Habari za leo kwanza naomba utambue kila mlaji ana uchaguzi wake wa Mbuzi saizi gani anamfaa kwa matumizi yake aliyoyapangilia. Mbuzi akisha fikisha umri wa miezi 4 kwenda mbele huyo anaweza kufaa kwa matumizi ya kuliwa, kuhusu hawa Mbuzi wetu wa kienyeji ukuwaji wao ni watatratibu sana na ndio maana kwa sasa tunashauriwa sana kuanza kuchanganya mbegu na hawa Mbuzi wa kutoka mataifa ya nnje. Mfano Isiolo/Galla. Boer,Red kalahare, Savanaha, nk.
Kwa majike tunashauri sana utumie wenye maumbo makubwa, Mubende hawa wanapatikana Karagwe,Biharamulo,Bukoba na Uganda. Buha hawa wanapatikana Kigoma zaidi. Na pia ukipata Mbuzi wanaopatikana ukanda wa usukumani, na kwenye mashamba ya uzalishaji wa Mbuzi Taliri,Mpwapwa,Tanga nas kwengineko. Huko utapata Blended, Gogo white,Newala nk. Karibu sana ktk ufugaji wa Mbuzi.