Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara

Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara

Nawasalimuni kwa jina la Mungu. naomba niwapongezeni sana nyote ktk kujenga mawazo ya kutaka kuingia ktk miradi kama hii ya ufugaji. Mimi ni mfugaji wa Mbuzi na nina fuga Mbuzi kwa muda mrefu, niwaombeni kitu ufugaji ni mzuri na una faida na changamoto zake, kikubwa ni kukubali kujifunza na kujijengea umakini ktk ukaguzi na usimamizi wa mifugo yako. Kwa aliyepo Dar namkaribisha kwangu aje tujifunze pamoja na tugawene ujuzi kwa pamoja. Kwa anae anaza kufuga nakuomba sana usinunuwe mbegu kwanza kabla hujapita kwetu wafugaji tulio kutangulia ujifunze vitu halafu ndio uingize Mbegu shambani kwako. Karibuni kwa maswali mbali mba;li nipo hapa tutasaidiana kwa kadiri Mungu atakavyo tujaalia.
Kwako wapi nije
 
Mje niwauzie mbegu za nyasi aina ya Juncao na Super napier kg 5000,yanafaa kulisha ng'ombe wa maziwa,nyama,mbuzi ,kondoo na mazuri pia kwa unenepeshaji.0756625286.
Yanakua kwa haraka,yana protein 17%.
View attachment 2819858View attachment 2819859
IMG_20230828_075622_953.jpg
 
Kwenye huu uzi ngoja ni sign in alafu nipite page kwa page kwa umakini ili nipate madini
 
Pole sana ndugu kwa hii chanagamoto naomba nikushauri kitu, ktk ufugaji wako unapotafuta Mbegu ya mapacha uwe unajuitahidi kutafuta na kuona kabisa Mbuzi mwenye watoto mapacha na kama ikiwezekana akuuzie na watoto wake kabisa itakusaidia kuwa na uhakika ktk hilo hitaji lako. Mimi huwa naitumia hiyo njia ktk kujihakikisha kama namhitaji huyo Mfugo, ila kwangu mimi kipaumbele ni Mbuzi kuzaa sio lazima mapacha ikitokea namshukuru Mungu nasonga, kipaumbele ni kuwa na majike bora yenye kunipatia matokeo bora, Barikiwa sana ktk ufugaji huu.
Ahsante. Umeiweka vizuri sana
 
Hivi

Hivi changamoto ya wizi wa mbuzi mnakabiliana nayo vipi? Hasa wamasai na mang'ati kwa mashamba ambayo yako nje ya mji?
habari za leo kusema ukweli hasa la wamangati ni changamoto kubwa sana maana hao jamaa bana wanambinu nyingi sana za uwizi na kununuwa viongozi wa vijiji kwamaana hata muwashtaki vipi hamna anae wagusa. wamasai sio waizi na ndio nawatumia mimi kwenye ufugaji shida yao ni kutaka kufuga kwa kieneyeji kama walivyo zoea kwao. Mimi wameshanifanya nikaliacha Shamba kongowe ya Mlandizi na mabanda yakaanguka ndani. Wamangati ni wabaya sana kuliko unavyo fikiria.
 
Nimepata eneo la kama heka 12 nataka kufuga mbuzi. Mpango ni kulizungushia uzio nipande nyasi na miti spesho kwa malisho ya mbuzi, so naomba mwenye ujuzi anielekeze nyasi na miti sahihi ya kupanda humo ili wawe wanajilisha. Ila naomba kujua Boar Goats madume kwa hapa Tz wanapatikana wapi na bei yao ili niwapandishe kwa majike ya kienyeji.
 
Hongera sana mkuu, hii ndio nataka kuifanya
Kwa pure Boer ni ghali ila wapo UG na tz wanacross wengi wao kwa hiyo utapata mix
Boer bei imechangamka na wapo Kalahari pia

Ukosikia mtu anauza bora uende mwenyewe kwa gharama zako hata kama ni maili 200 ukajionee mazingara yao
Muhimu zaidi certification zote maana kama Kenya na Uganda unaonyeshwa kila kitu waliponununuliwa mpaka makuzi yao na dawa wanazopewa nk
Uwe makini sana kuhusu majani yapo mengi hata kwenye insta wamejaa wafugaji na mbuzi pia utapata idea nyingi na humu pia wapo watu wema ila usiamini sana mpaka umeridhika na kila kitu
 
Shukrani kwa ushauri mkuu, ngoja niendelee kujifunza.
 
Back
Top Bottom