Nawasalimuni kwa jina la Mungu. naomba niwapongezeni sana nyote ktk kujenga mawazo ya kutaka kuingia ktk miradi kama hii ya ufugaji. Mimi ni mfugaji wa Mbuzi na nina fuga Mbuzi kwa muda mrefu, niwaombeni kitu ufugaji ni mzuri na una faida na changamoto zake, kikubwa ni kukubali kujifunza na kujijengea umakini ktk ukaguzi na usimamizi wa mifugo yako. Kwa aliyepo Dar namkaribisha kwangu aje tujifunze pamoja na tugawene ujuzi kwa pamoja. Kwa anae anaza kufuga nakuomba sana usinunuwe mbegu kwanza kabla hujapita kwetu wafugaji tulio kutangulia ujifunze vitu halafu ndio uingize Mbegu shambani kwako. Karibuni kwa maswali mbali mba;li nipo hapa tutasaidiana kwa kadiri Mungu atakavyo tujaalia.