Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara

Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara

Mkuu nashukuru sana kwa mchanganuo huo
Najua hawaji rahisi ila kama nikipata hata wawili jike na dume mbona inawezekana na kupata baadae watoto wao

SA ni mbali ila kwa Uganda naona ni rahisi kidogo maana kuna malori yetu yapo huko
Ila ni plan yangu hiyo pia ntapata ushauri zaidi kwa wataalamu na wafugaji wakubwa kama hao
Kwenye sherehe za wakulima huwa wanaleta mbegu tofauti tofauti kama unawajua nijulishe mkuu

Naona una uzoefu na pia mfuatiliaji mzuri na kama unafuga pia naomba utupe experience zako na changamoto zao

Najua Boer kupanda mbuzi wetu ni changamoto sana ila kama nitapata hata x breed sawa

Chukulia kenya kama wapo Uganda wana ushuru mkubwa mno
 
Hapa linatakiwa eneo kubwa , alaf unaligawa hata vipande vinane vya ukubwa wa hekari mbili kila kimoja , unazungusha fensi nzito , supply ya maji iwe constant , ataishi kifalme Sana , na mbuzi atawakimbia , Ila hii ya kuwapeleka machungani na kurudi chenga tupu , mbuzi Wana visirani Sana kila mara mchungaji atakuwa anarudi amevunja mgongo mmoja

View attachment 2470846
Hata kama kuna ukweli lakini kauli yako ni ya kukatish tmaa
 
Mimi pia NAOMBA muongozo nipo Geita MWAKA wa tatu bado Kuna Elimu ninakosa hasa nimesikia ishu ya vitamins na chokaaa pamoja na jiwe ingawa mbegu nishaanza kufahamu je hiyo ya mbuzi kumpanda mama ake ikoje
 
Mkuu nashukuru sana kwa mchanganuo huo
Najua hawaji rahisi ila kama nikipata hata wawili jike na dume mbona inawezekana na kupata baadae watoto wao

SA ni mbali ila kwa Uganda naona ni rahisi kidogo maana kuna malori yetu yapo huko
Ila ni plan yangu hiyo pia ntapata ushauri zaidi kwa wataalamu na wafugaji wakubwa kama hao
Kwenye sherehe za wakulima huwa wanaleta mbegu tofauti tofauti kama unawajua nijulishe mkuu

Naona una uzoefu na pia mfuatiliaji mzuri na kama unafuga pia naomba utupe experience zako na changamoto zao

Najua Boer kupanda mbuzi wetu ni changamoto sana ila kama nitapata hata x breed sawa
Hivi najiuliza wizara ya Kilimo na mifugo wameshindwa kutuletea mbegu ya Boer ya sampo hata wakachukue mabeberu na majike 2000 wayalete na kuyapeleka pale SUA ili waanze kuyabreed na kutengeneza mbegu za kusambaza kwa wafugaji?!
 
Nimefuatilia sana na kuangalia insta na YouTube
Nimefanikiwa kuwaona baada ya mdau kunipa mwanya kidogo
Wapo na wanauzwa sasa kwenye ranch
Hata Dodoma wapo pia
Wengine hawauzi Boer bali wanakupa cross breed yao ila ni wakubwa pia

Kwa sasa nikihitaji ntawapata Tz
Nimehangaika sana kuuliza mpaka nikawaona YouTube
Unaweza kuangalia YouTube
Boer goats in Tanzania utawaona sehemu nyingi hata Dar pia

Ila ni kupata wafugaji bora na wataalamu na kufika mwenyewe kuwaona usije ukauziwa kwenye gunia
 
Nikweli ulicho kisema TALIRI MPWAPWA walikuwa wanafanya utafiti wa mbegu na walikuwa na Boer walimcross na hawa wakienyeji na walizalisha mbegu nzuri sana ila kumbuka kituo ni cha serekali hapo sasa kuna wakati waliporomoka vibaya sana. Walizalisha Mbuzi gogo white, blended, malia, hao wote walikuwa wazuri sana. Ukienda TALIRI TANGA wao wanafanya utafiti wa Mbuzi saa nene wale wa maziwa wakiwa cross na wakienyeji ili waweze kutoa maziwa bila shida kwenye ukanda wa pwani, sasa shida inakuja hapa ukihitaji kupata hizo mbegu ndio shida unalipia na kusubiria kwa miezi 3 mpaka 4 na siku ukienda kuchukuwa hawakuruhusu kuchagua unaletewa mbuzi basi wewe ni kumchukuwa hata akiwa mzee, kwa ujumla sasa TZ bado tupo nyuma tukiwategemea hawa vituo vya serekali nazungumza kwa uzoefu wangu.
 
Hivi wakilishwa chakula kizuri hakuna uwezekano wakaongezeka ukubwa na uzito na wasiwe na udumavu?
Hata siku moja hawaongezeki hawaongezeki kwasababu ya vinasaba vyao vya uasilia, wao hata ukiwa cross bado ukuwaji wao hauendi kama hawa wenye vinasaba ya miili mikubwa. Ninawafuga hao na ukuwaji wao ni tofauti kabisa na kama isiolo/Galla, au wengine wa kisasa.
 
Hivi najiuliza wizara ya Kilimo na mifugo wameshindwa kutuletea mbegu ya Boer ya sampo hata wakachukue mabeberu na majike 2000 wayalete na kuyapeleka pale SUA ili waanze kuyabreed na kutengeneza mbegu za kusambaza kwa wafugaji?!
Mkuu ni kweli walishawahi kuleta lakini shida iliyopo ni moja tu Mbegu zinaletwa ila usimamizi unakuwaje? tulikuwa na SKU Mbeya, sasa ukienda utalia kisa usiamamizi mbovu walio lianzisha walipotoka basi tulio baki tukalimaliza, ukienda hizo NARCO RANCHESE ndio balaa kabisa, sasa ili kujikomboa ndio maana tukajikusanya na kuanzisha TAGOFA na miunganiko kwaajili ya kujiletea mabadiliko ktk ufugaji, kuna baadhi ya wanachama wa TAGOFA sasa wanaleta hizo mbegu bora kabisa toka huko Afrika ya kusini na zina patikana hapa hapa nchini bila shida kabisa. Rejea post zangu zilizo pita nilitoa taarifa na mawasiliano ya jinsi ya kupata hizo mbegu bila shida.
 
Nikweli ulicho kisema TALIRI MPWAPWA walikuwa wanafanya utafiti wa mbegu na walikuwa na Boer walimcross na hawa wakienyeji na walizalisha mbegu nzuri sana ila kumbuka kituo ni cha serekali hapo sasa kuna wakati waliporomoka vibaya sana. Walizalisha Mbuzi gogo white, blended, malia, hao wote walikuwa wazuri sana. Ukienda TALIRI TANGA wao wanafanya utafiti wa Mbuzi saa nene wale wa maziwa wakiwa cross na wakienyeji ili waweze kutoa maziwa bila shida kwenye ukanda wa pwani, sasa shida inakuja hapa ukihitaji kupata hizo mbegu ndio shida unalipia na kusubiria kwa miezi 3 mpaka 4 na siku ukienda kuchukuwa hawakuruhusu kuchagua unaletewa mbuzi basi wewe ni kumchukuwa hata akiwa mzee, kwa ujumla sasa TZ bado tupo nyuma tukiwategemea hawa vituo vya serekali nazungumza kwa uzoefu wangu.

Mambo ya hovyo kabisa yani ulipie wakucheleweshe kisha siku ya kuchukua mbuzi wanakupa yeyote?
 
Mambo ya hovyo kabisa yani ulipie wakucheleweshe kisha siku ya kuchukua mbuzi wanakupa yeyote?
Ndio hivyo wanavyo fanya, ukiwapigia watakupokea vizuri nakukupatia number fasta ya kulipia ngoma inakuja kupata huyo mfugo sasa duh!
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu. naomba niwapongezeni sana nyote ktk kujenga mawazo ya kutaka kuingia ktk miradi kama hii ya ufugaji. Mimi ni mfugaji wa Mbuzi na nina fuga Mbuzi kwa muda mrefu, niwaombeni kitu ufugaji ni mzuri na una faida na changamoto zake, kikubwa ni kukubali kujifunza na kujijengea umakini ktk ukaguzi na usimamizi wa mifugo yako. Kwa aliyepo Dar namkaribisha kwangu aje tujifunze pamoja na tugawene ujuzi kwa pamoja. Kwa anae anaza kufuga nakuomba sana usinunuwe mbegu kwanza kabla hujapita kwetu wafugaji tulio kutangulia ujifunze vitu halafu ndio uingize Mbegu shambani kwako. Karibuni kwa maswali mbali mba;li nipo hapa tutasaidiana kwa kadiri Mungu atakavyo tujaalia.
Dar upo sehemu gani mkuu?
 
Mungu akubariki na kukujaalia ufikie malengo yako, nikushauri pia ujaribu kupita kwa wafugaji kila mara ili uweze kujifunza kwa vitendo hii itakusaidia sana ktk utendaji wako, maana kila ulianzishalo linahitaji usimamizi wa karibu ndio utaiona nakujua faida yake.
Hata mimi ndani ya mwaka huo nina mipango kama yako.
 
Bongo makanjanja wengi mkuu ila ukienda Kenya, Uganda na SA utaona watu wanavyofuga kwa umakini

Kuna mbegu inaitwa Boer hawa mbuzi wanafika mpaka 100kg ila ukiuliza waswahili wanakuambia yes wapo mzee

Jichanganye sasa haha
Natamani kuwaleta toka UG kwa jamaa mmoja alitokea [emoji631] na anafuga pure breed View attachment 2472133
Mkuu uliwapata?
Kama bado nikuunganishe na jamaa yupo hapa Masaka anao wengi tu.
 
Ushauri wangu jitahidi baba asipande mwanae yaani uchanganye damu usirudie uzao ukapanda uzao unaofuta utapata wanyama bora sana. Japo sio lazima ni wewe na uwezo wako
Je ? Wakipandana uzao wa pili?
 
MUBENDE na wadau wote habarini??

Nimesoma uzi wote sijaona mahali palipozungumzia kuwa mbuzi toka anazaliwa mpaka kufikia kuwa mkubwa na mzuri wa kuliwa ni muda gani?? Natamani nijue hasa hawa wetu wa kienyeji!!
 
..kwa mbuzi wa kienyeji inaweza kuchukua mwaka mmoja, mpaka mmoja na nusu.

..mbuzi wa kisasi pure breed, au mbuzi chotara, inaweza kuchukua miezi sita mpaka miezi minane.
 
Back
Top Bottom