Habari wana Jf.Niliwahi kuwaletea uzi wa ufugaji wa mbuzi wa kienyeji ,namshukuru Mungu nilifanikiwa kuongeza mradi wa Mbuzi shambani kwangu, mdogo mdogo napambana!.Binafsi wanyama ni maisha yangu,nawapenda sana na ndiyo Kigezo cha mimi kujikita kwenye miradi ya ufugaji.Tuachane na hayo!
Lengo la uzi huu,nahitaji kufungua Zoo ya Wanyama pori kwa ajiri ya utalii.Nahitaji kuanza na Wanyama wachache kama vile Kobe,nyoka,swala,ndege na nitaongeza wanyama kadri biashara yangu itakavyokuwa ikikuwa.Nahitaji ushauri kutoka kwa yeyote mwenye uzoefu na biashara hii ya Zoo au Bustani ya wanyama pori.Je, napaswa kuwa na mtaji kiasi gani kama kianzio?(gharama za leseni),nizingatie mambo muhimu yapi ili mradi wangu uwe wa mafanikio?Nina eneo la ekari moja mali binafsi kwa ajili ya Kuanzia mradi,liko nje ya mji.Ahsanteni kwa kusoma uzi wangu.