Ntuzu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 17,418
- 10,877
Mkuu kifo katika katika imani ya kikristo ni ile kutengwa na Mungu, ndio maana tunaambiwa Yesu alikuja duniani na kila aliyemwamini ana uzima tele. Unapokufa hapa duniani, ndio mwisho wa mwili huu wa nyama lakini ndio mwanzo wa maisha yako ya milele. Na ndio maana mwili unapingana na roho kwa sababu unataka upate vitu vyote vya duniani lakini roho itaishi milele.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yohana 3:16
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Warumi 6:23
Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele; asiyemtii Mwana hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake daima
Yohana 3:36
Hapa ninachokiona ni ule uzima wa milele hayo ndio maisha yanayozungumziwa na kwamba Sio maisha baada ya Kifo!