mnyinda,tuwache kuingiza neno la mungu
kwenye ushabiki usiokuwa na mpango Mungikama unakataa kitu kataa kwa neno mimi neno la mungu linaniambia nikimwamini nitafanya zile kazi yesu alikuwa anazifanya tena na kubwa zaidi ya hapo sioni koza kunyanganya mchawi mtu na kuleta kwa yesu
kwani watu wanaopinga tu kwa akilizao ndio mwisho wa akili zao
soma 1wakorinto 13 soma yote biblia bana kila kitu kipo ila ni jinsi unavyokitafsiri... miujiza na karama zote vimeshakomeshwa..
mnyinda,
Mimi sikatai habari za ufufuo, so long naamini Yesu Kristo yupo na anaishi. Ninachosema siyo kupinga nielewe, bali ninataka unipe ufafanuzi kuwa, hao misukule waliofufuliwa Arusha hivi sasa wako wapi? je, wamerudi kwa ndugu zao? je, hao misukule waliofufuliwa ndugu zao ni akina nani? je, bado hawajitambua kuwa wao ni nani? kama hawajitambui basi naamini bado hawajafufuliwa katika kristo, bali katika mazingaombwe.
hivi tunapozungumza watu wametoka Arusha wameenda kwenye mikutano yake tena Moshi, Misukule wale wale waliofufuka Arusha ndiyo wanaoendelea kufufuka Moshi.
Hebu nifungue hata kiroho mtumishi wangu mnyinda
njooni kwenye nuru ya uislam. Hakuna maigizo wala tamthilia.
Ni uhalisia na mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu.
Umeulizwa swari la msingi sana na Eiyer lakini unajibu porojo. Kama jambo huna ufahamu nalo lanini unalikurupukia? Wakristo wenyewe tena wenye imani juu ya Yesu hawana shaka na hili. Unabisha bila facts na bila kuwa na uwelewa wowote wa jambo husika. Kaa chini ufundishwe NENO kwanza.
Mimi sio muumini wa hao uliowataja lakini ni Mkristo
Nalazimika kukuuliza yafuatayo
Ni kwanini unasema hayo ni maigizo?
Je unaujuzi wa hayo?
Kama ni ndio tuambie hapa
Pia tuambie unajua nini kuhusiana na misukule
Je una ufahamu wowote na hiyo kitu "maigizo"?
Nasema ni maigizo kwa sababu inawezekana hao misukule ni wakutengeneza tu.
Mkuu kiwatengu ni kweli huyu Josephat Gwajima anaonekana msanii, maana hivi tunavyozungumza anafanya mikutano Moshi. Lakini cha ajabu Misukule wale wale waliofufuka Arusha wameanza kufufuka Moshi. Inamaana baada ya kufufuka Arusha walikufa, hivi sasa ndiyo wanafufuka tena Moshi.
Jamaa anatembea na misukule kwenye Hammer.
Wakristo tunatakiwa tujiulize, kama kweli alikuja kufufua ndugu zetu, je, baada ya kufufuliwa wameenda wapi?
Usanii huu unatisha
Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha..
Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa..
Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma,
Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa!
Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa..
hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!!
Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..
unanitafutia tafsiri? nimeandika ulichouliza?
Maneno yenu yanafanana kabisa na wale waliokuwa wakimkebehi Yesu msalabani wakisema na ajiokoe mwenyewe sasa!!! Kama Yesu mwenyewe aliitwa mchawi na kudhihakiwa itakuwa hawa watumishi wake?
Binafsi najua kuna usanii mwingi siku hizi na pia siendi ovyo kwenye makanisa ya kilokole lakini pia sibezi kazi ya Mungu kupitia wachungaji kisa tu kuna wasanii.Kama ni usanii nitafanya utafiti wangu mwenyewe kupitia mafundisho yake na huduma yake ili kupitia matunda ya huduma yake nijue kama kweli ni mtumishi wa Mungu.
Sitaamini kamwe kwenye ufufuo wa aina hii..
Mungu naomba usinitoe katika imani niliyonayo,
inayonifunza katika kuyakabili maisha kwa njia ya halali! kutafuta kwa jasho..
Dah! mkuu watu8 huwa nakumbuka sana hoja yako uliowahi kuitoa sehemu juu ya kuwaamini watu kama kina Gwajima!
Hili la misukule mh! hapana kabisa!!
aise unaonekana una maslahi makubwa na huyo mchungaji maana kubanduki humu kumtetea
Hoja ilikuwa kwa nn huyo mchungaji asiende mahospitalini kuponya wagonjwa, wewe ukasema kuwa wagonjwa ndo waliotakiwa kumfuata kwa mfano ya Yesu kuwa wagonjwa ndo walimfuata sasa nimekuuliza hiyo misukule ndo inamfuata Huyo mchungaji?
Yesu ndio Ufufuo na Uzima! Hakuna Ufufuo kwa mwanadamu yeyote Yule! Huo ni upotoshaji mkubwa!
Tena Maandiko yako wazi kabisa Ile Yohana 11:25 inasema wazi kabisa kua Yesu ndio Ufufuo na uzima!
Basi ungeuliza nini kimetokea ili wanaojua wakuelimishe lakini sio kuanza kwa kupotosha habari za namna Mungu anavyofanya kazi.
Lakini pia watu wanaohudhuria hiyo miku
tano ndio wanaopaswa kusaidia wengine kuelezea kilichotokea ili kuwa wazi hivi vitu kupunguza upotoshaji (ingawa huwezi kumaliza ubishi).
Ukweli kuhusu misukule ya Gwajima siujui na siwezi kuwasemea chochote lakini nini msimamo wangu kuhusu misukule na imani yangu nimeelezea post zilizopita ukipitia kila post utaelewa nasimamia nini tangu mwanzo.
Ukisoma hata post yangu ya kwanza kabisa inatosha kukuonesha nasimamia nini.
Mimi sio muumini wa hao uliowataja lakini ni Mkristo
Nalazimika kukuuliza yafuatayo
Ni kwanini unasema hayo ni maigizo?
Je unaujuzi wa hayo?
Kama ni ndio tuambie hapa
Pia tuambie unajua nini kuhusiana na misukule
Je una ufahamu wowote na hiyo kitu "maigizo"?
Isije kuwa ni wivu tu wa kukosa waumini huko uliko ndio umekuongoza kuleta haya!