona hali kama hiyo -usizembee ni kuomba na kumwita mtu huyo kwa jina lake, Yesu alimwita Lazaro 'NJOOOO -HUKU NJE" na wewe ita -Njooo kwa jina La Yesu na unaweza kushangaa kitachotokea hutaamini. Watu hawa wapo na wanashuhudia waziwazi. Sio -kwamba hawafahamiki kama wadau wengi walivyosema wana familia zao na familia -zao zimetoa ushahidi wa wazi wazi.

--
- 2;- Kuna watu huchukuliwa wazimawazima, utakuta ndani ya jamii mtu anapotea. Mjomba alipoteaga zamani, baba aliondoka hakurudi tena, mwanangu mwaka wa nane aliondokaga nyumbani hatujui alipo, ni watu wengi sana wamekumbwa na kadhia hii, jamii haina majibu na jambo hili. Watu hawa wapo, wamefichwa kwenye majumba ya watu, wanabeba maboksi, wanakata miwa, wanafanya kazi za mahotelini na nyinginezo, wakiitwa wanarudi na tunazo shuhuda nyingi za audio na dvd za watu hawa.

--
- 3:- Aina hii ya Tatu ni watu wengi sana, Kimwili tunao ila Kiroho hawapo. mtu anachukuliwa roho na mwili unabakia. Mwili ule unapandiwa roho nyingine ya shetani na mtu huyo anaendelea kufanya operation za maisha kama kawaida akipretend ni yeye wa asili kumbe ni maroho ya kishetani. Hii ni common sana kwenye jamii zetu watu wengi ni misukule lakini barabarani wanakatiza na kazi wanafanya. Unaweza kuoa au kuolewa na msukule bila kujua na hapo ndippo utapokoma kwenye ndoa. Nikupe baadhi ya tabia ya misukule hawa.

- a) - Mume msukule:- -Ana tabia ya ukali uliopitiliza, hawezi kabisa kutembea na mkewe kwa -njia ya kawaida lazima iwe kinyume na maumbile, lazima atembeee na -mwanamke yeyote ndani ya nyumba yake iwe housegirl au ndugu yeyote ndani -ya nyumba yake (si wote wanaotembea na h/g ni misukule ila ishara -kwa misukule kuna dalili ambazo siwezi sisema hapa utazigundua kwa aliye -tembea na msukule). hawezi kuwazia maendeleo zaidi ya pombe, kipigo na tabia ambazo mwanadamu wa kawaida hawezi kuzifanya

- b) - Mke msukule:- ni mkorofi, mgomvi, anatokwa na damu sana, anaota anapaa au kula nyama usiku, magonjwa mwilini hayaishi kila siku ni mgonjwa madawa na madawa. Ni ngumu kubeba mimba na akibeba hutoka.-

- c) - Mtoto msukule; unashangaa tu mtoto kawa mjingamjinga, masomo yalikuwa mazuri la kwanza, pili tatu lakini ghafla ameshuka hadi wa mwisho na wala hana bidii ya kusoma unaweza ukapiga mtoto bure kumbe keshachukuliwa.

- d) - Housegirl msukule:- kifupi hapo ndoa hakuna, watoto wakimwona wanalia sana ila yeye anapretend kuwapenda na ukienda kazini huku nyuma watoto wananyukwa isivyo kawaida. Mchunguze bint yako unaporudi kazini. Na lazima amfanyizie vimbwanga mumeo na kifupi lazima aisambaratishe nyumba.watu wengi -wanayashabikia matukio haya kama ni ya kawaida kwenye jamii, sure i am -telling you hao si binaadamu wa kawaida. wanawake na wanaume wanaojiuza -asilimia kubwa ni misukule, na jambo baya ni kwamba ukitembea tu na -msukule na wewe unachukuliwa.. jichunguze mara baada ya kutembea na mtu -fulani ham ya maisha ilitoweka, bidii ya kazi ilikwisha, unachoka sana -na kulalalala masaa yote, ni mvivu kupindukia.. HAUPO.!!

- e) - Bosi msukule:- kama wewe ni mlolkole siku ukifanya maombi sana basi ofisini utapata matatizo mengi from huyo bosi msukule.
- Kuna category nyingi kwa leo niishie hizo

--
- Watu wote hawa wanarudishwa, na si kwamba hawajulikani, wanajulikana vizuri kabisa kwa jamii zao na jambo hili ni wazi kabisa hata kwenye mikutano yetu huwa tunaweka namba zao za simu kwa mwenye simu ili ampigie na kujiridhisha na kila hoja anayotaka aeleweshwe.-

LAKINI ZAIDI TEMBELEA-
website: UFUFUO NA UZIMA (GCTC)
blogu: -ufufuonauzima.blogspot.com
au jiunge na facebook Group: Ufufuo Crew
au nitumie E-mail: bihagaze@yahoo.co.uk
au piga simu moja kwa moja 0713254210

ahsanteni na mungu awabarikie
 
Mimi nadhani Gwajima alikuja na misukule yake kuwadanganya watu. Kama kweli amefufua watu hebu tujiulize hao watu wako wapi kama siyo amewachukua?

Mungu atupatie maarifa na hekima ya kutambua

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Humu jamvini kuna watu wengi sana. kama kweli wapo waliofufuliwa basi mmoja wetu humu anaweza kujua msukule mmoja aliyefufuliwa akatupa ushuhuda pasipo mashaka.
Inaonekana Wanaojipa majina makubwa ya utume, uaskofu nk. wanatumia neno imani na kuwageuza waumini wao kama watoto wanaodaganywa kuwa mtoto huletwa na ndege nk. juzi nalimsikia Lusekelo akitamba kuwa ana uwezo wa kuingia Somalia chini ya saa tatu na akawaangamiza Alshabab. aliendelea kudai anaweza kuingia nhi yoyote duniani muda wowote na kufanya lolote kwa njia za kimuujiza. alithibitisha hayo kwa namna alivoipeperusha Elnino. Waumini walimshangilia sana na kumzawadia mahela. Haya mambo ni Puzzle! Kwa kweli unatakiwa ushuhuda wa kweli. Kama Kweli Mungu yupo na anayaona haya basi ataweka yote wazi kwa sababu ana uwezo huo
 
Mimi huwa nachokaga na haya mambo. Sijawahi kufika katika hizo ibada ila nachojiuliza hao wanaoitwa misukule inafikaje hapo kwa Gwajima..yaani kama huyo alietoka Mortuary alikuja mwenyewe au? Duuh...
umesem sawa kwa sababu misukule haipaswi kuonyeshwa kanisani bali mfufuaji angeenda huko iliko akaiita na kuifufua kama yesu alivomfufua Lazro pale kaburini. Mfufuaji anaifufulia waapi muda gani na akiwa na kina nani na kwa sababu zipi au ombi la nani? Nadhani kuna haja ya sheria za nchi kutoa ufafanuzi juu ya mambo haya ya ufufuaji yasijeachwa kila mtu akajiingiza huko kwa sababu ya kifsadi na kiaghai
 
umesem sawa kwa sababu misukule haipaswi kuonyeshwa kanisani bali mfufuaji angeenda huko iliko akaiita na kuifufua kama yesu alivomfufua Lazro pale kaburini. Mfufuaji anaifufulia waapi muda gani na akiwa na kina nani na kwa sababu zipi au ombi la nani? Nadhani kuna haja ya sheria za nchi kutoa ufafanuzi juu ya mambo haya ya ufufuaji yasijeachwa kila mtu akajiingiza huko kwa sababu ya kifsadi na kiaghai

............sisi Waislaam, hutusumbuki na huo ujinga, Alhamdulilahi !
1. Nabii Ibrahim AS, yeye alikuja karne ya wajinga !.......watu wakiabudu nyota, jua, mito, masanamu, vitu walivyotengeza kwa mikono yao !.......Nabii Ibrahim, alifunja masanabu yaliyokuwa yakiabudiwa na Makafiri, kisha akaliacha kubwa lao. Wenye Masanamu waliporudi, wakauliza ni nani amevunja vunja miungu yao ? .....Nabii Ibrahim akwaambia waliulize kubwa lao, wenzake wamepatwa na nini ?
2. Nabii Musa AS, yeye alikuja karne ya wachawi !.........wakionyesha mazingaombwe na miujiza. Musa AS akajaliwa miujiza mikubwa zaidi yao !
3. Nabii Issah AS mwana wa Maryam (Yesu) yeye alikuja karne ya Utabibu, kulikuwwa na Waganga wengi wakisaidia jamii matibabu, ingawa kuna magonjwa ambao Matabibu uliwashinda. Ukiwapo ugonjwa wa ukoma !
Issah AS (Yesu) yeye alijaliwa miujiza ya kuponya upofu, mbalanga, ukoma na hata kufufua 'bi idhini llahi'
4. Nabii Muhammad SAW, yeye alikuja karne ya hoja ! Yeye alikuja kufumbua fumbo la uumbaji wa Dunia na kutoa 'fact' zinazoonyesha uwepo wa Allah SWT.

'Enyi watu ! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na Mwanaume na Mwanamke. Na tumekujakujalieni kuwa Mataifa na Makabila ili mjuane. Hakika aliye Mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye habari.
Qur'an: 49:13
 
linapokuja swala lakufa ili ni jambo jingine, but i think misukule sio kufa per Se, bali ni mtu kuibiwa ama kufichwa kimazingara something like that.:tape:
 
............sisi Waislaam, hutusumbuki na huo ujinga, Alhamdulilahi !
1. Nabii Ibrahim AS, yeye alikuja karne ya wajinga !.......watu wakiabudu nyota, jua, mito, masanamu, vitu walivyotengeza kwa mikono yao !.......Nabii Ibrahim, alifunja masanabu yaliyokuwa yakiabudiwa na Makafiri, kisha akaliacha kubwa lao. Wenye Masanamu waliporudi, wakauliza ni nani amevunja vunja miungu yao ? .....Nabii Ibrahim akwaambia waliulize kubwa lao, wenzake wamepatwa na nini ?
2. Nabii Musa AS, yeye alikuja karne ya wachawi !.........wakionyesha mazingaombwe na miujiza. Musa AS akajaliwa miujiza mikubwa zaidi yao !
3. Nabii Issah AS mwana wa Maryam (Yesu) yeye alikuja karne ya Utabibu, kulikuwwa na Waganga wengi wakisaidia jamii matibabu, ingawa kuna magonjwa ambao Matabibu uliwashinda. Ukiwapo ugonjwa wa ukoma !
Issah AS (Yesu) yeye alijaliwa miujiza ya kuponya upofu, mbalanga, ukoma na hata kufufua 'bi idhini llahi'
4. Nabii Muhammad SAW, yeye alikuja karne ya hoja ! Yeye alikuja kufumbua fumbo la uumbaji wa Dunia na kutoa 'fact' zinazoonyesha uwepo wa Allah SWT.

'Enyi watu ! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na Mwanaume na Mwanamke. Na tumekujakujalieni kuwa Mataifa na Makabila ili mjuane. Hakika aliye Mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye habari.
Qur'an: 49:13

Yaani kama ni michezo wengine wanacheza football mwenzetu netball, Mbaaaali sana, gizani kuleeeee.. Anyway Nuru yaja, Kazi ya nuru ni kuangaza gizani..
 
Yaani kama ni michezo wengine wanacheza football mwenzetu netball, Mbaaaali sana, gizani kuleeeee.. Anyway Nuru yaja, Kazi ya nuru ni kuangaza gizani..

Pan Inzinier Bihagaze;

Is it OK to use lies to glorify God?
 
jamani hili nchi limekuwa ni mtaji kwa wajanja wengi hata wachina ukienda kwao wanatangaziana jamani ee kuna inchi linaitwa Tanzania lina raia wajinga sana na ukienda masikini unarudi tajiri so mtaji wa gwajima na wachungaji wengine wa miujiza ni kuwepo kwa mindugu zetu mitahira mingi.
YAANI UTAKUTA YANAMUHUSUDU GWAJIMA KUSHINDA HATA YESU NA MUNGU YAANI HAYA MAFARA YAACHENI YAZIDI KULIWA MPAKA SIKU YA MWISHO LUSEKELO ANAYACHANGISHA HADI HELA YA NAULI NA AMEYAWEKEA MABASI YA KUWAPEREKA KWAO BAADA YA KULIWA HELA ZOTE.
HILI HALIPINGIKI MIJINGA ITALISHA WAJANJA MPAKA SIKU YA KIFO CHAO.
 
Huyu mse.nge si angeenda kutufufulia steve job, isac newton. Jk nyerere ambao ni watu muhimu sana kwa maendeleo anakuja na waigizaji wake anaowaweka kule bagamoyo na nchi jirani kudanganya wamefufuliwa.
 
............sisi Waislaam, hutusumbuki na huo ujinga, Alhamdulilahi !
1. Nabii Ibrahim AS, yeye alikuja karne ya wajinga !.......watu wakiabudu nyota, jua, mito, masanamu, vitu walivyotengeza kwa mikono yao !.......Nabii Ibrahim, alifunja masanabu yaliyokuwa yakiabudiwa na Makafiri, kisha akaliacha kubwa lao. Wenye Masanamu waliporudi, wakauliza ni nani amevunja vunja miungu yao ? .....Nabii Ibrahim akwaambia waliulize kubwa lao, wenzake wamepatwa na nini ?
Kwahiyo huyo Ibrahimu wenu hii imani aliimaliza au hakuimaliza?
Na kama hakuimaliza ni nini lilikuwa jukumu lake?
2. Nabii Musa AS, yeye alikuja karne ya wachawi !.........wakionyesha mazingaombwe na miujiza. Musa AS akajaliwa miujiza mikubwa zaidi yao !
Kwa mujibu wa maelezo yako haya Mussa huyu alikabiliana na wachawi ni kwanini nyie hamkabiliani na hawa wachawi wa sasa?
3. Nabii Issah AS mwana wa Maryam (Yesu) yeye alikuja karne ya Utabibu, kulikuwwa na Waganga wengi wakisaidia jamii matibabu, ingawa kuna magonjwa ambao Matabibu uliwashinda. Ukiwapo ugonjwa wa ukoma !
Issah AS (Yesu) yeye alijaliwa miujiza ya kuponya upofu, mbalanga, ukoma na hata kufufua 'bi idhini llahi'
Kwanini alifufua na kuponya wagonjwa?
4. Nabii Muhammad SAW, yeye alikuja karne ya hoja ! Yeye alikuja kufumbua fumbo la uumbaji wa Dunia na kutoa 'fact' zinazoonyesha uwepo wa Allah SWT.
Kwanini unadanganya umma?
Mohammad alifumbua kitu gani kuhusu uumbaji wa dunia?

Mussa alishalizungumza hili kwenye Biblia zaidi ya miaka 3000 kabla ya Mohammad wewe unakuja kusema alifumbua fumbo la uumbaji?Hebu acha masikhara kijana
'Enyi watu ! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na Mwanaume na Mwanamke. Na tumekujakujalieni kuwa Mataifa na Makabila ili mjuane. Hakika aliye Mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye habari.
Qur'an: 49:13
"Sisi" ni akina nani hao?
Halafu hii ni kauli ya nani?
 
Hakuna mwenye uwezo wa kumfufua mtu zaidi ya Yesu na baadhi ya mitume kama
Elia aliyemfufua mtoto wa yule mjane; Petro aliyemfufua Dorcus au Tabita

Hawa wanaojiita mitume na manabii wa miaka hii ni njaa tu hawa lolote.
 
Back
Top Bottom