Ni kweli changamoto ni urundikaji , chakula na malazi bora. Wengi hawawapi virutubisho zaidi ya majani ya kawaida tu, pia wengi wanawalaza chini pamoja na vinyesi vyao: magonjwa ya miguu. Ukiwapa mikunde unapunguza sana utumiaji wa concentrates za nafaka ila unashauriwa isizidi 30% ya chakula chao. Mwanzo niliitafuta sana kumbe imejaa tele hasa leucaena wanayoiita 'the alfalfa of Tanzania' mbegu unazoa tu na zinaota. Mkalianda wenye maua wanauita mti Xmas wa Dar, mlonge pia mbegu zake zipo na huu hata ukizidi 30% ni salama tu kwa wanyama wote. Mimi sina eneo kubwa nitawajaza tu na nikipata mapori yasiyolimwa nawatoa kuwalisha. Kikubwa ni invest kwenye malazi. Soko gawa hiyo idadi kwa mwezi na uanze kuulizia mapema. Pia ungepata mfano wa eneo la depot Dar ingekusaidia kuepuka pressure ya kuuza bei ndogo vingunguti kwa kuogopa gharama ya kukodi malazi yao.
Safi sana Mama Joe naona unagusa angle ninazozitaka tupu.
Naona changamoto kubwa ya kufuga mbuzi ni urundikaji wa mbuzi(population density) kwa eneo na ugonjwa unaotesa hasa ni minyoo,
Nakuja na wazo kuwa kama nitawalimia majani na nikatenga eneo maalumu kwa ajili ya kuwalimia virutubisho na ulaji wao ukawa ni wa kuwakatia majani naona ninaweza kuweka mbuzi hata 50 kwa hekari na nikawawekea na eneo la kucheza cheza
Hio mimea uliyoiongelea kama mlonge longe na calliandra kuna bwana mifugo kanitonya hapa kama uatweza kuwalisha mbuzi kama suppliments inawafanya mbuzi waongezeke uwezo wao wa kukua kwa siku kutoka gramu 900 kwa siku mpaka 1200 kwa siku kwa sababu ya high content ya protein, maana yake ni kuwa mbuzi badala ya kukua kwa miezi 6 yeye atakua kwa miezi 4 tu. Hii ni habari njema sana.
Changamoto bado naiona katika masoko. Kama ninatweza kuzalisha mbuzi 30,000 kwa mwaka niaweza kuwaingiza woote sokoni ndani ya mwaka mmoja hata kama ni kwa bei ya jumla ya tsh 60,000 maana nawalisha kwa kuwalimia majani na kuchelewa kwao kuingia sokoni ni hasara sana.