Ufugaji na kilimo unalipa sana

Ni kweli changamoto ni urundikaji , chakula na malazi bora. Wengi hawawapi virutubisho zaidi ya majani ya kawaida tu, pia wengi wanawalaza chini pamoja na vinyesi vyao: magonjwa ya miguu. Ukiwapa mikunde unapunguza sana utumiaji wa concentrates za nafaka ila unashauriwa isizidi 30% ya chakula chao. Mwanzo niliitafuta sana kumbe imejaa tele hasa leucaena wanayoiita 'the alfalfa of Tanzania' mbegu unazoa tu na zinaota. Mkalianda wenye maua wanauita mti Xmas wa Dar, mlonge pia mbegu zake zipo na huu hata ukizidi 30% ni salama tu kwa wanyama wote. Mimi sina eneo kubwa nitawajaza tu na nikipata mapori yasiyolimwa nawatoa kuwalisha. Kikubwa ni invest kwenye malazi. Soko gawa hiyo idadi kwa mwezi na uanze kuulizia mapema. Pia ungepata mfano wa eneo la depot Dar ingekusaidia kuepuka pressure ya kuuza bei ndogo vingunguti kwa kuogopa gharama ya kukodi malazi yao.
 

Nakubaliana nawe, ukiwekeza kwenye kilimo & ufugaji kwa umakini kuna faida. Hongera sn mkuu.....
 

Kaka, heka mia mbona ni tone la mvua mkuu, Kwa hakika ardhi bado bure hapa Bongo, mimi nilinunua ekari60 kwa chini ya laki nne, nikaongeza sasa ninazo mia mbili kama na sabini, haijazidi millioni tano!!! Jamaa naona alinunua millioni 10 eka mia, bado cheap. Kama uko serious unataka maeneo wewe tangaza hapa uone watu wanakuelekeza pa kuyapata. KAMATENI MAENEO KABLA WAWEKEZAJI HAWAJAYAGAWANA! Mimi nna project naitaka sana, bado najikusanya na mtaji, nitahitaji eka kama laki moja sehem yenye mto, nahangaikia kianzio tu, IGEMBE SABHO!
 
Huku ndo kwa kushinda na kupata maujuzi. Sio kila siku lema,kinana,mbowe zitto,

Ha ha ha ha ha haaaaa.......
Umenifurahisha kaka na hizo sentensi zako mbili hapo juu. Nyie mnawajadili (hao ulowataja), wenzenu wanaingiza kipato!!!
 

kaka ktk red,hili ni jambo la msingi sana,mimi nimenunua kilosa eka 10 kwa milioni 3 nadhani bei inatofautian kulingana na meneo
 


naomba nijue hapo shambani kwako chanzo kikuu cha maji ni nini?
kuna mto wa mwaka mzima?
umechimba kisima?
gharama ya kisima huko ikoje?
ni umbali gani kutoka moro mjini...
 
naomba nijue hapo shambani kwako chanzo kikuu cha maji ni nini?
kuna mto wa mwaka mzima?
umechimba kisima?
gharama ya kisima huko ikoje?
ni umbali gani kutoka moro mjini...
Tumeweka mifumo ya kuvuna maji ya kutosha.
Ni km30 kutoka morogoro,ni karibu na mikese
 
Mkuu kwanini usitenge eneo kidogo kwa ajili ya kufuga samaki?
 

Uko wapi tuje kuona darase
 
Hongera mkuu, sasa uweke na mabwawa ya kufugia samaki utapenda sana
Ahsante mkuu.na explore hiyo project.nimekuwa na study humu kuhusu ufugaji samaki!vp una ujuzi kuhusu hili
 

Mkuu hongera sana kwa kweli,ni ukweli usiofichika ukidhamiria kwa dhati kuwekeza kwenye kilimo na ufugaji lazima utakuja fanikiwa tu!kikubwa ni uvumilivu na dhamira,maana mwanzoni changamoto ni nyingi!kwa uzoefu wako mkuu kwa Morogoro ukilima mahindi kitaalamu kipindi cha masika,je katika uvunaji unaweza pata gunia ngapi minimum kwa heka moja?ahsante!
 
Gunia 25 utakuwa umepata sana
 

Mkuu hebu tujikite hapo kwenye tikiti maji kwanza.

Kilimo chake ni cha miezi mingapi na mmea mmoja unatoa matunda mangapi yenye uzito gani??

Vipi gharama za kilimo na ugumu wake kwa maana ya magonjwa na athari za mifumo ya hali ya hewa??
 
Gunia 25 utakuwa umepata sana

Asante mkuu,unajua mwenyewe nimepata eneo kama heka tano mkoani Morogoro,ila ni shamba jipya (halijawahi kulimwa) nilikua na plan kwa masika hii nipande mahindi heka zote tano,ila kuna watu wananiambia kua mahindi kwa shamba jipya unaweza usipate hata gunia 7 kwa msimu wa kwanza,ukweli walinikatisha tamaha ndio maana nikaona nipate uzoefu wako!
 
Nadhani inategemea na sehemu.pia wenyeji wa morogoro generally ni wavivu.pia kwangu niliambiwa mengi.ni vema ku study hali ya hewa na kujaribu kidogo.kama eka 1 hv .kwa kawaida shamba jipya ndo linaleta mavuno mengi
 
Watu wa morogoro generally ni wavivu na hawajui.nilisikia mengi shambani kwangu pia.kwa kawaida shamba jipya linatakiwa likupe mazao mengi zaidi.
Unahitaji ku study hali ya hewa na kujaribu kidogo,eka moja say!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…