Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 28,916
- 40,479
Ni hivii, sio kwamba naharibu biashara ya watu, NO.Jamani wana JF ni kweli kuna aina ya sungura ambayo ina soko sana au ni sungura wa aina yoyote naweza kufuga na nikauza Kama kawaida?
Nataka kuanza kufuga sungura nisije nikachukua mbegu ambayo haina soko
Ni kwamba nitastick kwenye ukweli.
Watanzania kawaida yao pale wanapopata habari ya biashara mpya huwa wana tabia ya kukurupuka katika biashara bila kupata uhalisia wa ufanyaji wa tathmini ya biashara hiyo na soko la bidhaa au huduma.
Halafu huwa inakuja kwa msimu.
-Ilianza biashara ya ufugaji wa Nguruwe....wengi wakaongeaaa ila walioweza kuifanya kiusahihi na kifaida ni wachache
-Ikaja biashara ya ufugaji samaki, wengi wakaongeaaa ila asilimia chache sana ndio walioweza kuifanya vizuri.
-Ikaja habari ya kware....wakaongeaaa shida ikatokea sasa watu wanaona mayai ya kuku ni bora kuliko ya kware.
-Ikaja habari ya sungura (na agents wakubwa ni Wakenya) wanaosambaza sana habari za kuwa wanakuletea breed nzuri ya sungura wakubwa, wanakupa na vyakula vyao, wanakutrain na namna ya kujenga banda au wanakujengea kabisa kisha wanakutrain namna ya kuwafuga na wanakuhakikishia kuwa watakuwa wateja wa sungura zako kwa 100%
UKWELI KUHUSU HAWA JAMAA:
Hawa Agents na makampuni yao yaliyopo Arusha na Dar Es Salaam ni WAONGO na hakuna soko la sungura kama wanavyowahakikishia wàtu.
Wakenya wengi wao wanaexport nyama ya sungura Uingereza na Astralia.
Nina ushahidi mkubwa kwani Ndugu zangu wawili wamefuga sungura wengi tu na mpaka sasa hakuna wateja. Na wale walioahidi kununua wamepotea wote.
Ufugaji wa Sungura ni HASARA.
Mkuu umenena,
Kuna kitu kinaitwa Ponzi scheme. Kitu kinapewa dhamani ilhali kwenye uhalisia hakina dhamani.
Na mara nyingi hawa wajanja wanaweka kipindi cha mpito ili wapate muda wa kukufumbaza na baadaye watokomee.
Wanakuuzia mbegu, na ndiyo unakuwa umeliwa. Kuna wachache sana huwa wanafaidika ili kuleta ushuhuda, lakini baada ya hapo ni kilio.