Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Maneno yenu yanafanana kabisa na wale waliokuwa wakimkebehi Yesu msalabani wakisema na ajiokoe mwenyewe sasa!!! Kama Yesu mwenyewe aliitwa mchawi na kudhihakiwa itakuwa hawa watumishi wake?

Binafsi najua kuna usanii mwingi siku hizi na pia siendi ovyo kwenye makanisa ya kilokole lakini pia sibezi kazi ya Mungu kupitia wachungaji kisa tu kuna wasanii.Kama ni usanii nitafanya utafiti wangu mwenyewe kupitia mafundisho yake na huduma yake ili kupitia matunda ya huduma yake nijue kama kweli ni mtumishi wa Mungu.
 
tuwache kuingiza neno la mungu
kwenye ushabiki usiokuwa na mpango Mungikama unakataa kitu kataa kwa neno mimi neno la mungu linaniambia nikimwamini nitafanya zile kazi yesu alikuwa anazifanya tena na kubwa zaidi ya hapo sioni koza kunyanganya mchawi mtu na kuleta kwa yesu
kwani watu wanaopinga tu kwa akilizao ndio mwisho wa akili zao
mnyinda,
Mimi sikatai habari za ufufuo, so long naamini Yesu Kristo yupo na anaishi. Ninachosema siyo kupinga nielewe, bali ninataka unipe ufafanuzi kuwa, hao misukule waliofufuliwa Arusha hivi sasa wako wapi? je, wamerudi kwa ndugu zao? je, hao misukule waliofufuliwa ndugu zao ni akina nani? je, bado hawajitambua kuwa wao ni nani? kama hawajitambui basi naamini bado hawajafufuliwa katika kristo, bali katika mazingaombwe.
hivi tunapozungumza watu wametoka Arusha wameenda kwenye mikutano yake tena Moshi, Misukule wale wale waliofufuka Arusha ndiyo wanaoendelea kufufuka Moshi.
Hebu nifungue hata kiroho mtumishi wangu mnyinda
 
Last edited by a moderator:
soma 1wakorinto 13 soma yote biblia bana kila kitu kipo ila ni jinsi unavyokitafsiri... miujiza na karama zote vimeshakomeshwa..

miujiza ni nini? na karama ni nini? mnaona kupitia kupondaponda ovyo wachungaji wakati mwingine bila sababu za msingi mnajikuta mnaanza kumponda Mungu mwenyewe bila kujua?
 
mnyinda,
Mimi sikatai habari za ufufuo, so long naamini Yesu Kristo yupo na anaishi. Ninachosema siyo kupinga nielewe, bali ninataka unipe ufafanuzi kuwa, hao misukule waliofufuliwa Arusha hivi sasa wako wapi? je, wamerudi kwa ndugu zao? je, hao misukule waliofufuliwa ndugu zao ni akina nani? je, bado hawajitambua kuwa wao ni nani? kama hawajitambui basi naamini bado hawajafufuliwa katika kristo, bali katika mazingaombwe.
hivi tunapozungumza watu wametoka Arusha wameenda kwenye mikutano yake tena Moshi, Misukule wale wale waliofufuka Arusha ndiyo wanaoendelea kufufuka Moshi.
Hebu nifungue hata kiroho mtumishi wangu mnyinda

Wewe ndio umeuliza vizuri ingawa sina jibu lako kwakuwa sihusiki na huduma ya Gwajima.Umekiri kuwa Yesu anaweza ingawa una mashaka na huduma ya huyu mchungaji kitu ambacho ni cha kawaida kwani hata Tomaso hakukubali kirahisi na Yesu mwenyewe alisema akina Tomaso wapo wengi.
 
Umeulizwa swari la msingi sana na Eiyer lakini unajibu porojo. Kama jambo huna ufahamu nalo lanini unalikurupukia? Wakristo wenyewe tena wenye imani juu ya Yesu hawana shaka na hili. Unabisha bila facts na bila kuwa na uwelewa wowote wa jambo husika. Kaa chini ufundishwe NENO kwanza.

ahaa! Neno la misukule uliliona wapi?
Mtu akifa huwa anapoteza origin kabisa? umeambiwa wazi kabisa hao misukule huwa hawana ndugu na hata watu wanaowatambua.
Wengine hudai kuwa wametoka mochwari, sasa huoni kama ni uongo huo na maigizo ya wazi kabisa?
 
Mimi sio muumini wa hao uliowataja lakini ni Mkristo
Nalazimika kukuuliza yafuatayo

Ni kwanini unasema hayo ni maigizo?
Je unaujuzi wa hayo?
Kama ni ndio tuambie hapa

Pia tuambie unajua nini kuhusiana na misukule
Je una ufahamu wowote na hiyo kitu "maigizo"?

Nasema ni maigizo kwa sababu inawezekana hao misukule ni wakutengeneza tu.

Isije kuwa ni wivu tu wa kukosa waumini huko uliko ndio umekuongoza kuleta haya
 
Mkuu kiwatengu ni kweli huyu Josephat Gwajima anaonekana msanii, maana hivi tunavyozungumza anafanya mikutano Moshi. Lakini cha ajabu Misukule wale wale waliofufuka Arusha wameanza kufufuka Moshi. Inamaana baada ya kufufuka Arusha walikufa, hivi sasa ndiyo wanafufuka tena Moshi.
Jamaa anatembea na misukule kwenye Hammer.
Wakristo tunatakiwa tujiulize, kama kweli alikuja kufufua ndugu zetu, je, baada ya kufufuliwa wameenda wapi?

Usanii huu unatisha

Ajabu iliyopo bado hapa kuna wanaoamini ni kwa Jina la YESU gwajima anayafanya haya!!
 
Last edited by a moderator:
Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha..
Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa..

Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma,

Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa!

Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa..
hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!!

Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..

Yesu ndio Ufufuo na Uzima! Hakuna Ufufuo kwa mwanadamu yeyote Yule! Huo ni upotoshaji mkubwa!
Tena Maandiko yako wazi kabisa Ile Yohana 11:25 inasema wazi kabisa kua Yesu ndio Ufufuo na uzima!
 
Misukule ni watu waliochukuliwa kichawi! Na Labda Hapa tungetofautisha Misukule na Wafu! Sasa Hapa ni watu gani wanaofufuliwa? Misukule au Wafu? Manake Kama Misukule ni maigizo na ushirikina tu na Kama ni Wafu hakunaga hiyo kitu mpaka arudi mwenyew Kamanda!
 
unanitafutia tafsiri? nimeandika ulichouliza?

Hoja ilikuwa kwa nn huyo mchungaji asiende mahospitalini kuponya wagonjwa, wewe ukasema kuwa wagonjwa ndo waliotakiwa kumfuata kwa mfano ya Yesu kuwa wagonjwa ndo walimfuata sasa nimekuuliza hiyo misukule ndo inamfuata Huyo mchungaji?
 
Maneno yenu yanafanana kabisa na wale waliokuwa wakimkebehi Yesu msalabani wakisema na ajiokoe mwenyewe sasa!!! Kama Yesu mwenyewe aliitwa mchawi na kudhihakiwa itakuwa hawa watumishi wake?

Binafsi najua kuna usanii mwingi siku hizi na pia siendi ovyo kwenye makanisa ya kilokole lakini pia sibezi kazi ya Mungu kupitia wachungaji kisa tu kuna wasanii.Kama ni usanii nitafanya utafiti wangu mwenyewe kupitia mafundisho yake na huduma yake ili kupitia matunda ya huduma yake nijue kama kweli ni mtumishi wa Mungu.

aise unaonekana una maslahi makubwa na huyo mchungaji maana kubanduki humu kumtetea
 
Sitaamini kamwe kwenye ufufuo wa aina hii..
Mungu naomba usinitoe katika imani niliyonayo,
inayonifunza katika kuyakabili maisha kwa njia ya halali! kutafuta kwa jasho..

Dah! mkuu watu8 huwa nakumbuka sana hoja yako uliowahi kuitoa sehemu juu ya kuwaamini watu kama kina Gwajima!

Hili la misukule mh! hapana kabisa!!

Kaka mkubwa ninaomba nikuulize maswali kadhaa, yakiwemo yale niliyokuuliza wakati uliopita na ukayapotezea:

1. Misukule ni kitu gani au ni nini?

2. Hapo juu umeandika kuwa huamini katika aina hiyo ya ufufuo, je unaamini katika aina ipi ya ufufuo?

3. Je unadhani mtu akifanya mambo makuu kwa jina la Kristo zaidi ya yale aliyoyafanya Kristo mwenyewe, je mtu huyu atakuwa anakosea?

NB:
Nimekuuliza hayo kwa kuwa ninaamini kuna jambo unalolifahamu kuhusu imani ipi ni sahihi na ipi si sahihi, pia ninaamini kuna jambo unafahamu juu ya yapi yakitendwa kwa jina la Kristo ni sahihi na yapi si sahihi.
Kwa mantiki hiyo ndio maana umeweza kuweka uthubutu na kuandaa thread yenye kukosoa kuhusu yale ayatendayo Gwajima.
Maana natambua kuwa, "siku zote yule mtu asiyejua katu hawezi kumkosoa yule ajuaye". Karibu utueleze kwa kina hayo ujuayo.
 
linapokuja suala la Imani huwa nashindwa wa kumuamini iwe msomi au yeyote ni utashi wa Mungu tuu ndio huhitajika... jiulize maswali haya. misukule Ndugu zake nani? wanaishi wapi baada ya ufufuaji? walikuwa wapi kabla? waliwahi kufanya kazi au kushiriki shughuli za kijamii mahali? wanaweza kuleta mazingira ya wazi kuonyesha misukule hukaa wapi? hula nini? huko misukule nayo hufa? nani aliwachukua kama misukule? kama huna majibu dhahiri yanatia shaka. hiyo itakuwa Imani tuu ambayo sio halisi kudanganya watu tuu.
 
Hoja ilikuwa kwa nn huyo mchungaji asiende mahospitalini kuponya wagonjwa, wewe ukasema kuwa wagonjwa ndo waliotakiwa kumfuata kwa mfano ya Yesu kuwa wagonjwa ndo walimfuata sasa nimekuuliza hiyo misukule ndo inamfuata Huyo mchungaji?

Basi ungeuliza nini kimetokea ili wanaojua wakuelimishe lakini sio kuanza kwa kupotosha habari za namna Mungu anavyofanya kazi.

Lakini pia watu wanaohudhuria hiyo mikutano ndio wanaopaswa kusaidia wengine kuelezea kilichotokea ili kuwa wazi hivi vitu kupunguza upotoshaji (ingawa huwezi kumaliza ubishi).

Ukweli kuhusu misukule ya Gwajima siujui na siwezi kuwasemea chochote lakini nini msimamo wangu kuhusu misukule na imani yangu nimeelezea post zilizopita ukipitia kila post utaelewa nasimamia nini tangu mwanzo.

Ukisoma hata post yangu ya kwanza kabisa inatosha kukuonesha nasimamia nini.
 
Yesu ndio Ufufuo na Uzima! Hakuna Ufufuo kwa mwanadamu yeyote Yule! Huo ni upotoshaji mkubwa!
Tena Maandiko yako wazi kabisa Ile Yohana 11:25 inasema wazi kabisa kua Yesu ndio Ufufuo na uzima!

Ndugu yangu hebu isome Biblia vizuri na uielewe....hiyo nukuu uliyotoa ni O.P.

Mathayo 10:

7 Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
 
Basi ungeuliza nini kimetokea ili wanaojua wakuelimishe lakini sio kuanza kwa kupotosha habari za namna Mungu anavyofanya kazi.

Lakini pia watu wanaohudhuria hiyo miku
tano ndio wanaopaswa kusaidia wengine kuelezea kilichotokea ili kuwa wazi hivi vitu kupunguza upotoshaji (ingawa huwezi kumaliza ubishi).

Ukweli kuhusu misukule ya Gwajima siujui na siwezi kuwasemea chochote lakini nini msimamo wangu kuhusu misukule na imani yangu nimeelezea post zilizopita ukipitia kila post utaelewa nasimamia nini tangu mwanzo.

Ukisoma hata post yangu ya kwanza kabisa inatosha kukuonesha nasimamia nini.

Hili swala haliitaji kuhudhuria mikutano yake au huduma Zake au kuwaita waumini wake watupatie majibu!
Kwa yeyote anaeufahamu ukweli wa Maandiko kwa hili hawezi kushindwa kulitolea majibu!
Hakuna cha Ufufuo wa Misukule au nini! Usanii mtupu!
 
Mimi sio muumini wa hao uliowataja lakini ni Mkristo
Nalazimika kukuuliza yafuatayo

Ni kwanini unasema hayo ni maigizo?
Je unaujuzi wa hayo?
Kama ni ndio tuambie hapa

Pia tuambie unajua nini kuhusiana na misukule
Je una ufahamu wowote na hiyo kitu "maigizo"?

Isije kuwa ni wivu tu wa kukosa waumini huko uliko ndio umekuongoza kuleta haya!

maswali mazuri sana.
Mimi siku zote nasema uwezo wa kuvumilia imani za wengine ni hekima kubwa.
 
Back
Top Bottom