Heri ya mwaka mpya! za siku nzuri, hongera kwa shamba kubwa, rufiji kweli kuzuri na lile mto duh mamba tuu hahaaa. Kuhusu mbuzi ninavyoelewa inashauriwa wawe na nafasi ya kuwa huru kufanya mazoezi kucheza wale wadogo nk. Pamoja na hayo ukubwa wa eneo la kulishia inategemea kilichomo ktk eneo kama ni majani tu ya kawaida yasiyo na virutubisho vya protein au umeotesha na mikunde au unawapa supplements za nafaka na za viwandani. Eka moja kwa kwa mwaka mzima inatosha mbuzi 15 maximum kama wanakula hapo tu hawapewi majani mengine wala kupelekwa kula nje. Utaona kuwa kama unawaletea chakula kwa kukata majani sehemu nyingine na kuwalisha basi eneo linalohitajika ni dogo zaidi mradi tu iwepo nafasi kwa wao kucheza na kufanya mazoezi. Kingine kinachoamua kuhusu nafasi ni minyoo na wadudu wa magonjwa, iwapo unawalisha eneo moja miaka yote jiandae kuwatibu minyoo na magonjwa, lakini ukiwa zungusha na kuwahamisha eneo likakaa hata mwaka bila kutumika na wao utapunguza uambukizo kwani minyoo itakufa na majani yatakuwa yameota vizuri. Kuhusu hii ya magonjwa inaweza fupishwa muda kwa kuwaweka kuku nyuma ya eneo walilokuwa mbuzi ili watakula wale vijidudu na kusafisha eneo wakati majani yakiota. Kifupi ni wewe mwenyewe kuangalia enao lako ukijaza mbuzi likawa kipara ktk muda mfupi basi itabidi uhamie eneo jingine ili nyasi ziote na kwa afya zao utajitahidi walau kwa mwaka kulipumzisha eneo ili vijidudu sugu vife. waweza tenganisha eneo moja toka eneo jingine kwa kupanda miti ya mikunde kama leucaena, moringa/mlonge na colliandra (sp) kama fence ambayo watakuwa wakiila pamoja na majani. Kwa iyo idadi kwa kweli ni mtu mwenyewe utakavyoweza kuchagua mfumo gani unatumia huria au. Kuhusu soko ni kama mdau aliyeleta uzi wa kuuza mbuzi bei yake ni 75 - 80 elfu kwa Dar na soko lipo tu maana licha ya groceries, bar, hotel hata bucha zote zinauza mbuzi na wenye kumbi za sherehe kwa ajili ya ndafu. Kwa muda mrefu tulikuwa tumezoea kuvizia safari za aidha Dodoma au Arusha au Moshi karibu na Xmas ili tununue mbuzi waliochinjwa mnadani (Dodoma) au barabarani Korogwe, nafikiri ukiwa mbunifu waweza kamata soko njia yako ukawauzia watu wanaopita kurudi Dar wakiwa wazima au waliochinjwa. Kuna mdau ameshauari kwa mbuzi walio wengi waweza tafuta soko hadi nje, kwaiyo kama unafikiria kufuga wengi hili nalo la kulipa kipaumbele.