Ufugaji ni Utajiri, kilimo ni mali

Nmekuelewa mkuu..ulichukua madume mangapi! !
 
mkuu uko vizuri, binafsi nimekuelewa na nimejifunza kitu. malengo ya muda mrefu ni kitu cha msingi sana, watu huwa wanatamani kukamilisha vitu kwa muda mfupi tu.

next time, usipende hitimisho la kudhani unachofanya wewe tu ndo fursa pekee kuliko vingine, heading ya post yako tu umeanza kwa kuponda ufugaji wa kuku na nguruwe. kuna watu wametajirika kupitia huko. sema wewe hujaona huko kama kuna fursa, tunatofautiana miono, kuna mwingine wewe unakodhani ndo fursa usimwambie hata kidogo.

by the way! hongera sana na Bwana akubariki.
 
acha mihemuko, toa somo unafugaje hao ng'ombe
 
 
The unseen opportunities are seen by

I don't see anything out of my Shillings. My way, my plan
 
Karibu wadau tujifunze namna ya kufuga ng'ombe kwa faida.
 
Copied and Pasted

Usione watu waliofanikiwa wanakaa zao kimya na siri zao za mafanikio, wakiendelea kula maisha. Uhalisia ni kwamba kuwasaidia watu wengine kufanikiwa ama kuwaonesha njia ya mafanikio inahitaji wito kamili na moyo wa chuma! [HASHTAG]#SmartMind[/HASHTAG]
 
Subiri mpaka uvune usianze mbwembwe mapema teh teh
 
Subiri mpaka uvune usianze mbwembwe mapema teh teh

Siyo Mbwembwe. ni uhalisia. Majanga yapo. hatutegemei yatufike. yakikufika siyo mwisho. Endelea Endelea Endelea na fanya zaidi kwa sababu hiyo ndiyo maana ya Maisha
Maisha hayafiki mwisho pale majanga yanapotupata. ila huwa ni mwanzo mzuri wa kuboresha cha zamani na kutengeneza kitu kizuri zaidi ili kishindane zaidi na changamoto izo.
 

HONDA XL. Comment Nzuri.
 
HONDA XL
UMESEMA VYEMA.
Najua ufugaji w kuku na nguruwe na uwekezaji mwingine unalipa. Nimewahi kutembelea mradi mmoja wa nguruwe upo tabora, njia ya kuelekea Urambo kulia kwako kabla hujafika Tumbi. Nilijifunza mengi sana kuhusu ufugaji wa nguruwe. ni uwekezaji mkubwa sana wa Shamba la Nguruwe. Na inamlipa sana huyo bwana. kwa wale wanaotaka kijifunza wanaweza kufika apo uyo bwana anapenda sana vijana wajasiliamali wajifunze pale. ana mabwawa ya samaki pia. Mwaka 2014 alikuwa na changamoto kwa ufugaji wa samaki. Lakini pia Mwaka huo wa 2014. nilibahatika kutembelea mradi mkubwa wa kuku wa kienyeji. unamilikiwa na mzee mmoja bi Auditor yupo pale Tabora. Ni mradi ambao pia umefaulu sana. yupo karibu na Hospital ya kitete Mita kama mia 600 kutoka hospital ya Kitete. Alikuwa na mpango w kununua shamba ili apanue zaidi Mradi wake. Kuna vitu nilijifunza sana kwa hao Mabwana. how they started and Sustainable projects. Sikuopt iyo fursa nimeopt fursa nyingine kwa sababu nimetumia muda pia kuwa na uelewa wa hii Miradi.
Mungu Awabariki Wapendwa
 
NARUDIA TENA
VIJANA UFUGAJI SIYO KUKU NA NGURUWE TU.
TUAMKE
TANZANIA NI NCHI NZURI NA RAFIKI KWA VIJANA WOTE
 
Mkuu hapo mahali kwenye nguruwe Tabora napajua,ni kati ya sehemu zilizonihamasha kufanya ufugaji wa Nguruwe,
 
Mkuu hapo mahali kwenye nguruwe Tabora napajua,ni kati ya sehemu zilizonihamasha kufanya ufugaji wa Nguruwe,
Hiyo ni njema Sana. Ona na Shinda
 

Hoja nzuri inahitaji kupanuliwa kidogo.Wakulima wanalima mwaka hadi mwaka hawasogei mbele si hoja ya ukweli sana ,ungesema wakulima walio wengi.Wapo wakulima wachache wamepiga hatua kubwa za maendeleo.Tafakari pia mbona kuna watu wameajiriwa na wanafanya kazi zaidi ya miaka 30 ajira zao zinapokoma huishi kwa shida isiyo na kifani wapo pia wafanya biashara nimewakuta wakifanya biashara tangu nikiwa mtoto.Hadi leo nimekuwa mzee aina ya biashara na ukubwa wa biashara zao havijabadilika.Kutunza kiwango chako cha mafanikio ni tija japo ni bora ikiwa kubwa na bora zaidi.Waajiriwa wengi wanajua kukosoa wengine lakini hishia vibaya mno kiasi cha kuwashawishi wanaofuata nyuma yao kudhani suluhisho ni kuiba ili wafanikiwe haraka.

Mtoa mada katoa mchango wenye tija kuacha mtindo wa mazoea na kutegemea mafanikio makubwa.
 
Habari za Jumapili Jamii. Kama kuna mtu ana kitabu cha ' THE RICHEST MAN IN BABYLON" BY GEORGE S. CLASON asaidie kukiattach apa. kina ujumbe ambayo natamani mtu yeyote ambaye hajakisoma akisome. ni kitabu maarufu sana.
 
Ulianza na 29mil. Duuuuuuuuuu
Ulianza na 29mil. Duuuuuuuuuu

Tunza kidogo unachopata wekeza kwa mafanikio. wakati naanza zoezi la kutunza pesa ilikuwa ngumu kwa sababu nilikuwa mtu wa starehe na Marafiki wengi. Niliweka malengo. kwa mwezi nitunze kiasi gani. ? kwa mwaka itakuwa wapi? Miaka miwili itakuwa wapi? Miaka mitano itakuwa wapi? Nina furaha nimeweza kufanya ivyo. mwanzoni sikuweza.

Sina mke. mtihani mugumu kabisa ni pale nilipokosa pesa ya mahari na mke mtarajiwa akijua nina pesa ya mahari na harusi. aliamua kuolewa na mwingine akijua sina mpango naye. Ni kosa langu. nilimtakia maisha mema.

Fikia ndoto zako kwa kutunza pesa kwa muda mrefu. kwa sababu nilikuwa na pesa fursa nyingi sana za maisha zilikuja. Nyumba inauzwa. unaona una pesa ya kununua lakini sikuwa na iyo plan. na kununua iyo nyumba maana yake ni kwamba malengo yako mazuri yanaishia apo. kiwanja kinauzwa bei poa. sikuweza kununua. Bado nimepanga. natumia gari ya ofisi. Baada ya uwekezaji huu sasa naweza kufanya yote hayo. na hakuna chichote kimebadilika kwa sababu sikununua nyumba ile au kiwanja kile.
Mbarikiwe wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…