Ufugaji nyuki wa kisasa

Wakuu,
Ningependa kufahamu yafuatayo,

1. Je! ni kweli upo utaalamu wa kuzalisha makundi ya nyuki na kuwahamishia kwenye mizinga?

2. Zoezi hilo huchukua muda gani hadi kuzalisha malikia mpya na kundi jipya?

3. Humu yupo mtu anayefanya hiyo kazi anayeweza kutoa ushuhuda au kuonesha practice?
3. Mfumo huo una ufanisi kiasi gani na changamoto zinazotegemewa ni zipi?

nawasilisha.
 
Habari Mkuu, Pole sana kwa kasumba ya kupoteza nyuki wako mara mara...

Kwa kawaida Nyuki wa asali hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ya kuambukizwa ambayo husababishwa na bakteria, fangasi, protozoan, virusi na mara chache hushambuliwa na predator na sumu...

Pia magonjwa haya huenezwa kutoka kundi moja kwenda lingine kwa nyuki wakubwa, kwa kutumia mzinga ulio na vimelea, waangalizi wa mizinga, vifaa vinavyotumika katika kulina asali, na pia nta kutoka katika mimea ambapo nyuki hufuata nta kwa ajili ya kutengenezea asali...

Magonjwa ni mengi mno, kwa maelezo siwezi kusema moja kwa moja ni ugonjwa gani unaowasibu nyuki wako hadi kupelekea wao kufa kwa wingi hivyo. Ingawa kwenye industry yetu hii tunapoona vifo vya ghafla na kwa wingi zaidi huwa moja kwa moja huwa ugonjwa husika husababishwa na virusi...

Hivyo, ningependa kujua unafugia katika mazingira gani? upo peke yako au umepakana na mashamba husika?

Pia, vifo hivyo ni kwa nyuki wakubwa tu au hadi wale nyuki watoto ambao hupatikana katika masega?

Na hali husika katika masega yapoje? hapa nataka kujua rangi ya sega la nyuki lina rangi gani? au kuna mabadiliko yoyote ya rangi?

Nataka kujua hayo ili kuweza ku narrow diagnosis mkuu..

Ahsante...
 
Je na ninyi mnauza mizinga tayari imiwa na nyuki?
 
Mzinga mmoja elfu 70??


Daah we jamaa umetisha
 

1. Wamekufa kwenye mizinga kadhaa kwa ndani ya mwezi mmoja hivi.

2. watoto kwenye masega nao pia wamekufa, sasa sijajua labda ni baada ya nyuki wakubwa kufa kwa hiyo na watoto wakafa kwa kukosa huduma au laaa,

3. kuhusu madawa kwenye mazo bado nafanya utafiti ila sidhani,

4. Kuna kundi lilikuwa kubwa sana tukaligawanya kwa majaribio pamoja na watoto kwenye masega, na asali pia, baada ya muda wakawa wanaonekana kama wamechoka, tukafikiri labda stress, baada ya kama mwezi hao wakafa na mizinga mingine wakafa pia imebaki michache lakini nao kama wanapungua.

5. Masega yenye watoto wamefia ndani, ambayo hayana watoto masafi kabisa.
 
Hawa wanatembea kwa makundi, ingia youtube search hornet bees uone balaa lao wakivamia mizinga ya nyuki.
Dah! mkuu, hii inaweza kuwa jibu labda inahitaji utafiti Zaidi. Hawa nao hutembea kama kundi au mmoja mmoja, na wanakuwa wanatokea wapi? na ni kwa vipi unaweza kuwatambua na kuwadhibiti?
 
Huku tz sidhani km kuna wale nyuki wakubwa yellow jacket ambao huwaua hawa nyuki wa asali.... Adui mkubwa kwa huku ni siafu na upigaji mbovu wa sumu mashambani
 
Hoja ya Alexander the Great ina point kubwa pia. Niliwahi kuona hili NatGeo, hao nyigu hawafai hata kidogo, wanaua nyuki mzinga mzima ndani ya dakika chache. Hoja yako nayo ina mashiko ya nguvu, hizi dawa za mashambani ni hatari kuliko maelezo kwa kuangamiza nyuki.
 
Huku tz sidhani km kuna wale nyuki wakubwa yellow jacket ambao huwaua hawa nyuki wa asali.... Adui mkubwa kwa huku ni siafu na upigaji mbovu wa sumu mashambani
Siafu wanaweza kuua nyuki? Vipi sisimizi?
 
Dah, kwa hiyo hao nyuki wauaji hata Tanzania wapo sana sio? Ila madawa unaweza kuwa changamoto iliyoenea zaidi
 
Niliona hii teknolojia ya kuzalisha malkia kupitia tv huko tabora sikonge wkt waziri kigwa akigawa mizinga ya nyuki, inafanywa na kitengo cha misitu na nyuki tabora
 
Yap ni kweli kabisa nyuki kama viumbe vingine vinaweza kuzalishwa kwa wingi,kama ilivyo kwa mifugo kama kuku nyuki huweza kuzalishwa kwa wingi zaidi,na wataalamu wabobezi wa nyuki hushauri ni vyema ukazalisha nyuki wako wenyewe ambao wanasifa za kuresist magonjwa kuwa na uwezo wa kuzalisha asali kwa wingi،wafugaji wengi wa nyuki hawajui tasnia nzima ya ufugaji wa nyuki kwa undani na kudhani ufugaji wa nyuki ni jambo LA kawaida na kupata asali ni bahati,kimsingi kinachodhalishwa ni malkia wa nyuki,huyu ndio kiwanda cha nyuki wote kwenye mzinga.sio kazi nyepesi kumdhalisha malkia ,lakini ukiamua in rahisi sana,ikumbukwe malkia hutaga mayai yanayoweza kuwa workers au queen,kama unahitaji malkia basi kuna namna ya kufanya mayai yaliotagwa kutoa malkia tu,kuna chakula spesho unatakiwa kuwawekea malarva ili wawe malkia ,na hivyo kuwa na malkia wengi ambao utawapandikiza kwenye mizinga mipya na hivyo kuongeza uzalishaji wa nyuki

sio rahisi kueleza mchakato mzima hapa,lakini ukipenda ntaleta somo lote lijulikanalo kama "practical queen rearing"

kingine kwa wafugaji wa nyuki hawajui kuwa kupata asali kidogo husababishwa na drone kuwa wengi kwenye mzinga,na hivyo kula asali yote,embu fikiri unafuga kuku halafu majogoo wako 100 mitetea 20,tarajis kupata hasara kwa sababu majogoo watakula Shea ya chakula nyingi huku wakiwa hawana faida ukulinganisha na mitetea,kitaalamu jogoo mmoja kwa mitetea mitano mpaka nane،ndivyo ilivyo kwa nyuki inabidi ukontrol idadi ya nyuki dume dhidi ya nyuki jike, nyuki dume wanahitajika wachache sana kwenye mzinga،kazi yao ni kumpanda malkia tu.

wakiwa wengi hutafuna asali sana na kusababisha mfugaji kupata mavuno kiduchu unapaswa kijifunza namna ya kuwapunguza nyuki ,mzinga unapaswa kuwa na nyuki jike wengi zaidi,kwa sababu ndio huzalisha asali

udhalishaji wa nyuki unahitiji kujitoa kwelikweli kama unajaribu acha kabisa
udhalishaji wa malikia unahitaji vifaa maalumu,mizinga inayotumika kudhalisha malkia inapaswa kutengenezwa kitaalamu na inapaswa kuwa karibu na mfugaji 24 hours wakati wa kupandika mayai kuwa malkia,

ikumbukwe tunadhalisha malkia kwa kuwa ndio kiongozi mzalishaji wa asali
malkia anapopandwa na nyuki dume kutaga mayai yanadestinate kuwa workers na Queen asipopandwa hutaga mayai yanayokuwa drone pekee
 
Salama wakuu,

Nimekuwa nikikabiliwa na changamoto ya nyuki kufa kwenye mizinga kwa sababu ambazo sijazielewa mpaka sasa.

Kwa wazoefu wa nyuki, ni mambo gani hasa yanaweza kupelekea nyuki kufa?
magonjwa ya bacteria,ama wadudu wanaoshambulia nyuki kama simimizi au simba wa nyuki,kagua mzinga wako kouna kama kuna wadudu wasiofana na nyuki ndani ya mzinga,kuna Mdudu anafanana na nyuki sana ila yeye ni mkubwa kuliko nyuki huwaua nyuki sana anapovamia nyuki,ukikuta hakuna Mdudu mvamizi basi ni magonjwa yanayosababishwa na bacteria
 
Sisimizi wanaweza kuua nyuki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…