Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara

Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara

Galla/isiolo huwa wanapatikana majike wakubwa amabao tayari kupandwa na kuzaa ni sh laki 2, madume ndio wana bei ni kuanzia laki 2 mpaka 5 inategemeana na ukubwa na umri wa Mbuzi, napo wakati wakununuwa unapashwa uangalie swala la umri ni muhimu sana hasa kwa Dume usije chukuwa mwenye umri mkubwa sana akashindwa kutumika vyema.
Asante sana
Je mna Instagram au YouTube?
 
Sisi ni TAGOFA chama cha wafugaji Mbuzi Tz na mletaji ni mwanachama , Mbuzi waliletwa kwa njia ya bara bara na hata ASAS last week kaleta Ngombe kutoka south kwa njia ya bara bara. Msafirishaji anashughulikia vibali vyote wewe unapokea Mbuzi mwenye nyaraka kamili, nawaomba ruhusa niweke number zao humu mtaweza wasiliana nao moja kwa moja.
Naomba namba zao mkuu. Au na mimi uniunge kwenye tagofa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nimeikuta FB
FB_IMG_1673775969869.jpg
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu. naomba niwapongezeni sana nyote ktk kujenga mawazo ya kutaka kuingia ktk miradi kama hii ya ufugaji. Mimi ni mfugaji wa Mbuzi na nina fuga Mbuzi kwa muda mrefu, niwaombeni kitu ufugaji ni mzuri na una faida na changamoto zake, kikubwa ni kukubali kujifunza na kujijengea umakini ktk ukaguzi na usimamizi wa mifugo yako. Kwa aliyepo Dar namkaribisha kwangu aje tujifunze pamoja na tugawene ujuzi kwa pamoja. Kwa anae anaza kufuga nakuomba sana usinunuwe mbegu kwanza kabla hujapita kwetu wafugaji tulio kutangulia ujifunze vitu halafu ndio uingize Mbegu shambani kwako. Karibuni kwa maswali mbali mba;li nipo hapa tutasaidiana kwa kadiri Mungu atakavyo tujaalia.
Ahsante kwa mawazo mazuri sana...
 
..Pure Boer bei yao ni kubwa sana kuweza kuwasafirisha toka Afrika Kusini.

..Kwa hapa Tanzania sio rahisi mfugaji kukuuzia mbuzi Boer Pure kwasababu wengi wako ktk stage ya kuwa-cross na kuwazalisha ktk miradi yao.

..Kuna wafugaji wakubwa kama Mbogo Ranches nilisikia kwamba wanaweza kuwasaidia wafugaji wadogo kuagiza mbuzi hao.

..Naamini njia nzuri ni watu kuwa ktk kikundi na kuagiza beberu ambaye atatumika ku-cross na mbuzi wa kienyeji.

..Jambo lingine la TAHADHARI ni kwamba beberu la Boer likiwa kubwa sana linaweza kumuumiza mbuzi wa kienyeji wakati wa kupanda.

..Pia mbuzi wa kienyeji anaweza kupata matatizo wakati wa kujifungua baada ya kupandwa na Boer.

..Kwa hiyo ni vizuri kuchagua beberu ambaye ni mdogo-mdogo ili aweze kuwapanda mbuzi wa kienyeji bila kusababisha ajali.

..pia ni vizuri kuwa makini ktk kuchagua majike wakubwa imara watakaoweza kuhimili mshindo wa beberu la Boer.
Ahsante Joka.Nimejifunza kitu kutoka kwako.Ubarikiwe!
 
Naomba niwasaideni kitu hapa kuagiza Mbuzi south Afrika hakuna urasimu wowowte mimi nazungumzia uzoefu na ninacho kifahamu, mwakajana mfugaji mwenzetu kaleta Red kalahar bila ya shaka na ktk umoja wetu wote walio agiza wamepata, shida ni moja kubwa hata kule south kunawapigaji sana. mnacho takiwa ni kufwata waagizaji wanaojuwa wazalishaji wa ukweli, hata ukienda uganda hata Mubende watakupiga tu ninaushahidi kwakweli. Mbogo Ranchese, Mavuno Farm, Biswalo, Usangu, ASAS. Hao ni waagizaji wa kweli na watakupatia kitu unacho hitaji, wakikuzulumu njoo Nyumbani kwangu nakulipa Mubende 1 bure kabisa.
Nakufata inbox ndugu,Nahitaji namba yako ya WhatsApp kwa ushauri zaidi kuhusu ufugaji wa Mbuzi.
 
Bei ya mbuzi Sokoni ipo vipi yaani The Highest na Lowest Price ?

Namaanisha haiwezi kutokea una mzigo watu hawanunui na wenyewe wanaendelea kula faida (chakula)?

Je demand ni mwaka mzima ? au Machinjioni wanachukua kwa bei gani ?
 
Naomba kufahamu kuna mbuzi nilionaga mahali ni weupee mwili mzima baadhi wana rangi nyeusi kichwani na wanamaumbo makubwa pia wanazaaa mapacha,hawa ni aina gani na wanapatikana sana maeneo gani??
 
Naomba kufahamu kuna mbuzi nilionaga mahali ni weupee mwili mzima baadhi wana rangi nyeusi kichwani na wanamaumbo makubwa pia wanazaaa mapacha,hawa ni aina gani na wanapatikana sana maeneo gani??
Kwakweli hapo ungetueleza ukanda ulipowaona hapo labda tungeweza kukusaidia ni aina gani wanapatikana ukanda huo, na picha ingesaidi kusoma hilo.
 
Back
Top Bottom