Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ufufuaji wa Misukule: Ina tofauti gani na Maigizo?

Ulilolisema ni ngumu sana kutekelezeka! misukule wana ma bodyguard..
u cant touch them!!

Nilisema wewe piga keleuuwiiii. Mwite jina lolote na kusema unamjua tena ni wa kwenu kijiji tena useme kwa sauti kuwa mama yake yupo utamleta hapo hapo na kuomba waandishi wampige picha. Kama ni wa utapeli atakimbia
 
Nilisema wewe piga keleuuwiiii. Mwite jina lolote na kusema unamjua tena ni wa kwenu kijiji tena useme kwa sauti kuwa mama yake yupo utamleta hapo hapo na kuomba waandishi wampige picha. Kama ni wa utapeli atakimbia

aisee! Mkuu mawazo yako unayapeleka kama vile inawezekana, ukipiga kelele pale, utaanza kuombewa na wewe kama vile una mapepo..

Ogopa mipango ya watu, inayowapa kula!
 
Kuna mtu alisema wanaombea wagonjwa na wanapona,sasa swali la kujiuliza kwanin wasiwe wanaenda hospital moja kwa moja? Na kama umate umate si watapewa na ndugu wa wagonjwa?
 
Kazi kidogo tu ilu;
Nenda kwenye mkutano wake au kanisani kwake, akisema tu kwamba kuna msukule hapa, wahi mbele. Mkamate huyo msukule, ng'angania kuwa ulimjua na utampeleka kwao.
Mpelekee waandishi wa habari, wamchimbe miswali mpaka ateme uongo wake. Utakuwa umetuponya wengi na utamwaibisha huyo Gwajima Ni kaushauri tu kwako ilu.

Heee mangatara huo ushauri wako mmmhh unataka mm niwe mbuzi wa sadaka eee... Unajua gjarama ya kuharibu deal za watu lakini?
 
Last edited by a moderator:
Binadamu kila kukicha tunazidi kupata mbinu za kuyakabili maisha..
Inafikia hatua ya kujigeuza miungu watu sasa..

Kwa kujipa uwezo wa kuwafufua binadamu waliokufa siku za nyuma,
Ndugu zangu haswa Wakristo na Wafuasi wa Gwajima (Ufufuo na Uzima) kuweni makini sana na maigizo mnayofanyiwa!

Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kumrudishia uhai mtu aliyekufa..
hili alifanya YESU peke yake tena mara chache sana!!

Tutakoseshwa mbingu kwa kudanganyika na kumezeshwa imani zisizoendana na Mapenzi ya mungu..

Mimi sio muumini wa hao uliowataja lakini ni Mkristo
Nalazimika kukuuliza yafuatayo

Ni kwanini unasema hayo ni maigizo?
Je unaujuzi wa hayo?
Kama ni ndio tuambie hapa

Pia tuambie unajua nini kuhusiana na misukule
Je una ufahamu wowote na hiyo kitu "maigizo"?

Isije kuwa ni wivu tu wa kukosa waumini huko uliko ndio umekuongoza kuleta haya!
 
Mimi sio muumini wa hao uliowataja lakini ni Mkristo
Nalazimika kukuuliza yafuatayo

Ni kwanini unasema hayo ni maigizo?
Je unaujuzi wa hayo?
Kama ni ndio tuambie hapa

Pia tuambie unajua nini kuhusiana na misukule
Je una ufahamu wowote na hiyo kitu "maigizo"?

Isije kuwa ni wivu tu wa kukosa waumini huko uliko ndio umekuongoza kuleta haya!

Wivu wanini? ulimbiwa kuwa hata mimi ni nabii?
 
Kwahiyo Gwajima ni mmoja kati ya wanafunzi wa Yesu waliopakwa mafuta?

Ndugu narudia tena mimi ni Mkatoliki lakini sipendi kupinga tu bila sababu.
Unakumbuka wanafunzi wa Yesu walikuta watu wasio miongoni mwao wakitoa mapepo na kuponya watu wakaenda kwa Yesu kulalamika kuwa kuna watu wasio miongoni mwao wanafanya miujiza kwa jina lake akawajibu "asiye kinyume chetu ni mmoja wetu"
tutawajua kwa matunda yao!! Zijaribuni roho zao na sio uzushi while unajua maandiko! Uzushi waachieni watu wa mataifa ndio maana binafsi sibishani na aliye kinyume na ukristo.
 
Kuna mtu alisema wanaombea wagonjwa na wanapona,sasa swali la kujiuliza kwanin wasiwe wanaenda hospital moja kwa moja? Na kama umate umate si watapewa na ndugu wa wagonjwa?

Hata Yesu hakutafuta wagonjwa bali wagojwa walimtafuta yeye.
uponyaji wa Yesu ni wa imani na imani inaanzia kwa mtu mwenyewe.
 
Si tii neon hapa...Ila Watanzania wanapenda mazengaombwe sana.

si watanzania tu hata Yesu alishalalamikia kizazi chake kwa kupenda miujiza.
Lakini kupitia miujiza imani nyingi zimejengeka.
Sisi Wakatoliki toka wale wana wa FATIMA watokewe na Bikira Maria imani ya kusali rozali iliongezeka mara dufu.
Lakini pia moja ya sifa ya mkatoliki aliyekwishafariki kuwa mtakatifu ni miujiza!!!
 
Hata Yesu hakutafuta wagonjwa bali wagojwa walimtafuta yeye.
uponyaji wa Yesu ni wa imani na imani inaanzia kwa mtu mwenyewe.

Kwa hiyo iyo misukule ndo inamtafuta huyo gwajima?
 
Wivu wanini? ulimbiwa kuwa hata mimi ni nabii?

Umeulizwa swari la msingi sana na Eiyer lakini unajibu porojo. Kama jambo huna ufahamu nalo lanini unalikurupukia? Wakristo wenyewe tena wenye imani juu ya Yesu hawana shaka na hili. Unabisha bila facts na bila kuwa na uwelewa wowote wa jambo husika. Kaa chini ufundishwe NENO kwanza.
 
Yesu alitoa mamraka juu ya wanafunzi wake ya kuponya na kuwatoa kwenye vifungo mbali mbali wale wanaoonewa na kuteswa na nguvu za giza. Hata wewe waweza kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo pale tu utakapoamini na kubatizwa na kukulia katika wokovu maana kila imani lazima ufundishwe baada ya kuamini[ lazima ufundishwe kwanza Yesu ni nani na alifanya nini na wanafunzi wake wakwanza walifanya nini ili kuijenga imani yako]
Mimi binafsi nimeshahudhuria mkutano wa Gwajima pale Relini Arusha mjini wiki mbili zilizopita. Anachofanya ni kuelezea vifo visababishwayo na nguvu za giza [pale wachwawi wanapoitaji damu, nyama au watu wakuwatumikisha katika kazi zao katika ulimwengu wa roho]. Jamani ulinzi wa Mungu [Yesu Kristo ni muhimu sana katika maisha yetu] maana hawa wachawi wakikutaka kama huna kinga yeyote either yakichawi kama wao [kupitia waganga au mizimu ya kwenu au ulinzi wa Yesu wenye nguvu kuliko ulinzi wowote ule] hawa jamaa wanauwezo wakukuchukua na ndugu zako wakajua umefariki kihalali kumbe hapana.
Kuna aina nne za misukule, watu wachukuliwavyo kwa njia za giza[ kwasasa sitaelezea] ukiona ndugu yako amefariki katika aina ya mojawapo za hizo basi jua kuwa kuna jambo wachawi wameshafanya hapo. Na hapo ndipo Nguvu za Yesu Kristo zinahitajika kumrudisha huyo mtu. Akasema yeyote yule mwenye imani kamilifu na Yesu anaweza kufanya yeye ayafanyayo. Kwani wangapi tulishasikia wameomba misukule ikarudi? Baada ya kutoa somo hilo ndipo anawashirikisha wote katika hayo maombi, wote mkiomba na sio peke yake na hata mimi nilishiriki na kuona miujiza ya Bwana Yesu Kristo wa Nadhareth aliye hai.
Kwahiyo kama ulifahamu Neno, biblia yenyewe husomi kwa msaada wa roho mtakatifu au imani yako haijajengwa kupitia Yesu wadhani utayajua haya? Jua kwanza Neno kisha uraise urguements zako kwa facts
 
Kuna mtu alisema wanaombea wagonjwa na wanapona,sasa swali la kujiuliza kwanin wasiwe wanaenda hospital moja kwa moja? Na kama umate umate si watapewa na ndugu wa wagonjwa?

Kweli,na nadhan hata Yesu angekuwepo angeenda Muhimbili.
 
Hata Yesu hakutafuta wagonjwa bali wagojwa walimtafuta yeye.
uponyaji wa Yesu ni wa imani na imani inaanzia kwa mtu mwenyewe.

Kuna kipind alienda kwenye birika la yakobo, ambapo walikuwa wanaka wagonjwa wakisubir uponyaji
 
shida kubwa ya watanzania wengi hawajui maandiko
napia hawamwamini mungu
wamekuwa wachunguzi;
wana roh ya tomazo:
neno la mungu limeweka wazi na ishara hizi zitaambatana na hao wamwamio yesu kwajina la yesu tutafufua wafu;
pia nitoe ufafanizi kidogo sii kweli ukifa nikweli umekufa wengine wanachukuliwa kichawi na kiroh wewe ujafa umeibwa tu
neno linasema watu hawa wamechukuliwa wako kwenye mashimo wala hapana asemae rudisha:
hivyo kazi ya mtu yeyote anaye mwamini kirsto amepewa mamlaka ya kurudisha mateka:
wacheni kucheza na kazi za mungu
soma 1wakorinto 13 soma yote biblia bana kila kitu kipo ila ni jinsi unavyokitafsiri... miujiza na karama zote vimeshakomeshwa..
 
Mkuu Mungi! binafsi nilishtuka sana nilipoona eti Gwajima afufua misukule zaidi ya 20 Arusha..
haya ni maigizo ya jukwaani kabisa na anayafanya bila uoga akidhani watanzania wote akili zetu zinafanana..

Sitaamini kamwe kwenye ufufuo wa aina hii..
Mungu naomba usinitoe katika imani niliyonayo,
inayonifunza katika kuyakabili maisha kwa njia ya halali! kutafuta kwa jasho..

Dah! mkuu watu8 huwa nakumbuka sana hoja yako uliowahi kuitoa sehemu juu ya kuwaamini watu kama kina Gwajima!

Hili la misukule mh! hapana kabisa!!

Mkuu kiwatengu ni kweli huyu Josephat Gwajima anaonekana msanii, maana hivi tunavyozungumza anafanya mikutano Moshi. Lakini cha ajabu Misukule wale wale waliofufuka Arusha wameanza kufufuka Moshi. Inamaana baada ya kufufuka Arusha walikufa, hivi sasa ndiyo wanafufuka tena Moshi.
Jamaa anatembea na misukule kwenye Hammer.
Wakristo tunatakiwa tujiulize, kama kweli alikuja kufufua ndugu zetu, je, baada ya kufufuliwa wameenda wapi?

Usanii huu unatisha
 
Last edited by a moderator:
Kuna kipind alienda kwenye birika la yakobo, ambapo walikuwa wanaka wagonjwa wakisubir uponyaji

Yes,wagonjwa waliokuwa wanasubiri uponyaji! Huwezi kusubiri uponyaji bila kuwa na imani! Huwezi kwenda muhimbili kwenye wodi na kuanza kuombea kila mtu kwa jina la Yesu while kuna hadi Mashekh mle!!

Lazima mtu mwenyewe awe ameamua ndio maana kwenye mahospitali huduma za kiroho hutolewa kwa wanaoamini na si kuanza kushusha tu maombi!!
 
Back
Top Bottom