Ufugaji wa kisasa wa Sungura: Ushauri wa masoko na faida za ufugaji

Jamani wana JF ni kweli kuna aina ya sungura ambayo ina soko sana au ni sungura wa aina yoyote naweza kufuga na nikauza Kama kawaida?

Nataka kuanza kufuga sungura nisije nikachukua mbegu ambayo haina soko

nakuomba fanya mengine mkuu!!inamaana hujaona watu wanalia hawana wa kumuuzia??dah u people
 
Jamani wana JF ni kweli kuna aina ya sungura ambayo ina soko sana au ni sungura wa aina yoyote naweza kufuga na nikauza Kama kawaida?

Nataka kuanza kufuga sungura nisije nikachukua mbegu ambayo haina soko

nakuomba fanya mengine mkuu!!inamaana hujaona watu wanalia hawana wa kumuuzia??dah u people
 
Pole mwanzishaji uzi kwa kutojibiwa swali ulilouliza, Kuhusu Breeds (mbegu) za sungura zimeganyika ktk makundi makuu matatu
1. Small breeds (mbegu yenye umbo ndogo) mfano; Dutch, Angora, Dwarf breeds n.k
2. Medium breeds (mbegu yenye umbo wastani) mfano; Newzealand white, California white n.k
3. Large breed (mbegu kubwa) mfano; Flemish giant, Chinchilla, Germany breeds
Kibiashara yaani kwa ajili ya nyama nakushauri ufuge kati ya Newzealand white, calfornia white au crossbreed ya Newzealand & Calfornia white
Zifuatazo ni sababu kwanini nakushauri ufuge medium breeds rather than large breed rabbit
*Wana mature early 3-4 months ukilinganisha na large breed 8-9 months
*Wanafikia marketing weight ndani ya muda mfupi as mentioned above with carcass average weight (2.5-3kg)
*Most of small breeds wanastahamili joto wakati hizi large breed zina perform well mazingira ya hali ya baridi
*Wanakula small amount of feed.

SUNGURA KIBIASHARA ZAIDI
Kwanza tukubaliane ktk baadhi ya maeneo hapa nchini ufugaji wa sungura ni jambo geni hivyo kupelekea hata ulaji wa nyama yake haupo popular ukilinganisha na nyama ya kuku, mbuzi,ng'ombe.

PIA USIKURUPUKE/USIFUATE MKUMBO UKAINVEST PESA YAKO BILA YA KUFANYA UTAFITI JUU YA MASOKO YA NYAMA NA BIDHAA NYINGINE ZITOKANAZO NA SUNGURA
 
Asante mkuu
 
Nimekuelewa sana, nashukuru
 
Ila kweli, unaweza fwata mkumbo alaf ukaangukia pua
 
Wewe umeshaona wapi mtu anakula sungura?!!
Alafu watakudanganya sungura mmoja 50,000
Chaka hilo!
Fuga samaki.....

Soko la sungura lipo tafuta kampuni ya Namaingo Business Agency watakunganisha na kampuni inayonunua sungura tena kilo
 
Jamani wana JF ni kweli kuna aina ya sungura ambayo ina soko sana au ni sungura wa aina yoyote naweza kufuga na nikauza Kama kawaida?

Nataka kuanza kufuga sungura nisije nikachukua mbegu ambayo haina soko
Wasiliana na Namaingo, hii ni kampuni inayojishughulisha na ufugaji wa sungura.
 
Ni kweli Kuna aina ya sungura ambao wanasoko ila sijui majina yao, watafute Namaingo watakuelewesha
 
Mkuu binafsi nakushauri ufuge mbuzi au kuku wa kienyeji maana soko ni kubwa sana na uhitaji wake ni mkubwa pia, Sungura walaji wake ni wachache mno kiasi kwamba utaweza kukata tamaa mapema na kujiuliza kwa nini ulichukua uamuzi huo wa kufuga Sungura. Mkuu huo ni ushauri tu na jinsi nilivyoonelea.
 
hakuna soko la sungura toka Tanzania ni utapeli tu. niliwekeza sana kuwafuatilia Namaingo hakuna kitu nilipoteza muda tu na pesa. Fuga Kuku, kitimoto, au mbuzi unapenda kufuga.
 
Jamani wana JF ni kweli kuna aina ya sungura ambayo ina soko sana au ni sungura wa aina yoyote naweza kufuga na nikauza Kama kawaida?

Nataka kuanza kufuga sungura nisije nikachukua mbegu ambayo haina soko

Zukisa, napenda nikujibu kwa faida ya walio wengi. Swali lako ni zuri. Kwanza lile tu wazo la kufuga, hiyo ni hatua dhidi ya umaskini. Kwauzoefu, ktk harakati za ujasiriamali, jambo muhimu sana kwa kuanzia huwa ni WAZO. sasa hilo wazo ikiwa kwa bahati mbaya umemshirikisha mtu asiyekuwa sahihi au mwenye allergy na jambo hilo, unaweza kuishia hapohapo usiendelee nalo kumbe mafanikio yako ndo yalikuwa hukohuko. Sungura ni bidhaa adimu, nyama ya sungura ina watu wake wenye uelewa juu ya faida zake. Nyama ya sungura, Kiti moto, kuku, bata, samaki ni white meat (nyama nyeupe), ambayo hivi sasa dunia inageukia kuepuka madhara ya nyama nyekundu. Nataka unielewe vizuri, watu wengi wanapenda kufanya biashara kwa mazoea kwa kuogopa risk hata kama biashara ile faida ni kidogo sana, hawawezi kuona fursa zinazowazunguka na kufanya kitu kipya cha tofauti ambacho pengine kingelipa zaidi. Ndiyo maana utakuta eneo fulani ktk mtaa kuna utitiri wa salon za nywele za kike au za kiume au baa, au workshop za pikipiki, maduka ya vipodozi, shule za chekechea, migahawa, bucha za samaki au nyama n.k. Hawa huishia kugawana wateja na tatizo kubwa hapa ni kukosa ubunifu wa kuanzisha kitu chako cha tofauti. Lakini pia ujue biashara ni matangazo, kama usipowajulisha watu huduma uliyonayo na mahali unapopatikana watajuaje sasa! mfano hapa ulipokuja humu kwa wana JF kuuliza aina ya sungura na uhakika wa soko, kama ndo ungesema unao sungura unauza mimi ni mmoja wa wanaohitaji, pia nigekuletea wateja wa kuwachukua wote ulio nao bandani. Jambo la msingi kama ndo unataka kweli kufuga je, umejiandaaje kimtaji na unalenga soko lipi, ndani au nje ya nchi ama yote kwa pamoja. usibeep yaani watu watakupigia hadi utazima simu. Mtu asikudanganye mtu eti watu hawali sungura! wapo wateja wa jumla na rejareja. Ujasiriamali manake ujasiri. Anza hata na wachache ili ujifunze kisha uongeze maana inawezekana hata kwa mtaji mdogo sana na ktk eneo dogo sana hata kama unaishi nyumba ya kupanga. Ufugaji wa samaki unahitaji mtaji mkubwa ukilinganisha na sungura. Fanya kitu cha tofauti pia usichukue hofu ya walioshindwa ikawa dira yako. Kushindwa ktk biashara kuna sababu nyingi, pia kufanikiwa kuna mbinu nyingi cha msingi ni bidii ya kazi na kutumia ujuzi au watu wenye ujuzi (Taaluma) ili wakushauri kitaalam. Je, unajua kwamba kuna watu hapa Dar wanafuga konokono na wana masoko mazuri nje ya nchi na hapa pia? mji huu wa Dar es salaam hivi sasa una wakazi zaidi ya milioni 5 bila kujumlisha wageni toka mataifa mengine. sasa hii ni fursa penye wengi pana matumbo mengi
 
Jamani wana JF ni kweli kuna aina ya sungura ambayo ina soko sana au ni sungura wa aina yoyote naweza kufuga na nikauza Kama kawaida?

Nataka kuanza kufuga sungura nisije nikachukua mbegu ambayo haina soko
chinchira
 
Hoteli gani uswahilini uliwahi kuagiza "wali sungura?" ukifuga hao wadudu ufuge kama urembo ila kama biashara yatakudodea kama walivyoingizwa mkenge watu wakafuga kware yameishia wapi? fuga vitu vinavyoliwa na watu wengi.

Ukianza na Mtazamo kama huo (Negative attitude) hata ALMASI yenye bei , soko nk hutaweza kuuza.
Zukisa usikatishwe tamaa FUGA SUNGURA . Wajanja hutengeneza soko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…