MUBENDE
JF-Expert Member
- Nov 11, 2022
- 1,111
- 1,879
Kwanza naomba nikupongeze sana kw hilo la kuthubitu ktk ufugaji huu. Sasa naomba nikushauri kitu, kwanza kabisa kabla huja nunua Mbegu naomba ujitahidi upate nafasi upite kwenye masahmba ya wafugaji ambao tumeshaanza iliuweze kupata ABC za ufugaji wa Mbuzi. hii itakusaidia sana kuweza kujua hizo mbegu juu ya uangalizi wake na jinsi ya kuzihudumia kuanzia usafi,upandishaji matunzo baada ya kuzaa na jinsi ya kupishanisha baba asimpande mtoto au ndugu wasipandane.Nimepata eneo la kama heka 12 nataka kufuga mbuzi. Mpango ni kulizungushia uzio nipande nyasi na miti spesho kwa malisho ya mbuzi, so naomba mwenye ujuzi anielekeze nyasi na miti sahihi ya kupanda humo ili wawe wanajilisha. Ila naomba kujua Boar Goats madume kwa hapa Tz wanapatikana wapi na bei yao ili niwapandishe kwa majike ya kienyeji.
Pia nakusahuri wakati wa kunua Mbegu usiagize ufike kwa wahusika ili uweze kuchaguwa na kuangalia kwa kina kile unachokihitaji hasa hapo umegusia kuhusu Boer kum cross na jike wa local hapo kuna mtihani wakujua ubora wa jike kwaajili ya kumjumlisha na hao madume wa kubwa. Nakushuri uingie ktk page Ya Mbogo Ranches' kuna semina wanaendesha kwaajili ya ufugaji itakusaidia sana. Kuhusu Mbegu nakushauri uwasiliane na Mbogo ranches, Mavuno ranches, ASAS Afrifarmtz hapo utapata hitaji lako bila shaka, cross wapo hata kwa wafugaji wenzako wapo nao pia ukihitaji unapata bila ya shaka.
Nakuombea kila la kheri ktk wazo lako Mungu akubariki sana na kukujaalia kila yaliyo mema ktk ufugaji huu. Karibu sana kwangu msaada wa kwanz akama upo Dar karibu Kibamba kwa Mangi ujie tujifunze pamoja na tufuge pamoja bure gharama yako ni nauli tu ya kufika ghapo, Barikiwa sana.