Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 73,773
- 102,126
Mi nilidhani hoja ya Mungi uliielewa pale mwanzo..
inakuwaje tena unaanza kushikamana na maelezo ya watu8? anayetumia refference ya biblia ambayo kila mtu anaweza kuitafsiri kwa jinsi anavyoweza na bado akaeleweka?
lets sticky into reality mkuu!
umeambiwa misukule iliyofufuliwa huko Arusha ndiyo inayoonekana Moshi kwa ufufuo tofauti..
usanii mtupu, afu bado tuamini kuwa YESU anatumika hapo?
Hahaha mkuu kwa maelezo haya sasa nimejua kuwa dhumuni la bandiko hili ni kujaribu kumchambua Gwajima na yale afanyayo...
Kwa mantiki hiyo sidhani kama nitaweza kuendelea na mjadala huu, ningekuwa radhi kama tu tungekuwa tunajadili uwezo, nguvu na mamlaka ya Kristo...
Maana tukiongea habari za Kristo pasipo na shaka yoyote Mkatoliki, Mlutheri, Msabato na wengineo tungeelewana kwa kuwa tungekuwa tunazungumza lugha moja...ila hili la kumjadili mtu binafsi ni ngumu kwangu.